Biashara Imechacha Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara Imechacha Zanzibar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CHAMA cha Wafanyabiashara na wenye viwanda na Wakulima Zanzibar [ZNCCIA] kimesema kuwa Zanzibar imemalizwa kiuchumi na Tanzania Bara na sasa wafanyabiashara wakubwa wanahamishia shughuli zao upande wa pili wa Muungano.
  Rais wa chama hicho Abdallah Abass amesema kwamba mikakati ya muda mrefu ya kuimaliza Zanzibar kibiashara imetimia kwani licha ya kuwepo vikwazo visivyo na kodi ndani ya Jamuhuri ya Muungno wa Tanzania mashaka mengine yataikumba Zanzibar chini ya soko la pamoja la Afrika Mashariki.

  Alisema matatizo mengi yanachangia kuwakimbiza wafanyabaiashara wa kizanzibar kuwekeza visiwani hapa ni kuwepo kwa taasisi nyingi zinazosimamia maswala ya kodi katika kisiwa kidogo kama Zanzibar na kuitolea mfano TRA na ZRB kuwa zinaongeza urasimu kwa wafanyabiashara.

  Mbali na vikwazo hivyo lakini pia wafanyabiashara wa Zanzibar wanailalamikia Serikali kwa kutokuonyesha umakini kutoshughulikia kero za zinazowasumbua wananchi na wafanyabiashara kwa ujumla ikiwemo wasafiri wanaotoka visiwani Zanzaibar ambao tayari huwa wameshafanyiwa upekuzi kwani wanapofika bandari ya Dar es Salaam hupekuliwa tena kama wanatoka nje ya nchi.

  Raisi huyo alisema kuwa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) inawaona wafanyabiashara kuwa ni maadui badala ya kuwafanya ni sehemu ya ufanikishwa wa maendeleo ya nchi kwa kuwashirikisha katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.

  Alisema kitendo cha operesheni za kivamizi kinachofanyw na maafisaa wa ZRB kwa kisingizio cha kuwatafuta walipa kodi wasiolipa na kuwapiga faini ya laki tatu kila mmoja kuwa kinawarejesha nyuma wafanyabiashara
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwani Bara si kuna soko kubwa zaidi na pia ni sehemu ya Jamhuri ya Muunguano??

  Mtu anaangalia faida..na sii siasa!
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tatizo la ndugu zetu wa visiwani ni kutafuta visingizio vya matatizo yao huku wakiyafumbia macho mambo ya msingi yanayowasibu kuhusu uchumi wao! Uchumi wa Zanzibar unahujumiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wakishirikiana na wafanyabiashara wa nchi za nje; mfano mzuri ni biashara ya utalii ambapo katika mahoteli mengi makubwa, viongozi wa chama cha mafisadi na serikali wameingia ubia na wawekezaji hasa wa kitaliani ambapo mapato mengi yakuweza kuindeleza Zanzibar kwa kila nyanja hayaletwi visiwani bali watalii wanalipa huko huko nje, na fedha kubakia huko at the detriment of the Zanzibar economy! Hilo ndilo tatizo kubwa ambalo wazanzibari wanatakiwa kulitatua badala ya kulalalmiakia TRA!!
   
 4. Mzeeba

  Mzeeba Senior Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli wanachanganya mambo hawa ZNCCIA. Kama mazingira ya biashara ni magumu visiwani lazima wafanyabiashara makini wataondoka. Kama wanaona au wanajua tatizo ni ZRB mambo ya bara yanaingiaje hapo? ZNCCIA ni chombo kikubwa na natumaini chenye ushawishi visiwani, wakae chini watafiti na kutoa mapendekezo ya namna gani mazingira ya kibiashara yaboreshwe visiwani na sio kutoa malalamiko ya juu juu tu. Kutaja bara hakuzidishi ukubwa wa tatizo bali kunafanya suluhisho kuangaliwa kisiasa badal ya kibiashara
   
