Biashara ya Dry clean inalipa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya Dry clean inalipa?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by carmel, Oct 2, 2009.

 1. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tafadhali wana jamvi, nauliza kuhusu biashara ya dry cleaning, yani kwa mtu mwenye mtaji basic tu wa kuanzia, ina weza kucost shilingi ngapi? Na pia inalipa? Tfadhali, naombeni mawazo yenu maana sina idea yoyote kabisa.

  Thanks
   
 2. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Assumption - Unaangalia uwezekano wa kuanzisha hiyo biashara Dar.

  Kulipa kwake kutategemea na nguvu za kiasi gani utawekeza kwenye kuiba wateja wa drycleaning ambazo tayari zina majina. Kuna mlolongo wa drycleaning stores jijini ambazo zimeshakamata sehemu na wateja muhimu wa hiyo huduma.

  Hii biashara ni moja ya biashara ambayo soko la ukua polepole sana. Hii ina maana kiwango cha namba ya wateja wapya kujiingiza kwenye uhitaji wa huduma hii ni ndogo sana. Hii inatokana na kuwa, huduma hii bado inaangaliwa kama huduma ya 'anasa' kwa asilimia kubwa ya watu. Kwa hiyo, utakuta asilimia kubwa ya wateja ni hao hao miaka nenda miaka rudi.

  Hivyo basi, ili uweze kufanikiwa, itakubidi usuke mbinu za kuwaiba wateja wa drycleaning zingine. Kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu sana ukizingatia kuwa hizo drycleaning zimekuwa karibu sana kiuhusiano na wateja wao kiasi kwamba ni vigumu kwa wateja hao kuzikimbia.

  -o-o-o-o-o-

  Sasa basi, kuangalia upande mwingine wa shillingi, hii biashara inaweza kufanikiwa kama utajaribu kuongeza upana wa biashara yenyewe. Unachoweza kufanya ni kuweka mashine za self-service.

  Yaani pamoja na kutoa huduma ya drycleaning, pia unaweka washers na dryers kwa wateja ambao wangependa kuosha nguo zao wenyewe. Kitakachotokea wateja watakuja na nguo zao, wataziosha, watazikausha, na kuondoka nazo papo hapo.

  Wewe unachofanya ni kuwachaji gharama za utumiaji wa mashine zako tu. Mfano, unaweza kuwachaji load moja kwenye washer inagharimu kiasi kadhaa, na dyer kiasi kadhaa. Au ukaweka chaji moja kwenye combination ya utumiaji wa washer na dryer moja.

  Vitu vinne muhimu vya kuzingatia kwenye self-service hii ni:
  1) Kuhakikisha gharama za utumiaji wa mashine ni nafuu kuliko za drycleaning.
  2) Kunakuwa na maji na umeme wa uhakika
  3) Kuziweka hizo mashine katika hali ya usafi muda wote
  4) Kuna usimamizi wa utumiaji wa hizo mashine ili zisiharibiwe na waharibifu

  Well, ningependa kugusia suala la maji na umeme. Kama hii huduma ikichanganya, basi ujue kuwa itakugharimu maji na umeme zaidi kuliko kodi ya fremu. Kwa hiyo itabidi ujiandae vilivyo kwenye hivyo vitu viwili. Na kama unavyojua, maji na umeme ni matatizo sugu ambayo yako kwenye top 5 nchini mwetu. Na hiyo biashara bila ya hivi vitu viwili haiendi. Unajua hilo! Kwa hiyo, utakubidi uweke matanki na jenereta za kutosha.

  Pia, itakubidi uwe mwangalifu kwenye suala la usafi wa maji. Kama unavyojua, maji ya dar ni maji tope. Kwa hiyo, ili usijekujikuta na lundiko la malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu nguo zao kuchafuka zaidi (badala ya kusafishika), itakubidi utafute njia ya kuya-filter hayo maji. Nafikiri wizara ya maji ina ma-engineers ambao wanaweza kupatia mbinu ya ku-filter maji.

  ~~
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Umeme na maji ni issue hapo,Biashara yeyote TZ inayotegemea umeme kutoa product zake ni ngumu sana kufanikiwa...ndio maana bila umeme wa kuaminika na bei nzuri maendeleo nchi ile ni ndoto maana kila kitu kinategemea umeme!
   
 4. m

  majogajo JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hii bness inalipa sana ukiwa maeneo ya mgodini, si unajua wale jamaa baada ya shughuli nguo zao zinavyokua?
   
Loading...