Biashara ya duka la rejareja inahitaji roho ngumu

BradFord93

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
910
2,164
Chanzo kikuu cha maduka mengi kufilisika ni

1. Kodi kubwa ya fremu
2. Gharama za maisha (maana mwenye duka pia ni binadam na ana familia pia kama amepanga chumba ana kodi ya kulipa)
3. Kodi kubwa ya Serikali (wengi huangushwa na hili)
4. MIKOPO dukani (marafiki, ndugu na majirani)

Njia pekee ya kuendeleza biashara ya duka ni kuwatolea imani kuwa wakija kukopa watapata. Yaani wape hofu ya kukopa kabisa.

Mfano mzuri ni jana tu. Kuna mke wa mjeshi alizoea kuchukua vitu halafu hela ni mpaka mumewe akirudi. Kilichonitisha n kuwa nilickia maduka mengne wakilalamika kuwa huwa halipi kwa wakati. Jana kajileta akitaka maji ya lita 12, sikumpa (na nilisubiri mpaka anipe hela yangu).

Mfano wa pili ni rafiki yangu ambaye tumesoma pamoja kuanzia primary mpaka sekondari. Jamaa alkuja kunitembelea tu halafu baadae akatafta chumba jirani na ninakofanyia biashara.

Kila jioni akawa anakuja anachukua kitu cha 600 anatoa 500 (anasema ntaileta, hapohyo itapitiliza wiki) na kuna deni nilimkopesha 2012 mpaka leo hii hajawah hata kukumbushia.

Jana nikasema ngoja nimuoneshe ukatili. Tulipiga story fresh, tumecheka saana. Mwishoni akataka kitu cha 500 akisema hela atoe kesho nilimkazia na hakuamini. Akadhani utani lakini sikumpa chochote.

Kwa wale wanaotaka kuanzisha au wanaofanya biashara ya duka kama wahitaji kuendelea kimaisha

1. Ifanye biashara maisha yako
2. Isimamie ipasavyo
3. Urafiki na biashara vikae mbali
4. Kopesha kama mtu ni muaminifu na kama waona kweli kuna uhitaji wa kumpa(roho ikisita usitoe)
5. Hela ya dukani usitoe hata siku moja hata kama mtu amekuomba kwa muda mfupi
6. Kaa mbali na wanawake(tongoza wanawake wa mbali na wasiojua unafanya ishu gani au wajue unauza duka ila wadanganye location)
7. Roho nyepesi weka pembeni. Binadamu ukimchekea siku ukifilisika atakucheka

Natumaini wale wenye nia ya kufanya biashara ya duka au wenye hiyo bishara tayari tumejifunza kitu.

 
Siyo tu biashara ya duka! biashara yoyote ile inahitaji uzingatie sana uliyoyataja hapo.

Mi nilikuwa na baa yangu, mwishowe niliipiga chini, nilijikuta mtaji unazidi kuisha tu, pesa nyingi ilikuwa kwenye madeni ya marafiki zangu. mfano Mtu anadaiwa 50,000/= analipa 20,000/= sijui utahemea/utanunulia nini bia + vinywaji vingine siku inayofuata.

A Friend is sometimes a source of your decline, be more careful!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo tu biashara ya duka! biashara yoyote ile inahitaji uzingatie sana uliyoyataja hapo.

Mi nilikuwa na baa yangu, mwishowe niliipiga chini, nilijikuta mtaji unazidi kuisha tu, pesa nyingi ilikuwa kwenye madeni ya marafiki zangu. mfano Mtu anadaiwa 50,000/= analipa 20,000/= sijui utahemea/utanunulia nini bia + vinywaji vingine siku inayofuata.

A Friend is sometimes a source of your decline, be more careful!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana ndugu. Marafiki co watu. Mimi huyu rafiki yangu kuna cku aliniudhi ndo maana nkamkazia, alipita dukani tukasalimiana then akachukua keki akala aksema "hii utalipa wew". Nilikasirika kwakweli, ila nkasema ngojea nimuonyeshe upande wa pili nakuaje. Tangu juz nlpomkazia, hajaja mpaka leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha wakati nasoma sekondari, miaka ile maduka mengi ya wapemba. Na ule utaratibu wa kununua mahitaji ya nyumbani ya mwezi mzima haukuwepo, mfano sabuni ya kufulia kila siku lazima mtu aende dukani kununua. Vivo hivyo mchele na harage la jioni.

Sasa siku za jumamosi kuna duka jirani na nyumbani muuzaji alikuwa kijana tuu sikumbuki kabila lake ila alikiwa ananipenda balaa. Kila nikienda dukani nikimpa hela naomba sabuni anachukua sabuni ananipa hela hapokei, nikiendelea kusisitiza achukue hela anachukua hela nyingine kwenye droo ananipa. Nikajua huyu ananipenda ila mie sikumpenda hata kidogo nikaona anafanya vile ili niendelee kukaa dukani pale afurahie kunitizama.

Alivoona simuelewi akamwambia dada yangu mmoja tulikuwa tunaishi nae (mtoto wa baba mkubwa) dada akawa nanituma dukani, Kasie nenda dukani kanunue mafuta ila niombee na halfkeki.

Sikumfilisi duka lake Ila nilifaidi hela ambazo hakupokea nikawa naweka akiba.

Kweli biashara ya duka ni ngumu, yataka moyo.
 
Back
Top Bottom