Biashara katika uchumi

Othman Mohamed

New Member
Sep 29, 2021
1
1
BIASHARA KATIKA UCHUMI
Katika nchi yetu ya Tanzania kwa mwaka pekee idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu inazidi 1,000, Apo ni chuo kimoja kwahiyo tukiangalia idadi ya vyuo vyetu nchini tukijumlisha na idadi hii ya wahitimu tunapata idadi kubwa sana ya wanafunzi wanaomaliza kwa mwaka katika vyuo mbalimbali na hii ni ngazi ya shahada peke yake yenye michepuo yote.

Wahitimu hawa wapo kwenye makundi mawili. Kundi (A) ni wahitimu ambao wakimaliza wanategemea ajira na kundi (B) ni wahitimu wakimaliza wanataka kujiajiri. Wahitimu wa kundi (B) ambao wanataka kujiajiri huwa wanaupeo(vision) ambao wengi wao huwa wanatengeneza mpango wa biashara(business plan) tofauti tofauti kulingana na elimu walioipata vyuoni. Mipango hii ya biashara nyingi zinakua ni ya kuanzisha (start up business) lakini ma bank nchini huwa wanataka taarifa za kifedha za miaka ya nyuma ili waeze kukutathmini na kuwe na dhamana ( asilimia kubwa ya dhamana yenyewe inakua ni nyumba) ndo waweze kukupa mkopo. Vitu hivi vinakua vikwazo vikubwa kwa kundi hili (B) ambalo linataka kujiajiri.

Serikali yetu ingeangalia namna ya kuwekeza kwenye kundi hili (B) na kutafuta namna ya kuondoa vikwazo kwasababu kundi hili likiwezeshwa na kufanya biashara kupitia mipango yao itawezesha serikali kukua kiuchumi kwasababu kundi (B) litakua na uwezo wa kuajiri kundi (A) ambapo ajira zitatengenezwa na kodi kulipwa.
Lakini kwa hali ilivyo sasa hivi makundi yote mawili A na B yanategemea ajira serikalini na mashirika binafsi ambapo tunakua na tatizo la ajira nchini na nchi inakua na uchumi ambao unakua kwa kasi ndogo kwasababu vyanzo vya kukuza uchumi ni vidogo au ni vilevile kila mwaka.
 
Back
Top Bottom