Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

MzungukoMnangani

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
303
81
32ce772bb33ee4c64023c0dc30d0f08a.jpg


Poleni na majukumu wadau, me naomba kwa yeyote mwenye uzoefu wa biashara ya dagaa (wakavu) wa mwanza kupeleka Dar, naomba kujua gharama za kununulia kwa wavuvi, gharama za kuwakausha pamoja na usafirishaji, soko lake na mtaji wa kuanzia na yote yanayohusu biashara hii.

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU BIASHARA HII
Wakuu nimesikia watu wanatengeneza hela kwa kufanya hii biashara, so nadhani na mimi nilikua nataka kujua deep zaidi inakuwaje hasa advantages and Disadvantages? Kwanza kabisa najuwa humu ndani wazoefu na kuna watu wa kila aina so sidhani kama itakuwa vibaya tukishauriana wakuu.

1)Kwanza kabisa kiasi ambacho unaweza kuanzia kwa biashara kama hii kuanzia milioni ngapi ambapo utanunua mzigo wa kutosha?

2)Sehemu ya kuuzia zikitoka Mwanza na kufika Dar, Je sehemu zipo ambapo zinaweza kuuzikana kwa ujumla I mean Soko?

3)Je kuna faida gani na hasara gani katika kuzisafirisha na njia ipi ya usafiri ni njia nzuri zaidi

Wakuu kwa haraka haraka nadhani hayo ni ya muhimu kwa sasa nadhani itakuwa vizuri zaidi wengine kama watakuja na idea au maswali mengine na tukapata majibu zaidi.

Nawakilisha
Mimi ni kijana wa miaka 26, baada ya kumaliza kusoma kitabu cha “Rich Dad Poor Dad” nakumbuka nilikuja na uzi wa kuahidi kuyafanyia kazi yale yote niliyojifunza kutoka kwenye kitabu kile.

Basi nilianza kufanya saving za hapa na pale mpaka sasa nina laki 4 na elfu 32, wazo la biashara nililokuwa nalo toka muda niliplan kufanya biashara ya dagaa wa kukaangwa kutoka mwanza kwenda Dar so jana nilipata nafasi ya kwenda pale ferry kuuliza bei na vitu kama hivyo.

Ndoo ya dagaa wa kukaangwa ni elfu 65, boksi la package ni elfu 1500, kutoka pale ferry mpaka nata kwenye mabasi ya zuberi ni elfu 1000 kwa boda boda, kusafirisha mzigo kuanzia debe moja ni elf 10000 hadi 15 elfu. Sasa hapa najiuliza mimi uko Dar nitauzaje hao dagaa ili kufidia hizo gharama na nipate faida?

Dar es salaam bado sijafanya utafiti wa soko lenyewe hapa si naenda kuangukia pua wakuu? Nimetoka kusoma ule uzi wa hasara gani umepata kwenye maisha yako ndo nimeishiwa nguvu kabisa.

Naomba mtu mwenye uzoefu wa hii biashara aniambie kwa mchanganuo huo wa gharama naweza vipi kupata faida nikija kuuza Dar au kama nitaangukia pua mniambie mapema, kitabu Kimenifunza kutake risk lakini mmmh.

Nb. Mimi makazi yangu yapo Dar so ni mwenyeji sema Mwanza nipo kwa muda huu.
Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Nina mpango wa kufanya biashara ya dagaa wa kukaanga wa Mwanza niwe napaki kwa vipakeji nasafirisha mikoa hii Dar na Moshi Ila sina uzoefu.

Naombeni kujua changamoto na je ni lazima nikatie kibali mtaji wangu ni wa laki tu nisaidieni njia za kufikia lengo.
Mimi ni kijana niliyeamua kuongeza kipato kwa njia nyingine bila ya kutegemea ajira.

Wazo lililokuja kichwani mwangu ni kuuza dagaa wabichi waliokaangwa kutoka mwanza. Maana huku niliko(mbeya) zinapatikana kwa uchache sana.

