Biashara na juba,sudan

Zamazamani

JF-Expert Member
Jun 13, 2008
1,859
763
Wadau nafikiria kufungua milango ya kibiashara ya kupeleka vyakula huko Juba ,Sudan...Je hawa jamaa wanaeleweka au ni matapeli kama comoro na kongo???(nilishawahi tapeliwa na hawa jamaa)..hasa kama sintotumia LC from the bank???.je kuna mtu mwenye uzoefu na hawa jamaa???? naomba mawazo!!
 
Kaka ngoja tusubiri wadau kama watakuja, hata mimi ningependa kufanya biashara huko. Sababu yangu ni kwamba ninahisi kwa kuwa ni nchi changa basi fursa zitakuwa ni nyingi na za kueleweka.
 
Ikiwezekana tumia LC kila unapofanya biashara na mtu kutoka nchi yeyote ile. Hakuna nchi ambayo hakuna matapeli.
 
South Sudan (RSS) kuna fursa nyingi sana, wanaija wameanza kwenda RSS kwa wingi. Kwa kweli kwa biashara ya chakula unaweza fanya vizuri sana. Changamoto kubwa South Sudan ni Insecurity na Miundombinu hasa barabara. Ni vema transactions zikafanywa thru bank. ;.,k f Nilikuwepo huko Kuanzia Nov. mwaka mpaka January 2013. Juba, population ni kubwa sana na ndugu zetu wa Uganda ni kama nyumbani kwao wanafanya biashara zote kuanzia bodaboda, mama ntilie mpaka biashara kubwa.

Hawa jamaa (wenyeji) wanaamika sana, tatizo ni kuwa wamechanganyikana sana na majirani zetu hivyo polepole wanaanza ku-copy. Ninakumbuka miaka 2007-2011, Juba ilikuwa shwari sana na hata sehemu nyingine za South Sudan, watu walikuwa wanatembea na dollar kwenye plastic bags.

Wakenya na Waethiopia wanafuatia. Kama mtu ambaye uko tayari ku-take a risk South Sudan is the place to do business.
 
Back
Top Bottom