Biashara ndogo za chakula zinazoweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo kabisa

Livingson1

Member
Jul 13, 2021
30
26
1 Chipsi. Mtaji ni mdogo hapa unaeza anza na ndoo moja ya viazi, mafuta lita 2 vyombo vya kupikia na vyombo vya kuuzia bila kisahau genge ama banda la kupikia na kuuzia.

2 Sambusa. Mapishi ya sambusa pia ni biashara nyingine isiyohitaji mtaji mkubwa.

3 Maandazi. Biashara ya kuuza mandazi haina tofauti na biashara ya sambusa. Mtaji wake ni mdogo pia.

4 Popcorn 🍿 mfano mzuri ni wale vijana pale makumbusho stand.

5Chapati. Hii ni biashara isiyotofautiana na biashara ya maandazi, ama unaeza changanya mandazi na chapati kuwa biashara moja vile mtaji unaendelea kukua.

6. Juice ya matunda. Hii ni biashara inayokuwa na soko kubwa now hapa mjini, watu wengi huoendelea juice za matunda halisi siku hizi. Na mtaji wake ni mdogo pia hata kwa mtu mwenye kioato kidogo ataweza kuifanya hii.

7. Juice ya miwa, haitofautiani sana na biashara ya juice ya matunda. Hapa mtengenezaji hutumia miwa.

8. Kuuza vipande vya miwa vilivyochongwa na kukatwakatwa vidogo vidogo.

9.ice cream 🍨.
10 cake 🍰
11. Viungo vya chakula.
12. Korosho
13. Karanga
.
.
N.k
 
1 Chipsi. Mtaji ni mdogo hapa unaeza anza na ndoo moja ya viazi, mafuta lita 2 vyombo vya kupikia na vyombo vya kuuzia bila kisahau genge ama banda la kupikia na kuuzia.

2 Sambusa. Mapishi ya sambusa pia ni biashara nyingine isiyohitaji mtaji mkubwa.

3 Maandazi. Biashara ya kuuza mandazi haina tofauti na biashara ya sambusa. Mtaji wake ni mdogo pia.
Mtaji "mdogo kabisa" unakadiria ni kama shilingi ngapi za kitanzania?
 
Chukua hii kwangu kwa walioko Njombe maeneo YA Nzengerendete NA kambarage wananipata.
Issue KUUZA MISHKAKI YA NYAMA YA NG'OMBE
Mtaji wa kawaida lilianza.
Jiko la kuchomea 30,000 hili ukinunua linadumu miaka hata tano
☆☆☆☆☆☆☆
Nyama kg 2 tsh 14000
Stick za nyama 1000
Tangawizi za 200
Kitunguu maji cha 200
Chumvi 300
Limau au ndimu 200
ANZA KAZI
mishikaki 500 kila mmoja.
Vipande vidogo vinne
Kg 2 faida elf kumi uhakika ukishazoea utachukua kilo nyingi kulingana NA biashara inavyokuivia
20210726_152909.jpg
 
Inategemea la umeme linaanzia laki tatu na nusu la gesi kuanzia laki 3 na tisini
Katika ujasiriamali/biashara kama utatumia chochote kinachotumia umeme Tambua ipo Siku utawalaani TANESCO.

Mfanyabiashara kuliko atumie jiko la umeme ni mara 100 atumie kuni au mkaa maana majiko ya umeme ni stress plus kupunguza faida yako.

Popcorn zina Pesa sana sana sana ila ONLY tu kama mtengeneza popcorn atatumia Jiko la GAS not otherwise.

Wanaotumia majiko ya umeme kuandaa popcorn ni wale wenye wanaweza uza box ya popcorn 5000k ujazo ambao huku mtaani unaupata kwa buku tu.

ila kama unataka uza popcorn bei ya kitanzania Komaa nunua Mashine ya gas na si ya umeme.
 
1 Chipsi. Mtaji ni mdogo hapa unaeza anza na ndoo moja ya viazi, mafuta lita 2 vyombo vya kupikia na vyombo vya kuuzia bila kisahau genge ama banda la kupikia na kuuzia.

2 Sambusa. Mapishi ya sambusa pia ni biashara nyingine isiyohitaji mtaji mkubwa.
Sawa
 
Usimkatushe tamaa bwana
"Popcorn Ni Zina hela kweli" ukipata location nzuri tu haijarishi Ni juko la umeme au gas.
Shahidi Mimi mwenyewe nipo stand ya bajaji pamechanganya napata hela nzuri tu Nina miezi sasa mashine imerudisha hela Mara nne yake+ na Ni ya umeme.
Nakubaliana na wewe TANESCO wakizingua utawalaani.
 
Wow hongera kwa biashara mkuu, vipi usimamizi ni wewe mwenyewe ama kuna mtu anakuletea hesabu?
 
Back
Top Bottom