Nahitaji msaada wenu kwenye mambo haya;
1. Dagaa hawa kwa pale mwanza wanapatikana wapi?

2. Bei yake kwa vipimo mbalimbali kama sado na ndoo ni shilingi ngapi?

3. Naweza kupata mtu wa moja kwa moja kutoka hapo ziwani bila kufanyiwa udalali wowote?

NB: Nina mtaji wa shilingi laki moja na nusu tu nina imani itatosha

Naombeni mnisaidie mawazo yenu sana sana kwenye hayo maswali matatu hapo juu.

Ahsante.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Habari za majukum wakuu,

Nimeamua kuanzisha uzi huu ili kupeana changamoto, motisha, ujanja , locationa ambazo dagaa wanapatikana kwa wingi na rahisi zaid, uandaaji ili zikae na shape nzuri kwa muda, pamoja na idea nyingine zinazohusiana na biashara hii.

Binafsi nimeamua kuanza kufanya hii biashara na nimejikita kwenye kuuza dagaa wa mafuta(sio dagaa mchele) kutoka Mwanza. Ninauza kwa jumla na rejareja japo mwanzo nilijipanga kuuza jumla tu lakini changamoto za wateja wa jumla kupenda kulalia wafanya biashara wapya ilinifanya niamue kuuza reja reja pia kuliko kuwategemea wao.

Changamoto mpya kwa sasa naona ni bei ya mafuta ilivyo panda, wateja wengi wanafahamu ilo lakin wanataka kubaki kupokea mizigo saizi zile zile kwa garama za zamani pia.

Natamani kujua bei za sehemu mbalimbali kwa wauzaji, mnauza kwenye Range ipi, na wanunuaji pia mnaweza tupea uzoefu mnanunuaje

Kwa mikoa ya kaskazini bei ina Range kutoka 32k -42k (inaweza pungua zaid au kuzid) kwa debe.

Kwa wanao hitaji Dagaa pia ni Dm nikupe mawasiliano

Karibuni wadau

MAJIBU/MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA
UZOEFU NA USHAURI

Ni muda wa Miezi Mitano sasa Toka nihitimu Chuo pale Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino (Mwanza) Tawi kuu. Namshukru Mungu nkapata Degree yangu ya Kwanza ya Falsafa na Elimu, lakini kwa kipindi chote hicho mpaka Sasa hivi nafanya Temporary work kwa Rafiki yang kipenzi (Boss Fulani) mmiliki wa Magari kadhaa ya mizigo na Mnunuzi wa Tani za Dagaa kutoka mikoa ya Mara na Mwanza.

Kiukweli Nje ya Business ya Magari ya Mizigo (Semi - Trailers) especially Scania R 420 , 114 n.k Jamaa hyu Business ya Dagaa inamlipa Sana kuliko Magari na pia sisi kama wasimamizi wake Maisha yanaenda japo kazi Ni Ngumu ila masilahi yapo.

Biashara hii Dagaa hufanywa kwa kuchukua Dagaa kutoka huku na kupelekwa Dar, Congo, Tunduma, Arusha na kwingineko na inalipa Sana ukizingatia yafuatayo, Mtaji, Soko, Muda wa kusimamia na juhudi na watu (Social capital), n.k

Mimi kesho na kesho na kesho ntaka Nijipange na nianze Mdogo mdogo. Karibuni Musoma karibuni Kwenye Dagaa. Tafadhali Mchanganuo kama ifuatavo; Dagaa inayonunulia ni Dagaa chafu (Chakula ya kuku) na Dagaa safi Chakula ya Binadam

1. Chakula ya kuku Inauzwa kwa Dumu yaani ndoo ya Litre 20 , Mara nyingi dagaa hii ya Chakula ya kuku huuzwa kwa Tsh. Elfu 10,000/= mpaka Elfu sita na Mia Tano kwa Kama Dagaa imepatikana nyingi Sana bei yake hususha Automatically Kwan kwenye Masoko Hufurika Sana.

