Biashara(soko) ya Mafuta ya Kulainisha Mitambo(Lubricants)Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara(soko) ya Mafuta ya Kulainisha Mitambo(Lubricants)Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KyelaBoy, Oct 25, 2010.

 1. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu tafadhali naomba msaada wenu kuhusu soko/biashara ya mafuta ya kulainisha mitambo(lubricants),pia oil, hapa Tanzania,kama kuna muelewa wa hii industry kwa hapa Tanzania naomba tuwasiliane kwa email: rayerasto@gmail.com.
  Ninachotaka hasa kujua ni
  1.watengenezaji waliopo hapa Tanzania,na je hayo mafuta yote yanatengenezwa hapa hapa au yanaagizwa nje ya nchi,na waaigizaji ni nani
  2.Ukubwa wa soko kwa hapa Tanzania,bei zake na chapa(brands) zilizopo sokoni
  3.Sheria za kuanzisha hiyo biashara kwa hapa Tanzania kama ni kwa kuanzisha kiwanda au kuagiza
  4.Mambo ya ushuru kwa upande wa EWURA na TRA.
  Nimejaribu kuangalia yote hayo kwenye mtandao wa Ewura lakini huo mtandao hauna data/informations kama hizo
  5.Pia kama kuna takwimu zozote juu ya hiyo industry kuhusu market share,
  Asanteni
   
 2. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kaka huwezi kupata taariffa kama hizo kwa mtandao wa EWURA , labda ufanye special request, hawawezi ku- disclose kwenye uwanja wa kila mtu kusoma- utaratibu hauendi hivyo.
  swali la kwanza
  watengenezaji tanzania ni oryx, Total, Bp Caltex Fuchis na MGS. hawa ninaokutajia wanatengeneza 80% ya products locally na 20% ( special products) wana ingiza kutoka nje. recent information inasema BP wana import 100% sasa. kuna viwanda viwili tu tanzania , kimoja cha oryx na kingine cha fuchis- so wote wanaotengeneza tanzania wanapanga foleni ya huduma kwa hawa wenye viwanda
  wauzaji wa tanzania ambao hawatengenezi tanzania ni wengi hao wakiwemo GAPCO, na wengne wengi~~~ ukiwasiliana na hawa wanaotengeneza locally watakuopa list ya wanaoingiza na nafasi zao sokoni
  swali la pili
  soko kubwa la vilainishi tanzania ni kwenye automotive( mainly retail)- ambayo ni kama asilimia sitini mpaka sabini, inayobali ( 30% ni industrial products ambazo haswa ni kwenye ujenzi (haswa barabara),cement industry and sugar volumes bado ni wewe upate kwa kuwasiliana na EWURA, au TRA. main brands ni CALTEX, BP, Oryx and TOTAL for retail, kwa industrial SHELL inaongezaka. soko lime vamiwa sana na bidhaa feki- hiyo ni changamoto ya walio sokoni
  swali la tatu
  sheria za kuanzisha biashara au kiwanda , taratibu za kawaida za biashara utakuwa unazijua - hazitofautiani toka biashara mpaka biashara, bali kwa hii ya mafuta, EWURA watakupa utaratibu unaohusiana na mafuta na vilainishi- iwe kuagiza, kuzalisha au kufanya ugavi au uuzaji
  swali la nne

  utalipa importy duty for imported products based on CIF, on top utalipa EWURA levy na VAT- rates zipo wazi kwa TRA na EWURA.


  swali la tano

  sina uhakika na market share kwa sasa- bado ukiwasiliana na hawa ma -giant ( oryx, Bp, Total etc wanaweza kukupa)


  nimekupa maelezo ya jumla. unatakiwa kutumia consultant atakupa mambo ya uhakika. maelezo ninayokupa unaweza kuyatumia tu kupima uhakika wa report ya consultant wako. kiujumla sikushauri upoteze muda kwenye website za taasisi za tanzania kupata habari muhimu- huwa hawa badilishi taarifa, waweza kuta taarifa ina umri wa miaka mitano.kama unaona hunauwezo wa kutafuta consultant, ni- PM niku- link na watu wa hizo kampuni na EWURA - mtaelewana wenyewe.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Maelezo ni sahihi kabisa.

  Ila BP imeshakufa/funga vilago Tanzania. Ukiweza kumpata mnene mmoja ndani ya Oryx (zamani Agip) anaweza kukupa maelezo mazuri sana,makampuni yote isipokuwa FUCHIS hawana mitambo ya kupikia oil,wanatumia mitambo ya Oryx pale Kurasini. Kwa hiyo ukitaka habari nzuri kuhusu soko mtafute mtu wa Oryx atakupa detail vizuri.
   
 4. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu nakushukuru sana umenipa pa kuanzia
   
 5. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu ni meku PM,naomba unijibu
   
Loading...