Raha ya biashara ni kufanya biashara halali,lakini biashara kama ya huyu bwana haina tofauti na ya wamachinga ya kiwizi wizi, kila siku utakuwa unatizama nyuma, nani ananifuata TRA, CITY, BWANA AFYA au Polisi. Watu wanasema kama hutaki kuota usilale - wewe kama ni mtu wa kutopenda matatizo ushauri wa huyo jamaa hautokufaa. Kikubwa mafanikio ya biashara yako ni kupata vifaa vizuri, mpishi mzuri,Packing inayovutia, usafi wa sehemu yako ya kufanya kazi na kuweka uangalizi mzuri maana wengi wenye bakery wanalia na wizi unaofanywa na wafanyanyakazi wa vitu kama Sukari, Unga, Mafuta na mara nyingine hata wanacheza na uzito wa mkate itoke mingi wauze inayozidi pesa wachukue wao.kuna jamaa anaitwa Thomas mikate,yeye yupo DAR, anuaza mikate mingi sana kwa kutwa,ni rafiki yangu kwa uteja kwake.
-hana brand wala Duka la mikate yeye anauzia ktk gari lake,ni suzuki mini van,kadogo hivi rangi ya blue na pia anayo nyeusi,huwa anapaki station opposite TRA offices ,jioni na pia huwa anakuwa maeneo ya posta karibu na CRDB holland house or ifm area.
mwaka 2009 aliniambia kuwa anapata daily profit ya 140,000. na kuwa mikate yake huwa haibaki.jaribu kumtafuta atakushauri ni mtu muelewa,ila hapendi watu wa TRA(kodi etc)walishawahi kumsumbua ndio maana hana BRAND ya mikate yake,
inasadikika kuwa bakressa wa Azam huwa ananunua mikate yake kwa matumizi yake na wajukuu zake.