UANDAAJI Chakula ya kuku huandaliwa kwa kuwekwa kwenye Gunia kubwa ambapo Kila gunia hubeba Dumu 21 na @ Gunia likipimwa hutoa kilo kuanzia 120- 95.

USAFIRI Baada ya kuandaliwa na kuwa tayari hupakiwa kwenye Magari ya mizigo na kupelekwa Kwenye Masoko kama vile Dar, Congo,Tunduma, Arusha n.k . bei ya Usafiri Inategemea Mzigo Wako na PIA Maelewano na Mwenye Gari lakini kama Semi- Trailer lenye Contena Kama vile Scania R420 Mara nyingi hubeba Gunia 270 na hapo hutegemea upakiaji WA Makuli husika na bei hapa Kwa Gari huwa Ni one million and point six 1,600,000/=

BEI kiwandani dagaa hizi huuzwa kwa kilo ambapo Kilo Ni 3500- 2500 Inategemea Upatikanaji wa Bidhaa na Kiwanda husika.

Kwa hyo gunia lenye Dumu 21, Na lenye Thamani ya Tsh. 210,000= na Gharama ya 25,000 Uaandaji usafiri , ushuru na Mengineyo na lenye kilo 120 Ambapo @ kilo 3500- 2500.

Hapo ukipiga Hesabu utakuta kwamba ni
120*3500= 420000
420000- 235000= 185000
Au 95*2500= 237500 Kama Dagaa umeinunua kwa bei nzuri na umebana Mapato saswa Sawa.

MASOKO
kwa Dar ndo habari yake Kwan ndo Viwanda vingi vya Chakula ya kuku hupatikana Hasa kwa Falcon, Kitunda kwa Matinde few to mention just Na hapa kwenye vizuri kufatilia mwenyewe kuepusha madalali na matapeli WA mujini , Nakaribisha Kitu Maswali, Matusi,Kejeli na Mengine.

MAWASILIANO

KARIBUNI MUSOMA KWENYE DAGAA WA CHAFU (CHAKULA YA KUKU)
UPATIKANAJI WA DAGAA MUSOMA NA CHANGAMOTO

1. Kwa Hapa Musoma Dagaa inapatikana Sana Maeneo ya Mwigobero kwani ni sehemu ambayo Dagaa uletwa kutoka Sehemu Mbali mbali na Kuja kuuzwa hapa.

2. Uhakika upo Kwan Huletwa kutoka Maeneo Tofauti

3. Zitatapatakana na itachukua Siku Mbili Semi ya Tani 29 Ni sawa na Dumu 2000 Ambazo naweza kuzipima kwa siku mbili au Tatu kama Dagaa imepatikana Sana

3. Muda ambao Dagaa chakula ya kuku hukaa zaidi ya Mwezi mmoja kabla ya kupelekwa kiwandani na PIA hutegemea aina ya Dagaa uliyonunua Cha msingi iwe chakula ya kuku ila yenye ubora isiwe na konokono Sana, Furu wengi Sana au isiwe ile size ndogo Sana Kwan ya aina hii ikikaa muda Fulani inachange color na kuwa red Sana.

4. Haaa Haaa Changamoto hapa ndg yangu ni nyngi Sana kwanza FITINA baina ya wafanya biashara , Uchawi lazima uwe nao WA kutosha, kubadilika kwa upepo ambao unaweza kuathiri upatikanaji mzuri wa Dagaa lakini hii utegemea miezi Fulani example June, July na August kidogo.

