Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,539
755
2348228_Tungi.jpg

Wana jamii jamani hebu nisaidieni.

Nataka kufanya hii biashara ya kuuza vinywaji kwa Arusha inakuwaje?


WADAU WENGINE WANAOHITAJI USHAURI KUHUSU BIASHARA HII
WanaJF habari za Jumapili,

Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo. Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani gin, grands, wine na jamii zake.

Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!

Karibuni kwa ushauri.
Msaada kwa mtu yeyote anaye jua Biashara hii ya Vinywaji vikali na Luxury (mf. wisk na wine) Naomba anieleweshe kwa kina.Mimi nipo hapa Dar na mtaji wa million 5.

Vitu ninavyohitaji kufahaumu kwa kina ni:-

1. Mtaji wa kuanzisha duka la biasahara hii (initial capital.
2. Mazingira yanayo faa kwa Bisahara hii, je ni karibu na bar kama ninavyofikilia mm?
3. Mahali zinako patikana bidhaa kwa urahisi na kwa bei nafuu
4. Utaratibu wa kupata leseni wa hii biashara pamoja na gharama zake
5. Ni bidhaa zipi zinakua na wateja sana hasa zinazofaa kwa kuanzia biashara?
6. Faida na Changamoto zake.
7. Nini ushauri wako kuhusiana na wazo hili na bishara hii?

Natumaini wenye kufahamu zaidi juu ya bishara hii na ni serious people watanisaidia mawazo bora na kujibu maswali hayo hapo juu. Nitashukuru kwa ushirikiano wako.
Habari za muda huu,

Naombeni ushauri nataka kufanya biashara ya vinywaji vikali, nipeni uzoefu.
Habarini wana jukwaa,

Jamani mwenzenu nawaza kufanya biashara ya vinywaji ila sijajua vinywaji gani vinafaida na vinauzika haraka hapa.

Nipo kwenye mchakato wa kutafuta mtaji angalau milioni 1, sasa wataalam wa biashara niambie ni vinywaji gani vitauzika sana kwa wanywaji?


MAJIBU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI KUHUSU BIASHARA HII
Wewe mwenyewe usiwe mnywaji wa kupindukia
Kwa mimi binafsi nilishindwa kuendesha duka la Wines & Spirits kutokana na kuwa ni mnywaji mno, nikaishia kulifilisi flat kabisa! KWAHIYO SITOONGEA NENO!

Lakini ukiwa na nia ya kufungua duka la aina hiyo kwanza ujiridhishe sana na sehemu husika!

Duka la Wines and Spirits linatakiwe liwe strong sana, lakini liwe na system ya surveilance maana mtu akichukua katoni moja ya eg Barcadi au Amarula, then ana uhakika kula siku kadha.

Ni njema kama litakuwa mjini, au eneo lenye constant patrols za wanausalama, hii ni kutokana na Sales zake kuwa za amounts kubwakubwa, na ni rahisi sana kuingiliwa na wajasiriamali wenye mtaji AMBAO NI NGUVU YAO WENYEWE!
Ushauri wa muhimu/ mambo ya kuzingatia

Ufuatiliaji

-Kwanza bei zinatofautiana, mkoa na mkoa. Sasa wewe tembelea Bohari za bidhaa hizo, na kila mkoa na wilaya nchi hii Bohari za bidhaa hizo zipo. Wao watakupa bei ya jumla.

Usambazaji na usafiri

-Kuna taratibu mbili hapa, kuna wale wafanyabiashara wanaofikia kiwango cha kusambaziwa bidhaa, na hii huwa inategemea na mtaji wako na mzunguuko wao wa biashara. Wale wenye mzunguuko mkubwa na mtaji mkubwa kiasi huwa wanapelekewa bure kabisa.

Na wapo wale ambao mtaji ni mdogo sana inabidi wajitegemee usafiri. Muhimu tafuta eneo lenye mzunguuko mzuri.

Uhakiki

Sasa nakushauri kwanza kabisa tembelea makampuni hayo,na ninakushauri bora uende moja kwa moja na sio kutumia kuuliza mawakala, maana kule moja kwa moja utapewa hadi ushauri wa kina, sasa utaamua usubiri mtaji ukue au la.

Mwanzo

Ili biashara unayoanza ili uone faidi yake lazima uwe na mtaji wa kiasi cha kati kwa maisha ya kawaida.Ukianza na mtaji mdogo wote utaishi kwenye usafiri na kulipa kodi.

Mie niliwahi kwenda kwa Bakhresa moja kwa moja headoffice yao,nilipewa Data za maana,mpaka nikasema kweli kuuliza nje kwa watu wa kawaida unakosa mengi ukienda sehem husika unapata kila kitu.Kwanza wanakupa moyo sana na kukupa mbinu na njia zote bila longolongo.Maana nilienda kwa issues za ICE cream.

