Biashara ya Binadam Tanzania imehalalishwa

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Kama kwa wiki hii mmeafatilia makala za bbc swahili,kuna makala maalum juu ya biashara ya binadam Tanzania hasa wanawake,hususan vibinti,mwandish wa makala hiyo ameanza kuonesha tangu wasichana wanapoletwa dar kutokea mikoani,lakin makala ya Asubui hii ya leo tar 14.9.

Inaonesha jinsi wanawake wasio na huruma wanavyojisifu kwa kujiusisha na biashara hiii pasipo kuguswa na dola,mwanamke ambae amehojiwa amesema huwauza mabinti hadi sh.elfu 50 na humpa yule mwanamke elfu 20,lakini hata anapojieleza unapata picha kuwa biashara hii kwa sasa hakuna ambae inamshtua,kwa sababu kama mhusika ameamua kukubal kuhojiwa na mwandish na anakiri kuwa ataishije hapa mjini ina maana watu kama yeye wapo wengi sana,,,,,

Watanzania, vijana wa kitanzania tupo kwenye changamoto sana,vijana weengi wa kiume wapo kwenye changamoto ya madawa ya kulevya,kukosa elimu na wizi lakin vijana wa kike wao wapo kwenye hatari zaid ya kuambukizwa maradh,matumiz ya madawa na kupata mimba za mapeeema,endelea kufuatilia makala hiyo JION YA LEO

BBC wamefanya kazi yao - Tunawashukuru! Kama walivyofanya wakati wa mauaji ya walemavu wa ngozi!

Tunasubiri Mh Pinda aje Bungeni "kulia" kama vile hawajui ni nini kinachoendelea! st**id!

Mkuu hata mimi nimeisikia hiyo story inasikitisha sana!huyo mama anaongea as if ni kazi halali kabisaaaaa!hivi nchi hii haina utawala wa sheria?au polisi wanakua bussy kuzuia watu wasiandamane?kwenye issue za msingi kama kulinda binadamu na mali zao hawaiwezi?very sad.........

Humu JF najua wengi tunaishi huko mitaani!hebu tumwage issue humu,hilo danguro au hayo madanguro yapo wapi?walau hao polisi wasiojua kazi zao wakisoma humu watafuatilia ili kuokoa hao vijana wanaoumia!

Kariako kuna mtu mmoja maarufu sana anaitwa "Kishonde", hii ndio kazi yake miaka mingi sana, ukitaka dada wa nyumbani unampigia simu siku ya pili anakuletea unamlipa, baada ya wiki mbili tatu msichana anapotea, Kishonde kisha mpeleka kwingine. Anauza binaadam kama hana akili vizuri.

Na hao wazungu kwao si wanafanya hivyo hivyo kutumia Man Power Agencies au escort services, hakuna cha ajabu, ushuzi ni uleule tofauti ni mlio tu.

Hule mama anadai eti bibi yake ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa danguro hilo!!! Je hiyo kitu tangu enzi hizo dola ilikuwa wapi!!? Real nimesikitika sana.

Raisi wetu mwenyewe anahongwa suti..huo si utumwa pia. Sasa tunategemea utawala utasemaje? Yaani hatuna viongozi kabisa.. Wapowapo tu. Pumb.avu zao. Nina machungu kuona wenzangu wanauzwa, tena watanzania ambao unakuta walipiga kura awamu iliyopita.

Mm huku mtaani kwetu kuna dalali wa wafanyakazi wa ndani(housegirls)
nayo hıı imekaaje wakubwa,maana anakuletea kama umeridhıka naye unatoa pesa,na hata kama haujaridhika naye unatoa ya usafiri,
wakubwa nayo hii imekaaje?

Hivi ni akina nani wanaowanunua? Tuache kumlaumu huyu mama, mimi lawama zangu zinaenda kwa wanunuz wa ngono.

Kwanza mimi nilipo sikia kuwa anauzwa elfu 50, nikajua ndo maana huyo mama anaongea kwa ujasiri. Bila shaka wateja wakubwa ni vigogo na wenye navyo. Na mama alisema, anawasiliana na wateja wake na kuwapeleka vibinti vyake. Huu ni mtandao mkubwa. Ndo maana majenga hayaishi.

Kumbe kuna baadhi yetu humu jamvini wahusika wa hiyo biashara mnawafahamu! Je mmeshafanya jitihada gani kulikomesha hili? Au ndio mnasubiri mpaka wauzwe ndugu zenu ndio mchukuwe hatuwa? Inaonekana wazi kabisa hata nyie mnaowafahamu hao wahusika wa hiyo biashara mnashirikiana nao kwa njia moja au nyingine.