Na Dawa ya hizi Changamoto Ni wewe Mwenyewe Kwanza namna unavoongea na wateja Wako na PIA wewe unajiwekaje ( Personality) kwanza, Mimi Hapa Mwigobero ni Mzoefu Mpaka Sasa Nina Miaka Minne niko Hapa Toka Nimalize Form Six Nkaja hapa kusimamia Ushuru wa mjomba nkapata Marafiki wafanyabiashara nimekua nikisoma Chuo nikpata likizo nakuja npaga kazi napata pesa ya kurudia Chuo kwa huu muda nimebahatika kujenga mahusiano mazuri na watu wote hapa Degree yangu ya Falsafa na Elimu kutoka Saint Augustine iko kichwani na sio mdomoni.

Sina kujiona wala kujisikia kwa lolote napiga kazi zote Kuanzia kusimamia mpaka Kutwisha makuli mizigo huku Nikisubiria Baba Magufuli Rais wetu apige kipenga vijana tuingie J.K.T au Tukapige Chalk afu Mimi nchecke na CRDB, EQUITY AU NMB nikope nije huku tena.
USHAURI: MTAJI, FAIDA NA USIMAMIZI

Nitatoa maelezo kulingana nauelewa wangu na uzoefu wangu japo si sana.

Kuhusu mtaji
Mtaji unatofautina kulingana na uwezo wa mtu as wapo wenye mitaji midogo na mikubwa! Wapo wanaoanza ata na laki 2 na kuendelea na wapo wasafirisha kupeleka huko Mtwara, Tunduma adi congo lakini hao ni wenye mitaji mikubwa na pia inahitajika uwe na soko ambapo ukichukua mzigo unajua utapeleka wapi nautakua ni kiasi gani cz huwezi kuchukua tu mzigo na kusema napeleka dodoma itakula kwako cz watu wengi wanakua wanachukua mizigo kwa oda na pia kulingana na soko alilonalo.

Kuhusu faida
Kiukweli dagaa inafaida tena nzuri tu sema inategemea na ukubwa wa mzigo na ubora mda unaokua umetumia kuanzia kununua, kusafirisha adi kuuza na pia wanaochukua mizogo mikubwa hua wanakua na faida kubwa na pia faida inatofautiana kulingana na mzigo uliochukua na bei ya soko unapouzia as bei zinatofautina sehemu na sehemu cz bei ya dom na Dar ni tofauti kabs kadhalika na masoko mengine.

Kuhusu uzimamizi
Usimamizi unahitajika sana hasa wakati wa ununuaji wa mzigo cz ndo wakti unapotakiwa kuangalia ubora wa mzigo nikimaanisha wa wawe wamekauka vizuri, wasiwe na mchanga mwingi na pia!! Usimamizi unahitajika wakati wa kupakia mzigo kwenye gari as mpakiaj anatiwa ahakikishe anamkabidhi dereva au mpakiaji kwa maandishi pia inatakiwa mpokeaji ajulikane na unakabidhi mawasiliano yako!!!! Vikwzo vipo kwenye sana kwenye kupata mtu mwaminifu ambaye unaweza kufnya nae kazi na pia mchanga hua unasumbua saaana.

Kwa maelezo hayo machache ni matumaini yangu kua mtakua mmepata mwanga na pia kama yupo mwenye maelezo ya tofauti au nyongeza anakaribishwa.

Kwa maelezo ziada kama bado unamaswali namba yangu nimeshaitoa call me me any time.

Karibuni
USHAURI: KAMA HUJUI PA KUANZIA USITEGEMEE FAIDA YA HARAKA

Habari ndugu. Hongera sana kuingia katika ujasiriamali. Hakuna tatizo kusoma vitabu sababu unaongeza elimu. Ila ukweli nikuambie kwamba waandishi wa hivyo vitabu wako kimaslahi zaidi. Huyo mwandishi wa hicho kitabu Kiyosaki anaitwa, yeye kampuni yake inayotoa hivyo vitabu ilifilisika na hadi aka-file bankruptcy. Sasa jiulize mtu anayeshauri vizuri anafilisikaje kama sio uongo tu kaandika.

