Biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya bila kuathiri masomo yake

kuuza boksa, chupi, kuuza ubuyu wa zanzibar, kuuza mapochi, kuuza bisi(popcorn) kuuza urembo wa wanawake(hereni, nk) kuuza vipodozi asilia manjano, scrub za asili, vitu vyote mtaji wake ni elfu 5 na kuendelea maximum hata elfu 20 unaanza biashara, vinaweza bebeka kwenye begi lako ukatembea navyo kokote. All the best
Shukran ndugu yangu
 
Sikia mzee baba

mimi nikiwa chuo biashara yangu kubwa ilikua ni kukodisha PAMBA KALI

Mimi nilitoka na nguo zangu kali zote home,yani siku naenda chuo nlienda na begi kama Mkimbizi

ila kichwani nilikua najua WHY,nimefika chuo nilichokifanya ni ku deal na masharobaro,hela hawana ila wanataka kupendeza

nakupa kiatu unaenda unapotaka unaniachia 5000 yangu,kofia,saaa,cheni,miwani hivyo vyote nilianza na Vyangu mwenyewe

na wala sikuanza na vya kununua maana sikua na hela, Hii biashara nilianza kama ku test tu maana nili iga kwa msela angu tulipokua advance ilikua ndio zake (yule mwamba kala hela zangu sana)

Nikajiapia nikifika chuo hii ndio itakua biashara yangu..So kuanzia nikiwa five nilikua nanunua viatu nguo,saa,kofia yani vile vitu ambavyo ukikiona lazima ukitamani.

Mzeee nimefika huko chuo Nilikua Q bOy msafi nakodisha nguo na hela ipo aseeee..

Piga hii ishu kama una viwalo vya kuanzia,ukiwa chuo acha urafiki mandazi

eti shost/mwana anakuja anakugongea nguo Aseee mwambie PESAAAAAAA
 
kINGINE Mzeee baba Geuka DOBI

chuo mijitu mivivu sana sana ,wewe ondoa usharobaro nunua mabeseni,nunua ndooo

vifaaa jikoki then ROOM yako andika pale Juuu DOBI yupo hapa,weka namba zako za simu

Baba unapokea nguo,unazifua usiku kama mchana huna kipindi lala pumzika,Usiku watu waliofua mchana

wameanua nguo woteeee wewe ndio muda unafua unajaza mikamba,BABA lakeeeee Utanikumbuka nakwambia.
 
Jifanye kama Chizi flani hakikisha unakaaa hostel then

Nunua mabeseni makubwa ya kufulia ndoooo ndoooo then Kodisha

Usikose pipa la maji muraaa hakikisha pipa lako lina maji 24hrs

Chuo ipo day tu maji yatayumba,sasa maji yakiyumba wewe hiyo ndo siku unapiga bingo muraaa

yani uza ndooo zako pipa likiisha mfukoni unamkwanja mzuriiiii
 
Nunua vocha za kukwangua za uwezo wako

then jitangaze kuwa unauza vocha at any time mzeee Utanikumbuka

Laini yako hiyo unayoitumia yaweza kua unatumia tigo,voda,eatel

nenda tigo shop au eatel shop depend na mtandao wa simu unaotumia

Wambie wewe ni mfanya biashara unataka laini yako iunganishwe na huduma ya VOCHA ZA KURUSHA + vifurushi

hiyo huduma ni bure kabisa watakuunganisha laini yako itakua na uwezo wa kuuza vifurushi + rusha vocha

utakua ukifanya hiyo biashara Chuo aseee mkuuuu Vifurushi vina hela sikia tu kwa jirani nakwambia
 
Biashara ya kufanya ukiwa chuoni huwa ni moja tu mkuu. KUSOMA KWA BIDII!

Angalia sana uwezo wako kabla hujajikita na kugawa muda wako. Watu huwa wanachanganya haya mambo na matokeo yake yote mawili yanashindwa!

Ukiishi kama mwanafunzi, uka control maisha yako na kujiweka kwenye nafasi ya mwanafunzi utatoboa ila ukitaka kuwa mwanafunzi lakini akili na spending kama za mfanyabiashara/mfanyakazi utajikuta unatawaliwa na ufanye biashara gani.
 
