Biashara ya bucha la samaki, nyama na kuku naweza kupata 60,000/= kama faida kwa Dar es Salaam?

jooohs

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
2,054
8,547
Ndugu wana JamiiForums nimekuja kwa mara nyingine kuomba ushauri kuhusiana na biashara ya bucha. Huu mwaka ni mpango wangu wa kuongeza biashara nyingine ili kukabiliana na ukali wa maisha.

Ukiachilia mbali biashara ya nafaka ambayo hadi muda huu nakomaa nayo wazo la kwanza nililokuwa nalo ni kufungua biashara ya bucha, upande mmoja ni dili na samaki upande mmoja niweke nyama na kuku kidogo. Niliopanga kuweka ni 5-7 millioni

Jee kwa muenendo wa hiyo biashara inaweza kunilipa maana sina uzoefu nayo kabisa, naombeni ushauri nisije fukia pesa au nikala hasara, namna ya kuendesha hiyo biashara kwa faida, na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.

1620112723953.png

Biashara ya chakula huwa zinalipa, ila kwakuwa ndio unaanza usianze na kiwango kikubwa cha nyama au bidhaa zako. Cha kufanya nipe mil 1 nisafirishie mchele wangu mpaka hapo Dar ukifika tupanue biashara maana mchele hauozi hata ukikaa mwezi.
Uo mchele wako ni wa wapi na unauzaje?
 
Ndugu wana Jamiiforums nimekuja kwa mara nyingine kuomba ushauri kuhusiana na biashara ya bucha. Huu mwaka ni mpango wangu wa kuongeza biashara nyingine ili kukabiliana na ukali wa maisha.

Ukiachilia mbali biashara ya nafaka ambayo hadi muda huu nakomaa nayo wazo la kwanza nililokuwa nalo ni kufungua biashara ya bucha, upande mmoja ni dili na samaki upande mmoja niweke nyama na kuku kidogo.
Mtaji niliopanga kuweka ni 5-7 millioni

Jee kwa muenendo wa hiyo biashara inaweza kunilipa maana sina uzoefu nayo kabisa, naombeni ushauri nisije fukia pesa au nikala hasara, namna ya kuendesha hiyo biashara kwa faida, na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.
Mimi nipo mwanza. Najitolea kukusafirishia samaki kutoka huko.

Tukubaliane namna ya kunilipa
 
Biashara ya chakula huwa zinalipa, ila kwakuwa ndio unaanza usianze na kiwango kikubwa cha nyama au bidhaa zako. Cha kufanya nipe mil 1 nisafirishie mchele wangu mpaka hapo Dar ukifika tupanue biashara maana mchele hauozi hata ukikaa mwezi.
Aiseeee
 
Kwa sasa bei ya sangara na Sato iko juu Sana Kwa Dar,watu wa Bucha za samaki hawapati faida kubwa.sangara 1kg---9000.
Kipindi cha nyuma kidogo faida ilikuwa nusu Kwa nusu.
Bei ya jumla ya sangara ni 8000-8500
 
😀😀.mnapigwa...! Bado ni ile ile tu mbona
 
Back
Top Bottom