Kiukweli kujua biashara ni kuifanya. Na utakapoifanya ndio utajifunza. Umetaka faida, napenda kukupa habari mbaya kwamba usitegemee faida hadi baadaye sana kwa hio biashara sababu umeshasema hauna soko na haujui pa kuanzia. Manake utafanya makosa mengi kwanza ya kujifunza ambayo yataleta hasara hadi ukipata mfumo mzuri ndio utapata faida. Kwa hio kama lengo ni faida sasa hivi, tafuta biashara unayoijua vizuri sana, na ambayo tayari una wateja ndio uanze nayo hio. Manake tafuta wateja kwanza kabla ya kuanza. Kama ni dar, usinunue bidhaa tafuta wateja wa uhakika kabisa kabis, ndio upeleke bidhaa upate hela yako. Hongera tena. Ujasiriamali ni mzuri sana, lakini mwanzo una changamoto nyingi.
 
Ha ha ha haa, kaka hilo jina lako, ngoja na mimi nijiite MZUNGUKOLUCHELELE
 
Kaka dagaa ukitaka kumpata nenda ktk visiwa vya ukerewe au sengerema hata bukoba na musoma pia utakuta wavuvi wanavua wakitoka huko huwaanika juani wakikauka majira ya mchana huwauza kwa wafanyabiashara kwa gunia ni sh,40000- 60000 au pungufu ya hapo na baada ya kutimiza mzigo wako husafirishwa kwa meli au mashua mpaka mwana na bei ya kusafirisha gunia ni sh, 2000 hadi mwanza na baada ya kufika mwanza ndo unafanya utaratibu wa'kusafirisha kuwapeleka dare es salaam umenipata.
 
Kusafirisha ni 1Mil/1.5 Mil kwa tani 10/15, kifupi ni rahisi sna kwa kuwa mwanza magari mengi yanarudi tuou hakuna mizigo wala mazao huko ya kuja jijini.
 
kaka dagaa ukitaka kumpata nenda ktk visiwa vya ukerewe au sengerema hata bukoba na musoma pia utakuta wavuvi wanavua wakitoka huko huwaanika juani wakikauka majira ya mchana huwauuza kwa wafanyabiashara kwa gunia ni sh,40000- 60000 au pungufu ya hapo na baada ya kutimiza mzigo wako husafirishwa kwa meli au mashua mpaka mwana na bei ya kusafirisha gunia ni sh, 2000 hadi mwanza na baada ya kufika mwanza ndo unafanya utaratibu wa'kusafirisha kuwapeleka dare es salaam umenipata

Shukrani ndugu ngoja kesho nitembelee maeneo ya Sengerema
 
Wakuu nimesikia watu wanatengeneza hela kwa kufanya hii biashara, so nadhani na mimi nilikua nataka kujua deep zaidi inakuwaje hasa advantages and Disadvantages?? kwanza kabisa najuwa humu ndani wazoefu na kuna watu wa kila aina so sidhani kama itakuwa vibaya tukishauriana wakuu.

1)Kwanza kabisa kiasi ambacho unaweza kuanzia kwa biashara kama hii kuanzia milioni ngapi ambapo utanunua mzigo wa kutosha??

2)Sehemu ya kuuzia zikitoka Mwanza na kufika Dar, Je sehemu zipo ambapo zinaweza kuuzikana kwa ujumla I mean Soko???

3)Je kuna faida gani na hasara gani katika kuzisafirisha na njia ipi ya usafiri ni njia nzuri zaidi

Wakuu kwa haraka haraka nadhani hayo ni ya muhimu kwa sasa nadhani itakuwa vizuri zaidi wengine kama watakuja na idea au maswali mengine na tukapata majibu zaidi.

Nawakilisha
 
Biashara ya dagaa inahitaji umakini mkubwa sana. Usipokuwa mwangalifu, kuna uwezekano mkubwa sana wa pesa zako (mtaji) kuuacha Mwanza! Madalali wa kuuza dagaa Mwanza sio waaminifu. Kwanza wanachakachua uzito wa kilo za dagaa kwa kuchanganya michanga.

