Biashara ya Uokaji (Bakery): Mbinu, Ushauri na Changamoto Zake

Habari zenu wana JF,
Ningependa kufahamu kwamba ni vitu gani vinahitajika ili kufungua kiwanda kidogo cha mikate (BAKERY), Hii namaanisha vifaa vinavyotakiwa ili uzalishaji uanze.
 
Salaams JF,

Nilipata wazo la kuanzisha bakery maeneo ya sinza. Products ni ; Mikate, Maandazi na cakes aina mbalimbali. Sikuomba au kutafuta ushauri kwa mtu yeyote. Pia sijafanya research ya uhakika kuhusu mahitaji halisi ya hizo bidhaa ninazotaka kuingiza sokoni. Pia sijafanya utafiti kuhusu ushindani wa hii biashara. Nimeamua kuchukua RISK 100% katika kuwekeza huko kwenye bakery. Kwahiyo bado sijaelewa / sijajua kama nipo njia sahihi au nimekosea. Naomba ushauri na uelewa wenu kwenu hii biashara.

Hadi sasa nimefanikiwa kupata vitu vifuatavyo;
- Machines- 3 Ovens ( moja kubwa inaingiza paltes 6 na nyingine mbili ni ndogo zinaingiza plates 2 kila moja); 1 Mixer aina ya B30; Shelf; 30 Oven Plates,
-Nimepanga Jengo na kulifanyia ukarabati kulingana na mahitaji ya kazi.
-Nimesajili jina la biashara
-Nimeshapata na TIN
-Nimeshapata leseni

Vitu vinavyohitajika kwa sasa ni;
-Connecting service line ( electricity) kwenye jengo ambalo nimeshafanya wiring
-TFDA authorization
-Source of more finance
-Hard working, knowledgeable and skilled person ( Baker) ambaye ataweza kutengeneza bidhaa mbalimbali
-Bread slicer
-Manager and cashier
-Marketing and sales person
-Distributor

Je mnaonaje wakuu? Je nipo sahihi? Nawakilisha

===========
SIMILAR CASES:
===========
Jan 19, 2012:
Uko sahihi balaaa wala huna haja ya research nakushauri tafuta baker mzuri walio cheap na wazuri wanapatikana burundi ,nenda si ghari hadi kigoma kwa basi ni 60 elfu hadi bujumbura na hadi bujumbura ni 20 elfu kwenda kurudi na kulala +kula haizidi 300,000 ila utawakula mikate mitamu africa nzima pale na wanavijua viungo vyao vya siri mkate unanukia ka pilau,na unaisikia harufu ya ngano harisi radha usiseme
 
Natuma hamjambo Wana jf. Naombien kupatiwa ufafanuz juu ya vifaa (equipment) zinazoitajika unapotaka kufungua bakery?
 
Oven machine
Mixer Machine
Slicer machine
Improver- kwa ajili ya kuumulia
Makopo ya kuweka mchanganyiko wa keki au mkate
Plates na tools nyingine kutokana na nature au bidhaa utakayotengeneza
 
UKITAKA OVEN YA MAISHA YA KITANZANIA NITAFUTE NAUZA MASHINE YA KUOKA MIKATE NA KEKI INAYOTUMIA MKAA KIDOGO KWA TSH 500,000/= TRANSPORT NI JUU YAKO
 
c74a63d2103a2054281c7a5bc8c88d62.jpg


Nitafute kwenye namba 0712823601 nauza iyo oven ya kuoka mikate,cakes n.k
 
Mkuu mpaka hapo ulipofika huna haja ya kufikiri kama umekosea au la. Go go go forward the world needs people who dare to risk.
 
Uko sahihi balaaa wala huna haja ya research nakushauri tafuta baker mzuri walio cheap na wazuri wanapatikana burundi ,nenda si ghari hadi kigoma kwa basi ni 60 elfu hadi bujumbura na hadi bujumbura ni 20 elfu kwenda kurudi na kulala +kula haizidi 300,000 ila utawakula mikate mitamu africa nzima pale na wanavijua viungo vyao vya siri mkate unanukia ka pilau,na unaisikia harufu ya ngano harisi radha usiseme
Jumuisha gharama ya work permit na usumbufu wa kuipata.
 
Wadau habari za leo? Natamani kufungua biashara ya mikate yaani Bakery hivi karibuni ila sina uelewa kuhusu biashara hii. Hivyo naomba wenye uzoefu mnielimishe gharama halisi zinazohitajika katika biashara hii ikiwa ni pamoja na vifaa/mashine na bei zake, sehemu zinakopatikana/zinakouzwa kwa hapa Tanzania, gharama nyingine za uendeshaji na jinsi ya kukokotoa faida/hasara katika biashara hii. Asanteni
 
Habari zenu wadau,naomba kujuvya kuhusu biashara ya bekary,mtaji wake,changamaoto.zake,faida yake ikoje.mwenye uzoefu wa biashara hii naomba msaada.
 
Hello Ndugu zanguni,

Nimekuwa na ndoto ya kuanzisha au kufanya project yangu ya kufungua a small and good bakery, kwa ajili ya only cake designing and decoration.

Naomba mnipatie idea mbali mbali za vifaa ambavyo ni muhimu, kwa ajili ya kuanzisha huu mradi wangu.
Na naweza pata wapi hivyo vifaa kwa hapa Tanzania au labda nchi jirani ya Kenya.

Kwa yeyote ana experience pia ya hii kind of business ningeshukuru sana kama pia angenipa mawazo na changamoto zilizopo.

Thankx and waiting for your response. Be blessed all and have a nyc Sunday.
 
Hii biashara kama ndo unaanza kabisa ni kazi kidogo kwa upande wa vifaa ila ukisha kua navyo ni mwendo wa kuingiza pesa tuu. Vifaa utakavyohitaj vya muhim
*Mixer
*Oven
*Masufuria
*Mabomba au karatas za kudecorate
*Nozzles

Hapo hujawek mazaga yanayotumik kutengenezea keki kama ngano, sukar n.k

Changamoto zilizokuepo kwenye hii biashara n wateja kukuzoea au kukuamini! Watu wenye jina ndio wanapata fursa nyingi tofauti na wasio na jina, so kama unaanza hakikisha unatengeneza vitu high quality, pesa utakuj piga mbele huko! Niko Dar, ukitak tukutane nkuwek waz zaid ni pm!
 
Back
Top Bottom