Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Mkuu hii inaitaji akili na kipaji pia alafu usipingane na nafsi yako huku ukiwa risk taker Mimi niliwai better 450 bet power team 24 nikachomoka na laki Saba na sitina tisa elfu kila mtu alishika mdomo
Uliendelea na kubet?au ulizifanyia nn€
 
Katika hustle za maisha huwa watu tunajaribu Biashara mbali mbali ili kuweza kufanikisha malengo yetu lakini Wengi wetu huweka Mitaji mikubwa pengine pesa za Kukopa lakini mwisho wa siku Changamoto zikiwa nyingi tunakata tamaa na Kuacha.
undefined
Mimi binafsi nakumbuku nilianza biashara ya kuuza saa za kike na viatu vya kike lakini changamoto kubwa ikawa ubora wa zile bidhaaa aisee nilipata malalamiko mengi sana Nikaamua kuacha Laiti ningejua ningeborasha ubora wa zile bidhaa tu pengine leo ningekuwa na mtaji mkubwa sana.
undefined
Karibuni tushirikishane kuhusu Bishara gani ulianzisha changamoto ulizopitia na ulizitatua vipi au uliacha??? Uzi huu unaweza kuwa mwanga kwa watu wengine pia.View attachment 1203317
undefinedundefined
 
Kipindi niko first year chuo nlinunua bodaboda mbili aisee io changamoto yake usipime stres tupu madereva pasua kinoma nikapiga chini nikaziuza zote aisee
2 years ago, nami nilinunua mbili nikawapa boda boda, dereva wa kwanza alikuwa analeta day ila akinipigia sim, jua yupo kwa fundi ameshagonga mbwa barabarani, ikawa no mwendo wa kubadilisha spea almost kila week, huyu mwingine yeye alikuwa ajigusi kabisa, ni misele tu na akichoka anapaki bar atakayopata ndio hiyo hiyo kama mpo share. Nikanyang'anya wote nikaachana na hiyo biashara...
 
So biashara ya Bodaboda mkuu hata ukipata mtaji leo hufanyi??
Kama utakuwa na pesa ya ziada na una uwezo wa kutunza pesa unampa mtu mkataba wa bodaboda kuanzia miezi 10 had 12 kulingana na aina ya pikipik na mahali ingawa pia anatakiwa awe na dhamana na wadhamini. Labda inaweza saidia..., vinginevyo upate kichwa iliyotuliwa sana, mana vijana wanae wenge sana barabarani.
 
Binafsi biashara yangu ya dawa za nguvu za kiume..dawa wa uzazi za wanawake na kuongeza shape zinaniendea vizuri tu Sina changamoto.
Duuh hii hizi dawa kweli zinafanya kazi hasa za shape?? Au utapeli
 
2 years ago, nami nilinunua mbili nikawapa boda boda, dereva wa kwanza alikuwa analeta day ila akinipigia sim, jua yupo kwa fundi ameshagonga mbwa barabarani, ikawa no mwendo wa kubadilisha spea almost kila week, huyu mwingine yeye alikuwa ajigusi kabisa, ni misele tu na akichoka anapaki bar atakayopata ndio hiyo hiyo kama mpo share. Nikanyang'anya wote nikaachana na hiyo biashara...
Madereva wanazingua sana aisee..
 
Niliwahi shiriki kilimo cha mpunga cha kutegemea mvua. Niliishia kuvuna fedheha. Nililima misimu miwili. Imagine kwenye plot ambayo the precious year imetoa gunia 25 we unavuna gunia 5. Msimu ujao nasubiri mavuno kisha ninunue zangu mzigo niweke stoo niuuze soko likikaa vizuri.
 
Bora hii aisee ya kununua na kuweka stoo
 
Bora hii aisee ya kununua na kuweka stoo
Na changamoto kubwa katika kilimo ni usimamizi mzuri. Unakuta mtu yuko Dar ila anajiita mkulima kwa kuwa na shamba la mpunga huko Kyela. Kila siku unapigiwa simu mara mbolea inahitajika, mara dawa unatuma hela, mtu anaenda kupiga picha shamba la jirani kisha anakutumia. Basi unajua mavuno yatakuwa ni mazuri. Ukifika msimu wa mavuno jiandae kupokea Breaking News.
 
unafanya kilimo online...siku ya Kuvuna ndo suprise kama zote
 
Back
Top Bottom