Mwisho

Kwa ufupi subiri waje wachambuzi humu,halafu chukua ushauri kisha nenda sehem husika moja kwa moja.
Usikatishwe tamaa kimaisha ndugu yangu,na wala usitume mtu nenda mwenyewe,maana kamahuna moyo unaweza kurudia mlangoni.

Kuna siku nilienda sehem kuuliza utaratibu nikakuta mtu anachukua order ya mzigo wa fuso nne,basi mie nilitamani kukimbia.Lakini kumbe kila mtu na uwezo wake hata hao wa fuso nne walianza kwa mzigo wa mdogo tu wa kubeba kwenye Carry.

Maisha lazima ujitoe na kujenga imani kwamba mwenye kumi alianza na moja,basi hapo huwezi kumuogopa mtu yoyote au tajiri yoyote kama ukiamini hivyo.
Hii biashara inahitaji uangalizi wa hali ya juu sana
Nina mdogo wangu anafanya, yeye yupo Kijitonyama na anafanya jumla. Mtaji wake ulikuwa 13 Million, na ana mauzo sasa kwa wastani wa million 1 kwa siku, na faida yake ni 40,000 wastani kwa siku.

Ukiangalia kwa karibu utaona faida ni 4% ya mapato baada ya kutoa gharama za uendeshaji, hii (razor skin margin) ni faida ndogo sana na hatari zake ni kwamba ukienda kwenye mtikisiko wowote ule biashara inakufa.

Ukiangalia urudishaji wa mtaji utaona kwamba anarudisha 10% kwa mwaka hii inaweza chukua muda mrefu sana yeye kurudisha pesa yake.

Ushauri wangu ni kwamba hii biashara inahitaji uangalizi wa hali ya juu sababu ya mzunguko wake wa fedha ni mwingi lakini faida yake ni ndogo sana. Kama unaweza tazama biashara angalia yoyote yenye 10-15% faida baada ya kuondoa gharama za uendeshaji. Biashara hii nafananisha na upigaji tofali zote hizi maumivu makali.

PIA, SOMA:

Ni dhahiri kwamba wajasiriamali wengi wamekuwa wakijiuliza ni njia gani wazitumie katika kuanzisha,kukuza ama kuboresha biashara zao za kuuza vinywaji ili wapate kunufaika na faida kubwa.

Kama wewe pia ni mmojawapo kati ya wajasiriamali wanaotafuta mafanikio makubwa kwa kufanya biashara ya namna hii utakuwa umewahi kujiuliza maswali kama haya;

Je, mtaji wa biashara hii (bar) ni kiasi gani?
Mbona baa ya huyu inalingana na ile kwa mwonekano lakini yule anamafanikio zaidi kuliko huyu?
Nitapajaje wateja wengi kila siku?

Majibu ya maswali yako yote ya kwanini na kivipi ni rahisi tu, zifuatazo ni mbinu zinazoweza kukuwezesha kufanikiwa sana katika biashara yako ya vinywaji au 'BAR'.

1. Fanya Maandalizi ya awali {Weka nia na malengo ya biashara yako (Ni vema Ukiandika)
Ili kufanikiwa katika biashara hii kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote,kitu cha kwanza kufanya ni kuweka nia na malengo au matarajio yako baada ya muda fulani. Kwa mfano, lengo lako la kwanza linaweza kuwa baada ya miezi sita, biashara hii iwe imekuzalishia faida kubwa inayoweza kutosha kuwa kama mtaji wa kufungua biashara nyingine n.k.

Ni lazima pia kuainisha mahitaji yote yanayohitajika kuanzisha biashara yako ikiwemo gharama ya ujenzi, malipo ya wahudumu (kwa miezi sita ya mwanzo), jinsi ya kufanya malipo, Gharama za bidhaa (vinywaji), friji, vyombo na samani za kukalia wateja.

Umakini wa hali ya juu unahitajika katika kufanya upembuzi yakinifu wa gharama za mahitaji ya biashara na muda wa kutosha pia unahitajika ili kupata bei sahihi.

2. Jiandae kiuchumi
Baada ya kufanya maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na kufahamu kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuanda biashara bila mawaa yoyote, sasa unaweza kujiandaa kiuchumi kwa kukusanya taratibu na kudunduliza pesa kwa ajili ya kufungua biashara (bar). Kama pesa ipo tayari ni vema kuihifadhi vyema na kuhakikisha haiingiliani na matumizi mengine.

3. Chunguza eneo unalohitaji kufanyia biashara
Eneo unalohitaji kuweka bar yako linanakiwa kuwa sehemu ambayo imezungukwa na wahitaji wa aina ya vinywaji unavyotaka kuuza. Kwamfano, eneo liwe sehemu ambayo ni rahisi watu kuhitaji kuja kupumzika baada ya kazi au kukutana na marafiki na sio karibu na Makanisa wala Misikiti au eneo lolote ambapo unaweza kuwakera watu wenye misimamo tofauti ya kiimani.

