Biashara ya kukodisha tents

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
ndugu zanguni, nimekaa nimefikiria kuhusu uanzishaji wa ka-biashara ka kukodisha Party and wedding tents pamoja na viti (kwa ajili ya harusi, sherehe nyingine, misiba, mikutano etc).. Lengo ni kuwa na tents size (ya kukaa watu kama 20-50) na size kubwa (watu 300-400). Tents hizi nimejaribu kuperuzi mitandao nikaona unaweza kuyaagiza toka CHINA.. na wameshaonyesha nia ya ku-supply.. gharama ya tents zinatofautiana ila nimeona moja 18x30m ambalo gharama inaenda mpaka 10,000 USD FOB (hapo hujaweka usafirishaji na insurance na kodi). Ila kuna supplier ambaye anauza 30USD per sq. meter na kaniambia ukitaka kujua watakaa wangapi inabidi uchukulie kuwa kila mtu anachukua nafasi ya 1.5 sq meter.

sasa wanajamii naomba msaada wenu katika masuala haya:

  1. Je biashara hii inaweza kulipa hapa dar es salaam? je mikoani
  2. Je ni ndiyo, je tents zinazoweza kupata wateja je ni zile kubwa (yaani ya >550 Sq M) au yale madogo madogo ya watu kama 20-50
  3. Je kuna watengenezaji hapa Tanzania? Contacts? gharama zake
  4. Competitors hapa ni akina nani zaidi ya "Maezeki"
  5. je location nzuri ya kufungua ofisi itakuwa wapi- kurahisisha upatikanaji wa wateja
  6. taarifa nyinginezo
natanguliza shukrani
 
mkuu hiyo FOB yake mbona kubwa sana au ni tents za aina gani unataka.Jaribu kutafuta za bei nzuri ili upunguze cost,naweza kukupa ushirikiano kuagiza kutoka Japan kwa bei nafuu.Kuhusu biashara ya tents inaweza kulipa kwa bongo lakini unahitaji kufanya research kwanza.
 
JAY2Dar4: SORRY, nataka kuyaagiza toka China, siyo Japan.. hebu niambie yanaweza kugharimu kiasi gani.. na mimi naona FOB yao ni kubwa nitashindwa kuimudu!!.. natafuta cheap one but mazuri
 
JAY2Dar4: SORRY, nataka kuyaagiza toka China, siyo Japan.. hebu niambie yanaweza kugharimu kiasi gani.. na mimi naona FOB yao ni kubwa nitashindwa kuimudu!!.. natafuta cheap one but mazuri

Kanyagio,mie nimenunua hapa Japan mwezi wa saba kwa matumizi binafsi ni kama mita 5 kwa 6 yenye uwezo wa kubeba watu 15,bei yake ilikua around USD400.Nililonunua yakiwa kama matatu yanatosha kwa watu 50,ambayo bei yake ni around USD1200.Kwa hiyo unaweza kuona utofauti wa bei hapo.Ukiihitaji kutoka Japan tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom