Inasemekana hapa Tanzania biashara imekuwa ngumu kuliko siku za nyuma.
Hii inaweza ikawa kweli au la.
Kwa ninyi wenye ufahamu na uzoefu wa biashara, je suala hili ni kweli?
kwakweli suala la umeme limeathiri biashara nyingi sana ukizingatia auna ratiba kabisa nfano kkoo wiki nzima kuna lina aipati umeme siku nzima jumapili tu ndio unakuwepo siku nzima siku nnyingine unarudi ucku ebu fikiria hali kama hyo
si mlichagua maisha bora kwa kila mtanganyika -- sasa mnaanza kulalamika nini - tulieni mliwe.
Kwa hiyo tunashauriana nini jamani? Bado nipo njia ya panda mwenzenu.
Mkuu umenena, umeweka ujumbe mfupi lakini ni zito sana kwa wafanyabiashara na wateja.Inategemea biashara unayofanya; kama ni ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Tanzania au imported from Europe and America biashara ni ngumu kwa sababu ya bidhaa za bei nafuu (fake products) toka bara la Asia - China, Singapore na kwingineko. Wanaoingiza bidhaa toka bara asia, mambo ni mazuri sana kwao na ghorofa zinaota kama njugu