4. Jenga Bar yako kwa jinsi ya kumvutia macho ya mteja (kistarehe)
Wateja wengi hupenda bar yenye mandhari mazuri ya kuvutia macho ikiwa ni pamoja na usafi wake na mpangilio wa counter, maeneo/vyumba vya kunywea na sehemu za starehe nyingine kama 'pool table' na Muziki/Tv. Vyoo pia vinatakiwa kuwa visafi muda wote ili kuvutia wateja kuendelea kuja katika bar yako kila watakapohitaji kunywa.

5. Ajiri wahudumu wenye mwonekano na lugha nzuri ya biashara
Kufanikiwa kwa Biashara kunategemea sana mahusiano kati ya wateja na watoaji wa huduma. Wahudumu wa Bar yako wanatakiwa kuwa wenye mwonekano na lugha nzuri kwa wateja, wasafi,wakarimu na wasiowahi kukasirika wakati wa kuwahudumia wateja. Wahudumu wenye sifa zilizotajwa hapo juu wanafaa na ndio hitaji la wateja wako wengi kama si wote.

6. Hakiki hesabu za mauzo ya kila siku
Unatakiwa kufanya hesabu za mauzo yanayokusanywa kila siku na kufahamu aina za vinywaji vilivyonunuliwa (kila aina kwa idadi yake). Uhakiki wa hesabu za mauzo ya kila siku yatakupa wastani wa mauzo ya kawaida kila siku, kwa wiki,mwezi na mwaka. Yanakupa pia uwezo wa kukadiria mauzo ya chini kabisa (minimum) na mauzo ya juu kabisa (maximum) kwa siku. Hii inakusaidia wewe kuweka malengo na faida unayoipata katika biashara yako.

Ni vizuri kuweka rekodi ya kila mauzo kwa maandishi ili kurahisisha tathmini yoyote inayoweza kufanywa kwa minajili ya kuboresha biashara.

7. Chunguza vitu wanavyopenda na vinavyowachukiza wateja wako
Ni rahisi kufahamu wateja wanapenda nini na wanachukia nini. Kwa upande wa vinywaji,ni wazi kuwa vile vinywaji vinavyowahi kuisha kuliko vingine ndivyo vinapendwa na wateja na inabidi viwepo vingi vya kutosha. Kuhusu ubora wa huduma, unaweza kuongea na wateja wako (wenye busara) moja kwa moja ili kutoa kero zao ili zile zinazorekebishika zirekebishwe maramoja ili kuepuka kupoteza wateja ambao ndio muhimiri wa biashara yako.

8. Epuka urafiki na mikopo kazini
Hii inawahusu wote, wewe mwenye bar, meneja na wahudumu. Biashara nyingi zinakufa au hazizai matunda tarajiwa kutokana na urafiki na mikopo mingi. Katika bar yako ni vema ifahamike kwa wote kuwa Ofa na mikopo isiyo na ulazima sio njia sahihi za uendeshaji wa biashara. Weka taratibu za wazi kuhusu kukata kwenye posho,malipo au mshahara ya mfanyakazi yeyote ambaye kwa uzembe wake mwenyewe au makusudi amesababisha upungufu katika mauzo ya kawaida ya kila siku.

9. Ubunifu na upekee katika biashara ya 'Bar' ni muhimu
Jitahidi kuwa na ubunifu wa pekee ili kufanya biashara yako kuwa tofauti na wengine. Kwa mfano, unaweza kuandaa tamasha dogo la muziki, urembo au vichekesho katika bar yako ambapo kiingilio chake ni kununua ki/vinywaji tu. Huu au ubunifu mwingine wowote utakukuzia biashara yako kwa kasi kubwa kama utakuwa makini kuwa utekelezaji wa ubunifu usigharimu zaidi ya faida unayoweza kupata.

10. Pokea ushauri na maoni kutoka kwa watu wengine
Unatakiwa kuacha masikio yako wazi kwa ajili ya kupokea kila wazo litakalolenga uboreshaji wa biashara yako wa Bar kutoka kwa wazoefu wa biashara ya namna hii au hata washauri wengine. Kuwa makini pia katika kutekeleza ushauri unaopewa kwani si wote wanaokupa uashauri wanakutakia mema katika mafanikio yako na wala si wote wanaokutakia mabaya katika biashara yako.

Hizo njia 10 zikifuatwa vizuri zitakusaidia sana katika biashara yako
 
Mkuu Uko sahihi sana. Mtaji wa vinywaji jumla ni mkubwa sana halafu faida yake ni ndogo sana. labda uuegemee zaidi kwenye pombe kali ndo zenye faida ila nazo ziko nyingi feki. pia ushindani ni mkubwa sana sana.