Vilevile soko lake huku Dar lina-fluctuate sana. Bei ya kilo ya dagaa inabadilika mara mbili au tatu ndani ya wiki moja. Hivyo ushauri wangu wa bure: tafuta biashara nyingine ya kufanya kuliko kuingia hasara kwenye dagaa.

Unaweza kuni-inbox if u need more clarification
  • Dagaa mza zinanuliwa SOKO LA MWALONI, KIRUMBA
  • Dagaa dar zinauzwa K'koo na ktk masoko mengineyo jijini japo madalali ndio wamekamata soko

- Endapo ni dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku, wasiliana na FALCON, maeneo ya Tegeta; falcon ndio wasindikaji wakuu wa chakula cha kuku hapa Dar.

Goodluck!
 
Biashara ya dagaa inahitaji umakini mkubwa sana. Usipokuwa mwangalifu, kuna uwezekano mkubwa sana wa pesa zako (mtaji) kuuacha Mwanza! Madalali wa kuuza dagaa Mwanza sio waaminifu. Kwanza wanachakachua uzito wa kilo za dagaa kwa kuchanganya michanga.

Vilevile soko lake huku Dar lina-fluctuate sana. Bei ya kilo ya dagaa inabadilika mara mbili au tatu ndani ya wiki moja. Hivyo ushauri wangu wa bure: tafuta biashara nyingine ya kufanya kuliko kuingia hasara kwenye dagaa.

Unaweza kuni-inbox if u need more clarification
  • Dagaa mza zinanuliwa SOKO LA MWALONI, KIRUMBA
  • Dagaa dar zinauzwa K'koo na ktk masoko mengineyo jijini japo madalali ndio wamekamata soko

- Endapo ni dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku, wasiliana na FALCON, maeneo ya Tegeta; falcon ndio wasindikaji wakuu wa chakula cha kuku hapa Dar.

Goodluck!

Nashukuru sana mkuu wangu kwa msaada wako na mawazo yako mazuri na ya maana, yeah nitakucheck tuongee vizuri zaidi kaka wala hamna tatizo kabisaa.
 
Kama uko na mawazo ya kufanya biashara ni bora ukaifanya wala mtu asikuogopeshe na ww ukaacha kufanya mjasiliamali hatakiwi kuogopa kufanya kitu cha kufanya ni kuangalia hizo risks alizozisema mdau hapo juu kuna kipindi kama mwezi umepita, nilitembelea Kilosa nikataka kwenda porini hivyo ikanipasa kununua baadhi ya vyakula pale mjin,nilistaajabu kukuta bei ya kilo moja ya dagaa iko sawa na kilo moja ya nyama kwa Dar.

Kwa huko nyama iko chini kidogo zaidi ya dagaa hao wa Mwz hivyo inaonekana soko lake ni zuri sehemu hizo ingawa sikufanya utafiti wa kutosha sana ila nilizunguka sokoni na nikakuta bei iko juu zaidi ya nyama hivyo kama kweli uko tayari unaweza ukafanya utafiti wako katika hiyo biashara ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko maeneo hayo sio kila bidhaa lazima iende k/koo mdau hata maeneo mengine kuna masoko mazuri tu cha msingi ni ujasiri na kutokata tamaa.
 
Kama uko na mawazo ya kufanya biashara ni bora ukaifanya wala mtu asikuogopeshe na ww ukaacha kufanya mjasiliamali hatakiwi kuogopa kufanya kitu cha kufanya ni kuangalia hizo risks alizozisema mdau hapo juu kuna kipindi kama mwezi umepita,nilitembelea Kilosa nikataka kwenda porini hivyo ikanipasa kununua baadhi ya vyakula pale mjin,nilistaajabu kukuta bei ya kilo moja ya dagaa iko sawa na kilo moja ya nyama kwa Dar