 5. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama huelewe ni vyema ukafumba Ch----- chako.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Wazanzibar tujiulize kwanini tunafika hapa? akti Wa Dr salimini , wabara kibao walikuwa wakija Znz kununua bidhaa, vp sasa mbona tofauti?

  lazima tujikomboe kutokana na huu ukoloni mamboleo
   
 7. l

  lovulovu Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wazanzibar tujiulize kwanini tunafika hapa? akti Wa Dr salimini , wabara kibao walikuwa wakija Znz kununua bidhaa, vp sasa mbona tofauti?

  lazima tujikomboe kutokana na huu ukoloni mamboleo


  mimi lovulovu nashangaa sana. biashara kuwa mbaya ndugu yangu huyu anadai wazanzibari wajikomboe na ukoloni mambo leo. tatizo ni mazoea ya kulelewa kama makinda.

  wapo watu wanaishi zanzibar lakini hawatumii busara katika kujadili mambo ya biashara badala yake wanayajadili kisiasa. eti mtu anaagiza bidhaa ng'ambo akijua fika kabisa kuwa soko lake liko bara lakini yeye anaamua kutelemsha bidhaa hizo zanzibar na kulipishwa ushuru kidogo na baadaye kuleta bidhaa hizo bara akidai ni ndani ya Jamhuri ya Muungano asilipishwe kodi!

  mtu huyu ndiye anayetugonganisha. na mwingine anafanya hivyo hivyo lakini yeye anauzia huko huko zanzibar na hataki wanunuzi wake ambao wanatoka bara walipishwe ushuru wa zida sawa na watz wengine wanaotumia bandari ya dar!

  maana ya msimamo huu wa watu wasiotumia busara kulitafakari suala hili la biashara ni kwamba mtu anayetumia badnari ya dar auze bidhaa zake kwa sawa na yule anayetumia bandari ya zanzibar wakti yule wa zanzibar alilipa ushuru kidogo! kwa nini ndugu zetu hawa hawataki usawa katika biashara? kwa hili hakuna anayependelewa kwa sababu mtu yeyote bila kujali ni mzanzibari au mbara anatendewa hivyo kila anapoingiza bidhaa kutoka ZNZ kama hazikulipiwa ushuru sawa na ushuru unaolipwa dar kwa bidhaa hiyo.
  jama acheni kulalamikia hata yasiyotaka ulalamishi.
  lovulovu
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Hivi lile wazo la Zanzibar Free Port kama Dubai limeishia wapi?

  2. Ila isiwe free port..halafu hizo bidhaa zinaletwa bara kwa bei ya chni kwa vile kuna soko kubwa!
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo la kuchacha kwa biashara lilianza baada ya biashara katika Zanzibar kuwa juu sana katika Afrika Mashariki, na ilikuwa ni kipindi hiko hiko cha Dr. Salmin. Hii ilisababishwa na baadhi ya watendaji wake wakuu kushindwa kudhibiti mbinu za muda mrefu za viongozi wa ngazi zao toka Tanzania Bara.

  Viongozi hawa walishindwa kabisa kulinda soko la biashara la Zanzibar, kwa kukubali kila pendekezo ambalo lilikuwa linatolewa na Viongozi wa Tz Bara katika vikao vyao mbalimbali. Viongozi hawa wakiongozwa na Mawaziri wa SMZ mwenye kuhusika na sekta ya biashara na mapato walikuwa wakuburuzwa sana katika vikao vilivyokuwa na lengo la kuimaliza Zenj kibiashara.

  Wafanyabiashara wa Zenj waliliona hili mapema, hata hivyo jitihada zao za kuwafumbua macho viongozi hao ziligonga ukuta. Niliwahi kuongea na Mfanyabiashara mmoja mkubwa sana visiwani humo, ambae aliniambia katika kipindi cha miaka kumi ijayo biashara nyingi zitakuwa zimehamia bara, na wafanyabiashara wengi wa zenj wanaweza kuwa na biashara kubwa nje ya Zanzibar. Hili sana limetimia.

  Kuchacha kwa biashara kwa Zenj kumesababishwa na viongozi ambao hawakuwa na misimamo dhabiti juu ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar na namna ya ukusanyaji wa mapato kwa faida ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Wengi walilemewa sana kiufundi na wenzao wa Bara na kujikuta wanaingia katika mtego, ambao sasa ndio tunaona matunda yake.

  Ni vigumu kwa sasa kuja na njia mpya ya kurudisha hali ile ya zamani pasipo kuwepo na mgongano mkubwa kwa jamii nzima ya Visiwani na Bara. Hii inatokana na jinsi hali ya sasa ya kisiasa ilivyo na hasa juu ya hatima ya muungano.

  Cha msingi ni kwa wafanyabiashara pamoja na serikali kuandaa njia nyingine ya muda mrefu ambayo itawezesha Zanzibar kurudi katika hali yake ya zamani, pasipo kuwepo na impact kubwa kwa jamii.
   
 10. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mzee wa Bia,

  Hapo umeongea!! swala la kujiuliza ni kwa nini SMZ inapelekwa watendaji lege2 ktk majadiliano na SMT?? Negotiation skills ni muhumu sana..SMZ wakipenda wanaweza kuwachukua watendaji wao ktk mafunzo ya negotiation skills..au hata wakaajiri na kumlipa Mtaalamu za Kunegotiate!

  Fikiria..Tanzania na US eti wanakaa meza moja ya majadiliano..wakati US wana utaalamu wa kutisha na unashangaa yaani nyie mnaenda na watu watano na wao wanaleta watu 100 tena waliobobea!

  Sasa kuna haja SMZ wajipange tena upya!
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo hili limechangiwa sana na SMZ kujaribu kuiga mambo mengi toka SMT, pasipo kujua yepi yanawafaa na yepi ya hayawafai kuyaiga.. Kama shuleni ni kudesa/phatom/ngima/.... Hii ikasababisha watendaji wengi kutokuwa na nguvu ya kusimamia hali halisi ya Zenj.

  Mbaya zaidi wengi wao walikuwa katika nafasi hizo kisiasa zaidi kuliko kitaaluma, na kujikuta wakiburuzwa katika vikao vingi vya pamoja, licha ya kuonekana ni wakali wakiwa Visiwani.

  Kiburi cha kutosikiliza maoni ya wafanyabiashara ama kuwashirikisha moja kwa moja nako kulipelekea kwa wajumbe hao kuwa vibonde sana wakivuka Chumbe na kuingia Bandari Salama.
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  These guys are narrow minded.
  Wigo wa bara kwenye biashara ni maradufu ya visiwani na ndiyo maana wafanyabiashara wengi wamehamia bara kwa sababu ya faida. Lakini jee hiyo faida wanawekeza wapi? jibu ni bara tu kwani returns ni kubwa pia.
  ZRB ni mali ya SMZ mnalalamika hivyo jee ingekuwa TRA ingekuwaje??????
  Acheni kulalamika na kama mnauona muungano hamuutaki si mseme tu?
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kheee heee heeee...Eeh!
  Hao TRA mipaka yao inaishia wapi kwa ufahamu wako? Na ZRB wanakusanya nini baada ya TRA?
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi ni kwa nini TRA wakusanye kodi Visiwani? Kodi hii hukusanywa kwa niaba ya SMZ?

  Kwani vyombo vya kukusanya kodi Visiwani vinafanya nini??

  TRA wanakusanya ngapi na ZRB ngapi??

  Kodi inayokusanywa Visiwani ni kiasi gani kwa mwezi/mwaka??

  Naomba mwanga!
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sina data kamili za kiasi gani zinazokusanywa, lakini vyombo hivyo viwili vinafanya kazi visiwani humo, hata hivyo ni TRA ambayo inasikika zaidi kuliko ZRB, nafikili wanakusanya kodi tofauti. Kwa ufupi TRA wanachokusanya kinakwenda kwanza SMT kabla ya kurudi kwa kiasilimia SMZ.

  Kwa kumbukumbu tu TRA ilipoingia Zenj, ndio ulikuwa mwanzo wa biashara kuanza kuchacha.
   
Loading...