Kama umepanga geto hakikisha umenunua Flat Tv

nunua king'amuzi cha azam weka magetoni,

mechi za ligi kuu zikianza baba la baba Onyesha mechi kila mwana ataetaka kuja geto chaji jero

wajaze hadi kitandani, washindilie humo ndani vya kutosha,
 
Biashara ya kufanya ukiwa chuoni huwa ni moja tu mkuu. KUSOMA KWA BIDII!

Angalia sana uwezo wako kabla hujajikita na kugawa muda wako. Watu huwa wanachanganya haya mambo na matokeo yake yote mawili yanashindwa!

Ukiishi kama mwanafunzi, uka control maisha yako na kujiweka kwenye nafasi ya mwanafunzi utatoboa ila ukitaka kuwa mwanafunzi lakini akili na spending kama za mfanyabiashara/mfanyakazi utajikuta unatawaliwa na ufanye biashara gani.
Mawazo ya kimasikini kabisa, hapa limtu litamaliza chuo alafu lirudi kwao kwenda kusubiri ajira ambazo azipo, biashara zinaanzia chuo baada ya chuo ni mwendelezo. Ukisoma tuu utafaulu tuu alafu unaweza kufeli maisha, sasa kipi bora?
Watu tunasoma na mishe mishe tunafanya, tunapata ela ya kujikimu na tunafaulu pia mkuu,
Sorry kama nitakua nimeku-crush mawazo yako ila dogo awaze vizuri aanze chap kwa haraka
 
Hujani crush ila mawazo yangu sio ya kimaskini nina hakika. Wakati nasoma sikufanya biashara nilisoma tu nikatumia muda kusoma na sasa mimi si masikini pia maana natumia muda kufanya kazi na biashara na si kusoma simple!
 
Biashara ya kufanya ukiwa chuoni huwa ni moja tu mkuu. KUSOMA KWA BIDII!

Angalia sana uwezo wako kabla hujajikita na kugawa muda wako. Watu huwa wanachanganya haya mambo na matokeo yake yote mawili yanashindwa!

Ukiishi kama mwanafunzi, uka control maisha yako na kujiweka kwenye nafasi ya mwanafunzi utatoboa ila ukitaka kuwa mwanafunzi lakini akili na spending kama za mfanyabiashara/mfanyakazi utajikuta unatawaliwa na ufanye biashara gani.
Mtu had amefika chuo means anajitambua na anajua kilichompeleka huko ni nn....

Cha muhim ni kubalance mda vzuri wa kusoma na kujishughulisha. BTW ratiba ya chuo iko flexible so mda mwingi mtu unakua free u can make something productive kuliko kulala tu hostel
 
Kuna vijana walikuja nyumban kwangu jumamosi asbh wa chuo wakaniambia wanafanya usafi wa nyumba pamoja Na kufua wajaniachia business card
 
Nunua macover ya simu chaji earphones protectors etc na accesories za simu kutoka kkoo na kwa masupplier wakubwa kwa bei ndogo then uza kwa wanafunzi wenzako hasa hasa mademu. Kuwa mwaminifu utapata deals kibao ata mali kauli utapata kwa wenye mali wakubwa. Utapiga pesa sana cha msingi build network yako ya wateja huku ukikuza mtaji ata kesho ukimaliza chuo utakuwa ushakomaa ni muendelezo tu.
Ila dogo chondechonde umeenda chuo kusoma hakikisha unakomaa na shule usisahau kilichokupeleka shule piga msuli huku unapiga biashara ni ngumu ila inawezakana usiige maisha ya wengine.
Take this advice and thank me later
 
Well said broo!!! Be blessed asee
 
Habari wana JF,

Naomba kuuliza kwa wale wazoefu, naomba ushauri ni biashara gani nzuri ambayo naweza kuifanya nikiwa chuoni. Ushauri wenu ni muhimu sana, pia nitashukuru na kuyafanyia kazi.

Asanteni.
Kama upo TIA karibu mbagala hapa tupeane mawazo, tatizo la biashara nyingi wanazofanyaa wanachuo huko chuoni hazina future unakuta boom likikata nayo imekata akienda likizo imekufa alimaliza chuo ndio zinakufa kabisa inakuwa Kazi bule...nashauri fanya biaashara yenye ofisi mfano uwakala hapo naeneo yanje ya chuo unaweka kibanda nk ukicheza kamari vizuri utakuta unamaliza una vibanda vitatu.
 
Back
Top Bottom