Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

thinka

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
334
148
Video game lounge.jpg

Nataka nianzishe biashara ya kuchezeshaa game aina ya playstastion ila kabla sijaanza inanibd nifanye utafiti kuhusu biashara. naomba kwaa aliye na uzoefu na hilo aniambie faida na hasara zake.


WADAU WANAOHITAJI MUONGOZO KUHUSU BIASHARA HII
Habari wana JF,natumaini nyie ni wazima wa afya.,mimi ni kijana wa miaka 19,nimepata mtaji wa milion mbili kutoka kwa mama yangu,ninahitaji play station 2 kwa ajili ya kufanyia biashara kwani nataka kufungua sehemu ya watoto ya kuchezea games na frem ninayo,nipo moshi soweto na naomba kusaidiwa mwenye details zozote kuhusu mahali pa kuzipata na kwa bei nafuu anisaidie, nakaribisha ushauri pia namna ya kuifanya ili niweze kufaidika na hiyo biashara kwani naamini kuwa hapa ndipo pa kupata mawazo mazuri yatakayoweza kuniongoza vizuri,naomba kama utakuwa huna la kunisaidia basi we pita tu kama hujaona kuliko kunikashifu.

Napenda kuwasilisha mada na Asanteni sana wana JF.
Habarini wanajamvi,

Ebu niende moja kwa moja kwenye mada Mimi ni graduate na kama mnavyo jua saivi hakuna tofauti kati aliyesoma na asiye soma cha muhimu ni kujiongeza tu.

Katika kufikiria kwangu nikaona ni vema nipate maelezo juu ya hiii biashara kabla sijaingia kichwa kichwa vitu ninavyo itaji kujua

  • Vifaaa vinavyo hitajika
  • gharama ya vifaaa ambavyo vinaitajika
  • namna gani ya kuvitumia
  • na technic mbalimbali za kuongeza faida

Kiufupi sina uzoefu ata kidogo na hii biashara ninacho jua mm ni kucheza tuuu napo baadhi ya magemu.

Naombeni msaada ili niweze kuendana na kasi ya hii ya awamu ya tano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wadau,

Binafsi nimepata frame maeneo ya soweto shukrani centre, nina tv za chogo mbili (nilitaka kutafuta flat ila wakanishauri udokozi wa TV za flat upo juu sana kwenye frame za mbeya especially maeneo ya uswahili )na PS 2 mbili, kuna kijana nimempata pia asimamie..

Sasa nilipata vyote hivi standby nimeviweka ila sijajua pros and cons za hii biashara...naomba mwanga kwenye yafuatayo:

  • Nianzie wapi kupata vibali rasmi wa biashara hii
  • Faida na changamoto za biasghara
  • Nipo location karibia na shule, natumai ni soko zuri ,je vipi kuhusu serikali za mtaa kwa walio jaribu hii biashara
  • Mida mizuri ya biashara
  • Ushauri wowote wa kunipa nikiwa nataraji anza hii biashara

Asanteni

MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU
BIASHARA YA KUCHEZESHA GAMES INAHITAJI MAMBO HAYA
Jamani habari zenu wadau.

Najaribu kutoa maujanja juu ya biashara amabayo nimeifanya kwa almost miaka mitatu mfululizo na nimepata mafanikio makubwa. Biashara ya kuchezesha GAMES inahitaji mambo yafuatayo:
  1. Eneo lenye watu wengi hasa kando ya barabara au makazi ya watu wengi..
  2. frame yenye upana wenye hewa kiasi cha kutosha
  3. console (hasa za playstation 3 au xbox 360) kuanzia 3 na zaidi na Televisheni 3
  4. unahitaji pia kuwa maeneo ambayo yana mlinzi wa duka hilo au kama frame iko karibu na nyumbani haina haja ya mlinzi unaweza kuhamisha console kila jioni hasa mida ya kufunga saa mbili usiku...
  5. mtaji wake ni kama mil 2.5 cash..
  6. generator la mchina (in case ya mgao kama sasa hivi)
Console za playstation 3 au xbox 360 ni bora zaidi kwani wachezeshaji wengi wanatumia hizi za kizamani za ps2 ambazo zishapitwa na wakati..na kama ukiongezea na TV zako zikawa ni flat screen inches 21 (hata kama ni za Used) itakuwa bora zaidi kwani itaboresha ubora zaidi wa picha...yaani high definition, pia unahitaji mtu wa kusimamia mradi huo we ukija jioni wakamilisha mahesabu tu

