Biashara ipi inaweza fanyika kwa mtaji wa milioni kumi

marrykate

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
733
442
Habari ya jioni wana jamii.

Mdogo wangu ana mtaji wa shilingi milioni kumi, ila hajapata chaguo sahihi la biashara ipi afanye, alikuwa amewaza kufungua salun ya kiume aiweke iwe na vifaa vizuri na mazingira mazuri , sijui kama itamlipa, je kwa pesa hiyo unaweza kufanya biashara gani hasa kwa maeneo ya mjini.

Yeye anaishi Geita.

Asanteni sana
 
Aingie shambani kulima.na kipindi cha mavuno anunue mazao na kuyaweka gharani kwa kuyauza baadae.biashara hiyo tu ndo itaweza kukuza mtaji wake kwa kipindi hiki.biashara za mjini ni stress kupita maelezo
 
Tafuta sehemu uanze biashara ya Nafaka. Mahindi na Maharagwe.

Wakati nakuja kwa bwana mshauri wetu
Nimepita Biharamulo, Muleba na Bukoba. Vitu hivi ni bei nafuu sana. Utafute ghala la kuhifadhi.

Nimekuta kopo moja la maharagwe(sawa na kilo) wanauza sh 400/=
Sikuamini kabisa.

Maeneo hayo naamini ni jirani sana na Geita. Usafiri hautakugharimu sana.

Ni maoni Yangu tu kwake.
 
hii ni information era.. kuna hela nyingi sana kwenye internet akiwa mjanja..

mimi hapa ukinipa hiyo hela.... nitakuwa na online tv ambayo itasumbua sana nchini... mwaka wa kwanza utakuwa wa introduction stage sitawaza faida hata senti...

mwaka wa pili tu napiga hiyo hela mara kadhaa...

unajua hata hii jamiiforums ni biashara ya mike na max... wametumiaa tu akili zao kupiga hela na wametoa ajira kibao kwa hawa mods wanaotupiga ban..

ukiona huwezi kutumia nguvu kufanya biashara... jitahidi utumie sana akili... utafanikiwa tu
 
"Ukiona huwezi kutumia nguvu kufanya biashara jitahid utumie sana akili"

My first 2018 quote
 
Yeye aliwahi kufanya bia8shara?kabla kupata hiyo hela alikuwa anajishuhulisha na kitu gani?namshauri atulie kwanza.aendeleze alichokuwa anafanya kwa kuongeza mtaji kidogo ili shughuli yake ikue/grow taratibu.balance aiweke fixed deposit.mwenzi...miwli...hata sita.
 
Back
Top Bottom