Biashara ya boda boda

Elie zer

Member
Sep 20, 2021
74
67
Nimejikusanyia ka pesa ka boom kwa miaka miwili sasa, nimepata 1, 400, 000. Nafikiri kununua boda halafu nimwachie mtu aendeshe ili jioni aniletee hesabu!

Hivi bodaboda itanilipa kweli? Na je, nikifanikisha itanibdi nipokee kiasi kipi kwa siku? Mwanachuo UDSM.

Nawasilisha!;
 
Kwa mwanafuzni hiyo biashara pasua kichwa sana labda upate mwaminifu sana tena awe anapaki kijiwe cha chuoni ambako unaweza kumuona mara kwa mara ukiwaaachia hao jamaa wanabeba nayo mkaa, cement, nondo, hadi wanabebea mirunda ndani ya muda mfupi huna chombo na hela haijarudi, tena ujanja ni kutafuta kijana ambaye unaingia naye mkataba kwamba ikifika kiasi fulani boda inakua yakwake hapo utatoboa
 
Mbona hiyo 1,400,000/= bado haijatosha ya kupata bodaboda kwa sababu kwa sasa Boxer/TVS ni 2,700,000/= +, kama ni hizi za Kichina ni 1,700,000/= +
 
Sasa unanshauri niitumie kwa biashara ipi ili nitoboe!?
 
Hongera kwa kufanya saving ya hiyo hela maliza chuo kwanza huku ukiendelea kujichanga na endelea kuchakata mawazo zaidi ya ujasiriamali.
 
Nimejikusanyia ka pesa ka boom kwa miaka miwili sasa, nimepata 1, 400, 000. Nafikiri kununua boda halafu nimwachie mtu aendeshe ili jioni aniletee hesabu!

Hivi bodaboda itanilipa kweli? Na je, nikifanikisha itanibdi nipokee kiasi kipi kwa siku? Mwanachuo UDSM.

Nawasilisha!;
Boda boda hesabu yinategemea na hali ya chombo ila aishuki 5000-8000 kwa hesabu za siku hapo unamwachia siku moja ya kumwaga oil kwa kila week, ikiwa mkataba unapokea 10,000 kila siku na matengenezo kwake.
Nashauri chkua umpe mkataba
 
ndgu boda boda utalia tu japo si vyema kukatishana tamaa,kwa kiasi hicho ulichonacho utapata bodaboda used ambayo iko kwenye hali nzuri ,ila utapompa mtu wiki ya kwanza na yapili hesabu itakuja vizuri kitachofata hapo ni kilio ,ila ukipata mtu mwaminifu huwenda ukatoboa ,MUHIMU KAMA UNA UTHUBUTU BASI TIA MKONO GIZANI TU "
 
Nimejikusanyia ka pesa ka boom kwa miaka miwili sasa, nimepata 1, 400, 000. Nafikiri kununua boda halafu nimwachie mtu aendeshe ili jioni aniletee hesabu!

Hivi bodaboda itanilipa kweli? Na je, nikifanikisha itanibdi nipokee kiasi kipi kwa siku? Mwanachuo UDSM.

Nawasilisha!;
Hongela mkuu nichek pm
 
Wazo zuri sana ila biashara ya vyombo vya moto inabidi uwe na roho ngumu sana, ni rahisi ukiona kwa mwingine ila ukianza mwenyewe ndo utajua ugumu wake,

Hiyo 1.4M utapata piki piki nzuri tuu used.
 
Nimejikusanyia ka pesa ka boom kwa miaka miwili sasa, nimepata 1, 400, 000. Nafikiri kununua boda halafu nimwachie mtu aendeshe ili jioni aniletee hesabu!

Hivi bodaboda itanilipa kweli? Na je, nikifanikisha itanibdi nipokee kiasi kipi kwa siku? Mwanachuo UDSM.

Nawasilisha!;
Fanya biashara kijna hela hiyo kubwa sana unaweza fanya kitu Cha maaana zaidiii ya hicho
 
Back
Top Bottom