Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,684
- 36,045
Habari!
Hapa naomba tuelewane kuwa sizungumzii pesa bali nazungumzia ndoto za vijana katika kuliinua taifa na familia zao.
Pamoja na kazi ya bodaboda kuwapatia kipato vijana na baadhi ya wazee ambao wanaifanya hiyo biashara lakini imechochea uchumi wa China na India kwa kiasi kikubwa.
Hapa kwa lugha rahisi niseme bodaboda Afrika wanatimiza ndoto za vijana wa India na Uchina kwa kuwafanya mabilionea kila siku.
Ukikaa bandarini na kuona maelfu ya pikipiki zinazoingia kwa siku utajua kuwa huko China na India wamejipanga kukusanya mabilioni.
Twende kwenye point.
Biashara ya bodaboda ina kilevi ndani yake, kila anayeingia anaingia kwasababu za kukwama akijisemea moyoni kuwa nafanya mwaka mmoja tu, au nafanya ili nitimize jambo hili tu kisha niache nirudi kwenye ndoto zangu.
Lakini ni kama 0.001% ndio wanaweza kurudi kwenye ndoto zao, wengi humezwa jumla. Wakikatika miguu huwapa mzigo mama zao maskini walioko kijijini.
Ndoto za kuwa madaktari. Ndoto za kuwa walimu. Ndoto za kubuni viwanda vidogo. Ndoto za kumiliki Education center na baadaye shule.
Nakadhalika, nakadhalika, zimemezwa na vijiwe vya bodaboda. Wanasiasa wanalitumia kundi hili kujiimarisha kisiasa.
Hata Wamachinga wengi pia wanatimiza ndoto za vijana wa Kichina kwa kuuza bidhaa za China.