Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Posta unapajua? Pana nyumba za kuishi za kupangisha pale?
Sasa kupata Kiwanja tu pale huweziii...Hata kikiwepo ni mamillion...!! Ukesema mil 20 useme unajenga kimara hukoo labda na hapo laki 2.5 ni nyumba yenye Tiles...madirisha ya aluminium..gypsum safii...Masterbed room Bado vingine kibaooo so sio simple mzeee
 
Ndachuwa,
Sio kweli kwamba kila wakati nyumba ina "appreciate" katika namna hii, kwamba thamani ya nyumba ina double au tuseme kuongezeka thamani kwa kiasi kikubwa!

Value ya nyumba au jengo inategemea mambo mengine mno na ni pamoja nyumba yenyewe, huduma za kijamii na miundo mbinu na kadhalika. Ukijenga nyumba la milioni 150 kwenye kiwanja chako Mlandizi haliwezi ku-appreciate sawa na nyumba ya namna hiyo hiyo iliyopo Sinza, hilo ni moja!

Pili kuna suala la soko, soko pia linashinikiza thamani ya vitu kama nyumba, ardhi. Wakati wa Kikwete kulikuwa na pesa nyingi mno mtaani na ilikuwa kawaida sana kuona ardhi, nyumba zikiuzwa kwa bei ya kufa mtu na pengine ardhi na nyumba hizo hazikuwa na thamani hizo...ndio kusema bei zilikuwa "inflated", sasa kwa sasa hali ni tofauti sana!

Ushauri wangu, tujielimishe zaidi kuhusu masuala ya "real estate"...nyumba, ardhi na itatusaidia. Kwa sasa sehemu nyingine duniani mambo yanabadilika, hata mtazamo wa watu kuhusu umiliki wa nyumba umebadilika.

Watu wengi wanachagua kuwa na nyumba ndogo lakini "functional" hivyo pengine kabla ya kujiingiza kwenye mkopo wa nyumba wa milioni 150 au 300 ni nzuri kufikiria je, unahitaji nyumba kubwa namna hiyo? Haiwezekani kujenga nyumba ya kadiri kwanza halafu kujenga hiyo "dream home" taratibu?

Mikopo ni bora tu kama inatusaidia kuingiza pesa zaidi au kuongeza ubora wa maisha yetu ila kama tunakopa halafu tunaumwa kichwa na kuwa stressed kila wakati nafikiri ni wakati wa kufikiria kidogo!
 
Mpogoro,
Pamoja na hali mbaya ya kifedha bei ya nyumba kwenye miji ya zamani kama Magomeni, Kimara, Sinza ikoje? Inashuka?
 
NJOLO,
Genius

Chief uelewa wako ni mkubwa sana kuna watu wanaweza wakashindwa hata ku comprehend. Uelewa wako ni very technical in a business sense. It is indeed next level
 
Pamoja na hali mbaya ya kifedha bei ya nyumba kwenye miji ya zamani kama Magomeni, Kimara, Sinza ikoje? Inashuka?

Bei zake zimeshuka, kama mtu alimataa bilioni moja wakati wa Kikwete yaani usawa huu wa Magu nafikiri hawezi kuiona kabisa!
 
Bei zake zimeshuka, kama mtu alimataa bilioni moja wakati wa Kikwete yaani usawa huu wa Magu nafikiri hawezi kuiona kabisa!
Arusha ppf kuna jamaa alikataa mil 750 kipindi cha JK sa hivi kila akipata mteja/dalali bei anayoletewa ina-range kwny mil 350-400 hapo full stop.
 
Mpogoro,
Mkuu nimependa mawazo yako ambayo yako wise and balanced. Unaonekana una uzoefu mkubwa sana kwenye masuala ya finance and cash flow management
 
Naona mahesabu yenu wengi hayako sawa. Mnaweka rejesho katika hela ya mkopo na sio hela ambayo wewe mwenyewe umewekeza. Unaponunua au kujenga nyumba kuna 'down payment' ambayo ni asilimia flani ya bei ya nyumba unatoa mwanzo.

Kama hela yote ya kujenga au kununua unakopeshwa basi kiwango hiki ni sifuri. Hivyo sasa kama umejenga na rejesho la kila mwezi ukijumuisha rejesho kwa benki, gharama za utunzaji wa nyumba na matumizi yote yanayohusiana na nyumba ukapata 500,000 halafu kodi ikawa 600,000 basi hapo faida yako ni 100,000 kila mwezi ambayo ni 1,200,000 kwa mwaka. Kama hukutoa hela yoyote katika ujenzi au ununuzi hii ni 1.2 million ya faida kamili kutoka mtaji wa sifuri.

