Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mtu aliekua anakusimamia nae mzinguaji
ANAJITAHIDI SANA .. HAZINGUI HATA KIDOGO !! Kwa mwezi namlipa 70k usiwe mbinafsi kumbana sana maana riziki hutoi wewe anatoa MUNGU ... mtaji wangu nilisha rudisha ndani ya miezi 13 hata zikilipuka zote saivi sina hasara ... kama biashara inajiendesha bila uwepo wako na unapata 15k kila siku inabidi umuheshimu sana anaesimamia biashara yako ...
 
1615730721988.png
 
Biashara moja ya kiboss sana.
Tafuta ps3 tatu na ps4 moja na ps2 moja. Then tv 4 za inch 32 kwaajili ya ps3 nanps4 na tv moja inch 22 flat kwaajili ya ps2.
Chukua kibali ambacho ni 20k kwq miaka miwili. Anza kula faida ya 20k j3 hadi j5 then 30k to 40k alhamisi na ijumaa. 50k jmos na jpili.
Huu ni uongo. Hamna uhalisia hapa.
 
Biashara moja ya kiboss sana.
Tafuta ps3 tatu na ps4 moja na ps2 moja. Then tv 4 za inch 32 kwaajili ya ps3 nanps4 na tv moja inch 22 flat kwaajili ya ps2.
Chukua kibali ambacho ni 20k kwq miaka miwili. Anza kula faida ya 20k j3 hadi j5 then 30k to 40k alhamisi na ijumaa. 50k jmos na jpili.
Mkuu fanya mchangauo wa gharama zote za vifaa ulivyovitaja hapo juu.. tufahamu ! Asante
 
ANAJITAHIDI SANA .. HAZINGUI HATA KIDOGO !! Kwa mwezi namlipa 70k usiwe mbinafsi kumbana sana maana riziki hutoi wewe anatoa MUNGU ... mtaji wangu nilisha rudisha ndani ya miezi 13 hata zikilipuka zote saivi sina hasara ... kama biashara inajiendesha bila uwepo wako na unapata 15k kila siku inabidi umuheshimu sana anae simamia biashara yako ...
Mkuu inamaana wewe ume wekaza zaidi ya 5M
 
Kutengeneza button moja tu ya pad za PS4 sio chini ya elfu 30.
CD ikisizingua tu, moja sio chini ya 120K OG, ku update mashine sio chini ya 30GBs za internet yenye speed kali.

Mkiongea haya mambo ongeeni kwenye uhalisia wake.

Nafanya hii biashara, usipokuwa makini, watu wavuta analogy joyride kama uoinde wa mshale, utajuta.... Zinameguka, spare elfu 60
 
Kwa uzoefu wako, Hasara kwa upande wako ni kubwa kuliko faida ? Umeongea changamoto za msingi kabisa mkuu!
 
Mkuu inamaana wewe ume wekaza zaidi ya 5M
5M nyingi sana!! Mimi mpaka leo sijaweza kuweka PS4 natumia PS3 ... !! Nilichukua TV tatu inch32 kila moja 300,000 kampuni STAR X (duka lampard electronics)kwa hiyo jumla 900k.......

Nilichukua ps3 tatu kila moja 250,000 used (alienipa wazo ndie alieniuzia, aliajiriwa ikabidi aache hii biashara)jumla 750k..
Viti sita kila kimoja bei 20,000 jumla 120K
Bei ya frame 50000 kwa mwaka 600K
Mambo mengine madogo madogo (vifaa vya umeme ..pazia na mengine ) 100K

JUMLA NILITUMIA 2.5M

KWA USWAHILINI HAIJALISHI NI PS3 AU PS4 WAO CHA MUHIMU WACHEZE GAME ... PLAYSTATION NI KAMA SIGARA RAHISI KUANZA NGUMU KUACHA (AKIKOSA PS4 HAWEZI KUSUSA AKAONDOKA WATAOFANYA HIVYO NI WALE WATU WAZIMA WANAOELEWA TOFAUTI YA PS3 NA PS4 ILA HAWA WADOGO CHA MUHIMU WAGUSE PADS)
 
Mkuu uliagiza kenya?
Hapana nilinunu kwa mtu !! ILA KWA USHAURI KAMA NDIO UNAANZA HII BIASHARA ANZA NA PS3 utajifunza mengi sana ukirudisha hela yako ya mtaji .... mapato unayo fata anza kununua PS4 taratibu ... ni pasua kichwa kwenye upande wa PADS .. watoto hawaelewi wanabonyeza tuu hawajali ... sasa pad moja ya ps3 mchina inakaa mwezi mmoja nanunua 15k .. pad moja ya ps4 mchina bei 85k na inaweza isimalize miezi miwili unajikuta unachezea hasara!!
 
Back
Top Bottom