Mradi huu unalipa vipi? kwa kawaida sie huchezesha kwa mtindo wa saa na nusu saa..kwa saa ni 1000 na nusu saa ni 500...na kufungua game center ni kuanzia saa 5 asubuhi wakati watoto wamekwenda shule siku za shule na mpaka saa mbili usiku..na weekend ni saa 3 mpaka saa mbili usiku...ukiwa mahali pazuri na unafikisha mpaka 25,000 kwa siku na inategemea una games nzuri kiasi gani inaongezeka hadi 30,000 (huu ni uzoefu wangu)

Ukija kutoa gharama ya umeme+ gharama ya ulinzi na mengine unabakia na aproximately 750,000 kwa mwezi...assuming umeme haukatiki katiki.

Console moja ya ps3 inapatikana kwa laki 3 mpaka 3 na nusu Zanzibar na Xbox 360 zenyewe ni laki 3 ukiagiza kupitia mtandao wa EBAY na hiyo ni pamoja na gharama ya TRA..

CD za games best way ni kuziagiza nje (used kutoka EBAY ambazo ni gharama ndogo sana ya elf 20 mpaka 25) huku bongo ni elf 70 mpaka laki na nusu madukani...mwenye kutaka kujua zaidi ani PM
FAIDA NA HASARA ZAKE
Nimefanya hiyo biashara mwaka jana. Iko na faida na hasara zake aghalabu changamoto ni nyingi. Kwa kuwa mimi nafanya kazi Zanzibar nilinunua kila kitu hapa.sasa kilichonikuta

Ili bidii nimpatie jamaa yang tv na magem anisafirishie mpaka morogoro mana kazi zilinibana sikupata chance ya kuvisafirisha. Nilimuamin jamaa kwa kuwa yeye ndo kazi zake na ila alichonifanya nimuachie Yehova. Mimi niliamua kuanza na tv tano na ps2 tano.

Kila tv nilinunua 70000tsh@1
Dek za ps nazo 70000tsh@1
Mikono ya ps 9000tsh@1
Flash gb 8 7000tsh@1
Memory za dek 3000tsh@1
Waya sauti 2000tsh@1
Switch cable 30000tsh
@1 zidisha mara 5.
Usafiri inategemea.

Sasa hapa kodi inategemea pamoja na mabench na meza.
Lazima upate maeneo yenye watoto wengi"uswahilini"
Umeme makubaliano yenu. Ukipata luku yako ni mali.

CHANGAMOTO
TV sehemu ya picha na saut isiwe ya kashata.tv itakua inabagua magemu rangi
Magemu ya baiskel na ngumi yanauwa sana mikono(pad).so inabidi uwe mwangalifu.na bei isiwe sawa na magem ya mpira

Kama ukifungua asubuh kuna uwezekano wa kutupiwa lawama na wazaz. Watoto hawaendi shule wanashinda kwenye magemu.

Nimefunga biashara baada ya kuandamwa na wenyeviti wa mitaa nifungue jion.ili vijana wao waende shule.
Magemu ni muda na ukifungua jion hupati faida. Nikashindwa

FAIDA
NIKIFUNGUA MAPEMA NA WATOTO WAKIWA WENGI NAPATA HADI TSH 25000
ENEO NI MUHIMU, WEKA GAMES NYINGI
Biashara hiyo sio mbaya lkn eneo ni muhimu. Pili vifaa kama unachezesha ps2 nunu vidude au mikono ya psone ni migumu kweli, kwenye upande wa tv nunua inchi 28.

CD weka mpira, magari, ngumi.
Jaribu kuweka kitu kama membershp ya duka lako mfano wewe unachaji 1000 kwa saa au miatano, jaribu kuweka kuwa mtu anasajili kwa 5000 badala ya kupata masaa matano anapata saba unusu. Lkn lazima uwe na game nyingi.