Elfu hamsini ni pesa kubwa sana kiasi kwamba sakala wa kawaida hawezi kununua penzi kwa pesa hiyo
Kwanza mimi nilipo sikia kuwa anauzwa elfu 50, nikajua ndo maana huyo mama anaongea kwa ujasiri. Bila shaka wateja wakubwa ni vigogo na wenye navyo. Na mama alisema, anawasiliana na wateja wake na kuwapeleka vibinti vyake. Huu ni mtandao mkubwa. Ndo maana majenga hayaishi.

Wanaume ndio wanunuzi hilo halina shaka,lakini amesema hata wasagaji pia wanakuja kwake,,,,,,,,
Hivi ni akina nani wanaowanunua? Tuache kumlaumu huyu mama, mimi lawama zangu zinaenda kwa wanunuz wa ngono.

Hiyo nayo ni biashara ya binadam wala haina shaka mdau,,,,,
Mm huku mtaani kwetu kuna dalali wa wafanyakazi wa ndani(housegirls)

nayo hıı imekaaje wakubwa,maana anakuletea kama umeridhıka naye unatoa pesa,na hata kama haujaridhika naye unatoa ya usafiri,

wakubwa nayo hii imekaaje?

Labda tatizo ni kwamba hilo ni dangulo lakini ki-uhalisia hata kule cassiono mchezo ndio huuhuu,ila ile ni legalized
Hule mama anadai eti bibi yake ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa danguro hilo!!! Je hiyo kitu tangu enzi hizo dola ilikuwa wapi!!? Real nimesikitika sana.

Wewe unazungumzia vyomba gani vya DOLA?????hebu fafanua,una maanisha hivihivi tulivyovizoeaaa yaaani polisi na mahakama na watu wa usalama,,,thubutuuuu hao hawawezi,kwa sababu wanadhiki na wanapata sana hongo juu ya hii biashara,biashara hii ni kama ile ya GONGO
BBC wamefanya kazi yao - Tunawashukuru! Kama walivyofanya wakati wa mauaji ya walemavu wa ngozi!

Tunasubiri Mh Pinda aje Bungeni "kulia" kama vile hawajui ni nini kinachoendelea! st**id!

Sikuweza kuamini kwa jinsi huyo mama alivyokuwa anaongea kwa kujiamini pasipo woga, yeye anadai biashara zote anafanya kuanzia vibinti vidogo, mashoga na hata wasagaji!!!! Kweli Tanzania imelaaniwa na kamwe majanga hayataisha!!

BBC waliweza kuweka wazi kuhusu mauaji na biashara ya viungo vya albino lakini Serikali haikuchukua hatua yoyote mpaka sasa, hii inaonyesha kuwa katika biashara zote haramu zinazofanyika hapa nchini kuna viongozi wa juu serikalini wanahusika moja kwa moja

Kama kwa wiki hii mmeafatilia makala za bbc swahili,kuna makala maalum juu ya biashara ya binadam tanzania hasa wanawake,hususan vibinti,mwandish wa makala hiyo ameanza kuonesha tangu wasichana wanapoletwa dar kutokea mikoani,lakin makala ya Asubui hii ya leo tar 14.9. Inaonesha jinsi wanawake wasio na huruma wanavyojisifu kwa kujiusisha na biashara hiii pasipo kuguswa na dola,mwanamke ambae amehojiwa amesema huwauza mabinti hadi sh.elfu 50 na humpa yule mwanamke elfu 20,lakini hata anapojieleza unapata picha kuwa biashara hii kwa sasa hakuna ambae inamshtua,kwa sababu kama mhusika ameamua kukubal kuhojiwa na mwandish na anakiri kuwa ataishije hapa mjini ina maana watu kama yeye wapo wengi sana,,,,,watanzania vijana wa kitanzania tupo kwenye changamoto sana,vijana weengi wa kiume wapo kwenye changamoto ya madawa ya kulevya,kukosa elimu na wizi lakin vijana wa kike wao wapo kwenye hatari zaid ya kuambukizwa maradh,matumiz ya madawa na kupata mimba za mapeeema,endelea kufuatilia makala hiyo JION YA LEO

Kutokana na ugumu wa maisha watu wanatafuta kila njia ili wajikwamue.
Kuna madalali wa kabisa wa wasichana wa kufanya kazi majumbani sijui wanalipa kodi?

Kwa kodi sahau sema wanalipa rushwa(ambayo si kodi rasmi)
Kutokana na ugumu wa maisha watu wanatafuta kila njia ili wajikwamue.

Kuna madalali wa kabisa wa wasichana wa kufanya kazi majumbani sijui wanalipa kodi?

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom