Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
21,448
41,808
Katika hustle za maisha huwa watu tunajaribu Biashara mbalimbali ili kuweza kufanikisha malengo yetu lakini wengi wetu huweka mitaji mikubwa pengine pesa za kukopa na mwisho wa siku changamoto zikiwa nyingi tunakata tamaa na kuacha.

Mimi binafsi nakumbuka nilianza biashara ya kuuza saa na viatu vya kike lakini changamoto kubwa ikawa ubora wa zile bidhaa. Aisee nilipata malalamiko mengi sana nikaamua kuacha. Laiti ningejua ningeboresha ubora wa zile bidhaa tu pengine leo ningekuwa na mtaji mkubwa sana.

Karibuni tushirikishane kuhusu biashara gani ulianzisha, changamoto ulizopitia na ulizitatua vipi au uliacha?

Uzi huu unaweza kuwa mwanga kwa watu wengine pia.
1581427149863.png
 
Forex
Baada ya kuvutiwa na uzi wa kwanza kabisa. Mzee nikapakua vitabu msuli ile ile mixer YouTube. Nikaanza kupiga practical ya live cent ya 1$ kwa 100$.

Hahahah nusu mwaka no development leo nikipata profit ya 5$ kesho nachoma 20$
Nikapiga chini na nishaisahau
 
Forex
Baada ya kuvutiwa na uzi wa kwanza kabisa. Mzee nikapakua vitabu msuli ile ile mixer YouTube. Nikaanza kupiga practical ya live cent ya 1$ kwa 100$

Hahahah nusu mwaka no development leo nikipata profit ya 5$ kesho nachoma 20$.

Nikapiga chini na nishaisahau
Yani unazungumzia dola 100 Tena ya cent account wakati Kuna watu wamechoma dola zaidi ya 5000 na bado wapo kwenye game.
 
Kipindi niko first year chuo nlinunua bodaboda mbili aisee io changamoto yake usipime stres tupu madereva pasua kinoma nikapiga chini nikaziuza zote aisee
Wewe mimi kabisa hii biashara niliitamani nimenunua boda nikampa dereva mwanzoni hela ya hesabu wanaleta vizuri kati wanabadilika mpaka hela ya hesabu ikifika mimi ndio nimtafute na kumfata kwake.

Jamani hii biashara ina presha mwisho wa siku nikaiuza na boda yenyewe sitaki hata kuisikia mtu aniambie mambo ya kufanya biashara ya boda.
 
Mkuu hii inaitaji akili na kipaji pia alafu usipingane na nafsi yako huku ukiwa risk taker Mimi niliwai better 450 bet power team 24 nikachomoka na laki Saba na sitina tisa elfu kila mtu alishika mdomo
Dadekii hivi unaangalia vitu gani mkuu embu npe ujanja maana mpaka apps kama footmob za kuangalia statistics za timu nlkuwa nayo lkni wap
 
Back
Top Bottom