Ps3 sio wapenzi sana lkn usiweke zaidi ya moja lkn ps2 imezoeleka na haina hasara kwenye vifaa vyake vikipata kuharibika.
HII BIASHARA INATEGEMEA SANA ENEO ULIPO
Biashara hiyo ni nzuri, ila inategemea na eneo uliopo, ila usisahau kila biashara inachangamoto zake.

Kwa mfano biashara hiyo ya kuchezesha video games, jambo la kwanza la kufkiria ni je eneo uliopo linaruhusu kuanzisha biashara hiyo. Maana kuna baadhi ya maeneo wazazi hawapendelei kabisa kuwepo mabanda ya michezo hiyo, wao huamini inapotosha watoto wao.

Jambo la pili ,uwe na muda wa kutosha wa kuweza kusimamia biashara hiyo
maana ina hitaji si chini ya masaa 12 iwe nafanya kazi kwa siku, yapo mambo mengi ,kama uzoefu wa kuitumia hizo ps, umeme , vifaa kama cds ,pad nk
View attachment 577189

MCHANGANUO WA BIASHARA HII

Mchanganuo wa mtaji wa biashara ya gaming centre

PS3 tatu 1,200,000
CD tatu (FIFA 18) 300,000
tv tatu 500,000
stabilizer 100,000
meza na viti 200,000
CCTV camera 100,000
Leseni 100,000
Chumba miez minne 400,000
usafiri, mchoraji, feni, extension n.k 100,000
JUMLA YA MTAJI 3,000,000

UTOZAJI = MTEJA ITABIDI ALIPIE 2,000 ACHEZE SAA ZIMA AU 500 KWA MECHI MOJA

Faida = mapato - matumizi

Ni muhimu kujua ya kwamba makadirio haya nimefanya kwa dhana ya kwamba matumizi yatakuwa makubwa sana na mapato yatakuwa ya kawaida sana

MAKADIRIO YA KAWIDA KWA MAPATO KILA MWEZI
Masaa 5 * tv 3 * 2,000 kwa saa * siku 30 = 900,000

TOA: MATUMIZI KILA MWEZI
Mshahara wa muhudumu 100,000
matumizi ya mhudumu(chakula,vocha,usafiri) 100,000
tra + ulinzi 100,000
umeme+kubadilisha pads mbovu 100,000
savings ya kodi ya pango 100,000
JUMLA YA MATUMIZI 500,000

FAIDA 400,000/= kwa mwezi
4,800,000/= kwa mwaka

Hela yako itarudi ndani ya miezi 8

N.B: HIZI GAMES NI ADDICTIVE SANA KAMA MADAWA YA KULEVYA, WATOTO WENGI HUDIRIKI KUTOROKA MASHULENI, KUIBA PESA NYUMBANI KWAO AU KUUZA VITU VYA NYUMBANI ILI WAJE KUCHEZA GAME, PANGISHA FREMU MAENEO YA BIASHARA, USIPANGISHA FREMU ZA BEI RAHISI MAENEO YA MAJUMBANI AMBAKO UTAKUWA ADUI WA FAMILIA ZINAZOKUZUNGUKA
MAPATO YAKE SI HABA
Kwa sasa ps4 ndio ina deal. Game pendwa ni fifa. (Unaweza kuwa pia na ps3 ukaweka pes)
Ps4 unaipata around laki 4.5 hadi 7 kwa mtu. Dukani fat au slim ni 800k hadi mil1+.
Tv inch 32 ni laki 350k unapata.

So jumla tuseme:-
Frame 300k
Ps4 1 jumla lak 7+
Ps3 2 jumla lak 70k
Tv 32" 3 jumla laki 9 hadi mil 1+
Cd za games jumla 400k (au kama console zimechipiwa utaweza kuwekewa games kwa gharama nafuu)
Viti na meza laki 150000

Mapato:-
Ps4 dkk 10 mpira tsh 1000 au 500 kutegemeana na location yako.
Ps3 mpira 500

Kwa nusu saa unaweza toza 1000 au 2000 kutegemeana na location yako.

Mapato waweza ingiza 20000+ per day kama mzunguko upo.

