Biashara United wamekwama tena kifedha. Mkuu wa mkoa yuko wapi?

Mpaka jioni bado walikuwa hawajaondoka, wamefanikiwa kupata ndege ya serikali lakini hawajapata vibali vya anga kwa ndege. Mkuu wa mkoa kajikausha kimya Kama sio yeye aliyekuwa anatoa ahadi.
 
Biashara United ya Tanzania hadi sasa haijasafiri kwenda Libya kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli, kutokana na ukata wa fedha.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa kesho saa 2:00 usiku. Katika mchezo wa kwanza Biashara ilishinda 2-0.
20211022_212558.jpg



tangu jumatatu viongozi wapo kimya tu..
 
Hapa hakuna tff Ni takataka tu Kama tungekuwa na shirikisho makini lingeshughulikia kila kitu hata kwa kuwakopea pesa waje walipe badae kwenye viingilio.

Huu upuuzi pia tff inatakiwa kulaumiwa
Acha kupenda lawama kama mtoto wa kambo mtu hakopeshwi hela bila yeye kutaka kukopa hao biashara walifanya juhudi gani ya kukopa hiyo hela kama taasisi
Tff haiwajibiki kulipia vilabu nauli zao wao kama timu na taasisi walitakiwa kujipanga kwani hawakushtushwa tu kwenda kimataifa na kama mwendo wao ndio huu wa kushindwa hata nauli bora wakati mwengne tusiwaone huko kimataifa wanatia aibu sana
 
BIASHARA UNITED NI TIMU KUBWA YENYE WACHEZAJI WAZURI,NINGELIKUWA NA UWEZO NINGELIINUNUA ISAIDIWE HARAKA HATA KWA HARAMBEE,AU CHADEMA IINUNUE TWENDE NAYO KWA HARAMBEE**kuliko kukichangia chama mfu
Huitakii mema hiyo timu. Ikinunuliwa na Chadema kila ichezapo referees no 1,2 na 3 watakuwa CCM.
 
Efm walimuuliza kuhusu kuisaidia biashara akadai hawezi kutoa pesa za mshahara wake tayari keshajiumbua ile ahadi haikuwa yake Bali gsm ila ushabiki wake maandazi kwa biashara unaweza kuiharibu timu badala ya kuisaidia
Kwa hiyo nje ya mshahara wake hawezi kupata pesa isipokuwa apewe na GSM? Simba akili zenu ni kama mnakulaga udongo.
 
Hapa hakuna tff Ni takataka tu Kama tungekuwa na shirikisho makini lingeshughulikia kila kitu hata kwa kuwakopea pesa waje walipe badae kwenye viingilio.

Huu upuuzi pia tff inatakiwa kulaumiwa
Biashara walijua wanatakiwa kusafiri, walitakiwa waanze mchakato mapema wao kama wao
 
Back
Top Bottom