Hii ni pesa unaipata kila mwaka kwa muda wote unamiliki nyumba. Kama ulitoa hela yako mwenyewe katika ujenzi au ununuzi mfano milioni 12 basi unachukua 1.2 m gawa kwa 12 m unapata 10% rejesho kwa hela yako kila mwaka. Mtu yeyote ataefanya maamuzi mazuri katika kuchagua sehemu inayopangishika basi atafanikisha hili.

Ila uzuri wa real estate unakuja katika uwezo wa kufanyisha kazi mtaji (leverage). Kila ukilipa rejesho unajenga umiliki katika nyumba. Hivyo kama una umiliki wa asilimia 20 katika nyumba (yani umelipa rejesho kufikia umiliki huo) basi unaweza kutumia ule umiliki (equity) kupata mkopo mwingine.

Kumbuka kwa kuwa kodi ndio inalipa rejesho basi hii inakuwa hela ya bure kwa kuwa wewe binafsi pesa yako mfukoni haitoki. Mkopo huu unaweza kutumia katika ujenzi mwingine au biashara nyingine. Ni wachache wanajua kuhusu hili.

Jambo lingine ni kadri muda unavyoenda thamani ya nyumba inabadilika. Na muda wowote unaweza kwenda bank na kuwataka wafanye tathmini ya thamani.

Kama thamani imepanda basi unaweza kukopa tena kwa kuweka dhamana ya nyumba hiyohiyo ambayo inalipiwa na wapangaji. Mfano umejenga kwa milioni 100 na ndio thamani benki imekubaliana mwanzoni. Baada ya miaka 3 umeshalipa milioni 30 katika 100 hivyo kiharakaharaka una umiliki (equity) ya asilimia 30.

Ila kama unadhani nyumba imeongezeka unaweza kwenda benki na kuwataka wafanyie tathmini nyumba yako upya. Kama wakija na tathmini ya milioni 120 basi ina maana unaweza kukopesheka milioni 20 zaidi, hela ambayo unaweza kutumia kulipia mkopo au kufanyia mengine kama kujenga nyumba mpya. Hili ni advanced kidogo na inahitaji ujue hayo mawili ya kwanza kabla ya kuja huku.

Na hivi ndivyo unaweza kuwa tajiri kwa real estate. Kodi peke yake haitoshi ila kucheza na thamani ya nyumba yako ni muhimu pia.
 
Jirani yetu sinza kijiweni alikua anapangisha nyumba yake kwa Tsh.600,000 sa hivi mpangaji analipa 400,000 tena huyu nae analipiwa na office la sivyo angekua ashasepa.
Hiyo ofisi soon itashindwa kumlipia. Landlord ajiandae kisaikolojia.
**Wadada nao wanadanga/kupiga mizinga kama wametumwa vile.
 
Mambo mengine yanafundishwa darasani siyo JF. Hapa JF hautaweza kuelewa maana ya asset na liability kama ilivyo kwenye vitabu. Nenda darasani! Wenzio wanakueleza ilivyo kwenye vitabu siyo hiyo unayoifikiria ya mtaani.
Argument yangu bado ipo pale pale. Kama inatoa tu pesa haiingizi, si bora uigawe tu?
 
Mimi siyo Mhindi wala sikusoma elimu ya biashara lakini akili yangu ya kuzaliwa iko kama hiyo ya Mhindi.

Siwezi kuweka mil 150 katika fixed asset na kubaki na mil 10 kwenye mzunguko ama benki. Tatizo la wengi wanataka kuonekana kwa wanadamu - gari la bei kubwa, nyumba kubwa, nk. Sisi na Wahindi hatutaki kujionyesha kwa wanadamu.

Pesa inakaa benki. Ukiwa na pesa ya kutosha utanunua nyumba leo hii, utapeleka mtoto shule, utanunua gari nk kama utataka. Cash is king... Lakini ukiwa na nyumba huku hauna pesa, inabidi uitangaze kwanza ndio upate pesa - na kama itapata mnunuaji.
Cash Money Forever,
 
Ngwanakilala,
Nikushukuru mtoa Mada, Uchambuzi mzuri,
Kutokuwa na taarifa na uelewa wa nini ufanye na wapi ufanye imeathiri wengi,
Nina imani hii tafakuri uliyoianzisha itatuletea wabobezi wa mambo ya Business Planning, Finance Management na Risk management ili angalau watu wajue akiwa na mtaji mdogo kipi cha kufanya, akiwa na mtaji wa kati kipi afanye akiwa na surplus ya fedha kipi afanye..
Ndaga
 
Ngwanakilala, Mwaka juzi nilijenga nyumba ya kisasa ya room 4. kwa ajili ya kupangisha, Lakini nilipo maliza kuweka paa, pamoja na madirisha ya chuma na milango miwili ya mbele na nyuma.wazo la kufuga kuku wa nyama likawa limeingia kichwani..Nikaacha kumalizia nyumba Naendelea na ufugaji..Kupangisha nyumba biashara kichaa.Mimi hapana
 
Back
Top Bottom