So kwa kuanza mtaji hapo utaitajika kama mil 3 - 3.5 unaweza kuanza biashara
(Ingekuwa mimi kwa mil 3.5 ningeanzisha biashara ya kuonyesha mpira kwanza ambapo kwa baadae ndani pia ningefanya hiyo biashara ya games)

Kila la heri.
JIANDAE KWA CHANGAMOTO HII
Jiandae, nasema tena jiandae, narudia tena kwa msisitizo jiandae kweli kweli maana zile pad za kuchezeshea utanunua kila leo maana zinakufa mapema mno na pad moja inauzwa kati ya elfu 10 mpaka 15.

Kila la kheri ni bishara ina vijisenti vya kununulia chumvi nyumbani endapo ukipata wateja wa kutosha, pia games zako ziwe latest mfano sasa hivi tuko PS4 na sio PS2 tena kama zamani.

Ila kumbuka kuwa wateja wako wakuu watakuwa ni wale watoto watukutu wasioipenda shule.

Kwa namna fulani ni biashara isiyopendwa na jamii kwa sababu ofisi yako huwa ndyo chimbo lao la kujifichia na huwafanya wawe wadokozi wa chenji nyumbani pale wakosapo pesa ya kuja kuchezea game!
 
Mkuu kama wewe ni great thinker usifanye hii biashara, naichukia sana, inafanya watoto wawe wajinga sana, Huu utandawazi unawaathiri sana watoto, make wanatoroka shule na kwenda kucheza hizo game, usiangalie tu pesa, au uweke sheria kwamba masaa ya shule hakuna mtoto kusogea hapo.
 
Biashara hiyo sio mbaya lkn eneo ni muhimu,pili vifaa kama unachezesha PS2 nunu vidude au mikono ya psone ni migumu kweli, kwenye upande wa tv nunua inchi 28.

CD weka mpira, magari, ngumi.

Jaribu kuweka kitu kama membershp ya duka lako mfano wewe unachaji 1000 kwa saa au miatano, jaribu kuweka kuwa mtu anasajili kwa 5000 badala ya kupata masaa matano anapata saba unusu. Lakini lazima uwe na game nyingi.

Ps3 sio wapenzi sana lkn usiweke zaidi ya moja lkn PS2 imezoeleka na haina hasara kwenye vifaa vyake vikipata kuharibika.
 
Mkuu kama wewe ni great thinker usifanye hii biashara, naichukia sana, inafanya watoto wawe wajinga sana, Huu utandawazi unawaathiri sana watoto, make wanatoroka shule na kwenda kucheza hizo game, usiangalie tu pesa, au uweke sheria kwamba masaa ya shule hakuna mtoto kusogea hapo,

Hapo sasa inabidi awe anafungua kwanzia sita unusu hadi jioni kwa siku za shule, weekend kwanzia asubuhi.
 
Habarini wadau.

Huku mtaani kwetu kuna ka biashara kanashamiri sana siku hizi kila kona ya mtaa utaona kakibanda ka michezo ya watoto yaani Play Station. Inaonekana kama inalipalipa hivi kwani kila uchao vyaongezeka.

Ombi. Kuna mdau yoyote mwenye kujua juu ya hili ili atushawishi kama ni kabiashara kazuri hasa kina sisi kapuku tujiweze kujihifadhi na maisha haya magumu kila leo?

Asanteni wadau.
 
Na wewe unataka ujiunge katika biashara ya kuharibu akili za watoto?

Sidhani kama inaharibu akili. Zama hizi sio kama zenu zile Big Papa enzi zenu za utoto. Viwanja vingi, Michezo kibao ya kitoto. Enzi hizi hakuna playground za watoto, afu wanazaliwa kwa fujo so i think is a kind of enjoyment to them. Mi naona kama ndo wanakua na akili aktive vile kwani hiyo michezo yenyewe inawafanya wawe very active esp in decission making etc.
Embu niambie inalipa?
 
Ukitaka ufanikiwe kibiashara uwe na passion nayo na uijue vizuri.

Mara nyingi ukiiga biashara kutoka ni ngumu sana. Good luck!

Usisahau ukitaka playstation 3 nitafute nikuuzie na cd zake maana umri umenitupa mikono, mishe za maisha nyingi sana nakosa muda wa kuicheza.
 
Hizi biashara uwa zinawafanya watoto wawe wezi hivyo kama unania njema fanya ruhusa kwa watoto walio juu ya miaka 18.
 
Back
Top Bottom