Hao wakala wanaochukua moja kwa moja kiwandani pia husambaza mitaani kwa bei ambayo angekuuzia wewe ndo ukauze mitaani. cha msingi jitahidi uchukue moja kwa moja kama ni soda bonite au pepsi na kama ni bia basi SBL au TBL hapo ndo utauweza ushindani, otherwise it is very challengin biznez. talking from experience.

Duh! Mkuu unahitaji pesa mingi,na kwa jinsi arusha ninavyoijua l;abda utafute kifaru muungane,cz lazma uwe na kausafiri cha kusupply kwa wateja wako,tena bureee,hapo ndo utapata watu,sikukatishi tamaa, kaza buti
 
Wana JF habari za Jumapili!

Naamini na ntaendelea kuamini kuwa JF ni kisima cha hekima na ushauri na ndio maana naleta kwenu ombi la ushauri juu ya uaanzishaji wa duka la vivywaji vya jumla.

Kimsingi eneo nilipo linauhitaji wa duka la vinywaji vya jumla, baada ya kugundua hilo nimeona nipate ushauri namna ambavyo naweza kuanzisha duka hilo.

Kwa haraka haraka eneo (Location) kwa ajili ya biashara hiyo ipo na ni centre nzuri tu.

Mwenye uzoefu namna ambavyo naweza kuanza biashara hiyo, kiasi cha mtaji , vinywaji kipaumblele, namna ambavyo naweza ku-link na depo za makapuni ya vinywaji hasa kwa mkoa wa (Arusha) kwa ajili ya ununuzi na la msingi kabisa upatikaji wa cret kwa ajili ya kuanzia, namna ya ununuzi wa pombe kali yaani Gin, Grants, Wine na jamii zake.

Kwa mawazo na uwezo wangu nilitaka nianze na cred 100 za beer, 100 za soda, kuhusu vinywaji vikali ntaomba kushauriwa zaidi!

Nashukuru kwa ushauri ambao utatolewa!!

Karibuni kwa ushauri.
 
Sina uzoefu sana na mambo ya biashara lakini pamoja na kuwa umezingatia location, lakini pia angali unatarget nani awe mteja wako kwa mahali hapo.

Suala la crates kampuni za vinywaji wanaweza kukuazima, na pombe kali ukiwa nazo za aina mbalimbali i.e. gin, whisky, brandy, rum, liquer, champagne, nk. itakuwa ni nzuri na bei iwe reasonable.

Kwa maoni yangu labda wadau wengine wanauzoefu na haya mambo watakuelewesha.
 
Wadau salama!

Naombeni mawazo yenu ya kina kabla sijaamua kujikita kwenye hii business.

Je, ni mtaji kiasi gani unaweza kunitosha kufungua duka au store ya vinywaji Kwa jiji la DSM au Mwanza.
Vinywaji kama:-

Whisky
Wine..
Nk ..
Nk..

Naomba pia muongozo kwani sijawahi fanya business hii ila wazo limenijia na nafikilia kuifanya. Naomba tuwezeshane kimawazo kwa wale mliona uzoefu wa mabusiness.

*Natanguliza shukrani*
FL1
 
Kwa mimi binafsi nilishindwa kuendesha duka la Wines &Spirits kutokana na kuwa ni mnywaji mno, nikaishia kulifilisi flat kabisa! KWAHIYO SITOONGEA NENO!

Lakini ukiwa na nia ya kufungua duka la aina hiyo kwanza ujiridhishe sana na sehemu husika! Duka la Wines and Spirits linatakiwe liwe strong sana, lakini liwe na system ya surveilance maana mtu akichukua katoni moja ya eg Barcadi au Amarula, then ana uhakika kula siku kadha.

Ni njema kama litakuwa mjini, au eneo lenye constant patrols za wanausalama, hii ni kutokana na Sales zake kuwa za amounts kubwakubwa, na ni rahisi sana kuingiliwa na wajasiriamali wenye mtaji AMBAO NI NGUVU YAO WENYEWE!
 
hahaha Fidel80 am serious bana ,Bar mie siiwezi kukimbizana na wahudumu
Nipe mawazo najua utakuwa mteja wangu mkubwa ,,,Huduma mpaka mlangoni

Mi ukiniweka meneja kazi itafanyika kwa ufanisi alafu Asprin anakuwa jikoni.

Hapo inategemea na mtaji wako unaweza anza kidogo kidogo huku ukiendelea kuongeza mtaji.

Unaweza anza na creti 200 za bia ili wateja wasikose biya na unaweka mavinywaji yanayo nyweka sana kama mdogo ake safari, mjomba ake safari, binamu yake safari bila kusahau viloba vya kutosha kwa bei ya jumla hayo maBallantines mdogo mdogo
 
Back
Top Bottom