Kwa huko nyama iko chini kidogo zaidi ya dagaa hao wa Mwz hivyo inaonekana soko lake ni zuri sehemu hizo ingawa sikufanya utafiti wa kutosha sana ila nilizunguka sokoni na nikakuta bei iko juu zaidi ya nyama hivyo kama kweli uko tayari unaweza ukafanya utafiti wako katika hiyo biashara ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko maeneo hayo sio kila bidhaa lazima iende k/koo mdau hata maeneo mengine kuna masoko mazuri tu cha msingi ni ujasiri na kutokata tamaa

Asante sana mkuu wangu na nashukuru sana kwa mawazo yako na kuwa open zaidi, yeah ni kweli kabisa na wala hujakosea biashara ni ujasiri na kuwaa na nia na kiu ambacho unataka kufanya ndio muhimu zaidi, so yes nitafatilia zaidi hizo sehemu, je una hint ya sehemu zingine uziweke hapa wazi mkuu?

Pamoja sana.
 
Saluti kwenu wanajamvi,

Mimi nipo Mwanza na ninafanya biashara ila ndo nimeanza na huwa nasafirisha kupeleka Dar na kwa sasa nataka kujipanua, natafuta soko Singida, Dodoma au Tunduma.

Kwa yeyote anayehitaji nipo tayari kufanya nae kazi au hata kunisaidia kupata soko hayo maeneo niliyoainisha! Yeyote ambaye yupo tayari ani PM! Pia ushauri na nk unakaribishwa.

Naomba kuwasilisha
 
mpambanaji1

Mkuu habar za majukumu,
Heri ya mwaka mpya..

Nilikuwa nafikiria kufanya biashara ya dagaa yaaniniwatoe wanapopatikana niwapeleke mtwara au niletewe huko japo mwenyewe naishi dar es salaam.

OMBI:
Naomba maelekezo,
1: Nahitaji mtaji kiasi gani ili kuanza biashara hiyo?
2: Vipi kuhusu faida katika biashara hiyo.
3: Kuhusu usimamizi wake (vikwazo vipi nitakumbana navyo)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu habar za majukumu,
Heri ya mwaka mpya..

Nilikuwa nafikiria kufanya biashara ya dagaa yaaniniwatoe wanapopatikana niwapeleke mtwara au niletewe huko japo mwenyewe naishi dar es salaam.

OMBI:
Naomba maelekezo,
1: Nahitaji mtaji kiasi gani ili kuanza biashara hiyo?
2: Vipi kuhusu faida katika biashara hiyo.
3: Kuhusu usimamizi wake (vikwazo vipi nitakumbana navyo)

Mkuu za majukumu ni njema tu na heri ya mwaka mpya pia mkuu! Tena mkuu huko Mtwara ndo kwenyewe kabisa kama unauhakika wa soko na unamtaji wa kutosha embu tuwasiliane ili tuongee kwa undani zaidi naona ndo itakua njia rahisi ili uweze kupata maelezo ya kutosha!
 
Mkuu za majukumu ni njema tu na heri ya mwaka mpya pia mkuu!! Tena mkuu huko mtwara ndo kwenyewe kabisa kama unauhakika wa soko na unamtaji wa kutosha embu tuwasiliane kwa namba hii 0713 470 536 ili tuongee kwa undani zaidi naona ndo itakua njia rahisi ili uweze kupata maelezo ya kutosha!

Mkuu ungetumwagia hapa tukafahamu hasa hasa maswali aliyokuuliza mkuu isack, otherwise kila mtu atakuwa akikupigia simu unatoa maelezo upya.
 
Ndugu weka mambo hadharani kila mtu ajue tuweze kufanya biashara, mimi nipo Mbeya
 
hiv mkuu je wale wakukaanga naweza kuwapa?

Hawa unaweza kuwapata lakini ni lazima uweke order sio kwamba unawakuta! kama vipi nipe order na offer yako ya kilo moja iliyokaangwa tuanze mwaka!
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom