puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 940
- 1,847
Habar zenu wadau.
Mimi ni mfanyabiashara wa kati, yupo mzee mmoja ni mteja wangu wa muda kidogo...kiasi Cha kuwa rafiki.
Baada ya kuniona namna ninavyofanya biashara yangu...alipenda. akanipa kazi ya kumuandalia mpango wa biashara (Business plan) yenye mtaji usiozidi mil 20, ambayo anataka kumfungulia kijana wake. Nilianza kutekeleza agizo lake ingawaje ilinichukua muda kidogo...maana hata mzee mwenyewe sio mtu wa hovyo...hivyo sikutaka kumchagulia kitu Cha hovyo hovyo...nashukuru Mungu niliamaliza na last week nimemkabidhi.
Sasa baada ya kupitia kwa makini, juzi aliniita ofisini kwake kwa ajili ya kunipa mrejesho. Kiukweli aliipenda Sana na akasema hakuamini Kama Nina weza kuwaza nje ya box kiasi kile.
Ila kilichonishangaza, amesema anataka kunipa kazi nyingine kabla hiyo haijafanyiwa utekelezaji. Kidogo alinipa mashaka kuona anaweza kunidhulumu wazo langu akalitumia bila Mimi kunufaika.
Ila aliweka wazi hana lengo la kufanya hivyo ila baada ya kusoma wazo langu amegundua Nina kitu kikubwa zaidi ya hicho.
Ananiambia nifikirie mradi utakaoweze kuzalisha faida ya 1bilioni moja ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja). Kiukweli nimewaza na kuwazua bado sijapata, Ni biashara gani hasa inaweza kuzalisha fedha nyingi kiasi hicho ndani ya hicho kipindi hicho kifupi. Yani Mil 83.3 kwa kila mwezi.
Ukizingatia hali yetu ya kiuchumi kwa hapa nchini. Naomba tupeane mawazo wadau angalau nipate hata mwanga juu ya hiyo biashara.
Sijui ana malengo gani huyu mzee..ila anaonekana yuko very serious, na business plan ya kwanza amenirudishia ili niondoe hofu juu ya kunidhulumu haki yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app