Biashara ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kufanya bila kuathiri masomo yake

Hapo chuoni kuna watu wana vibanda vya aina zote za biashara na ndiyo shughuli yao. Utashindana nao vipi?
Kama unasoma Sayansi sahau biashara. Kama umechaguliwa kozi zingine lainilaini endelea kusubiri maoni. Kusoma pia ni uwekezaji. Mshika mbili moja humponyoka.
 
Hapo chuoni kuna watu wana vibanda vya aina zote za biashara na ndiyo shughuli yao. Utashindana nao vipi?
Kama unasoma Sayansi sahau biashara. Kama umechaguliwa kozi zingine lainilaini endelea kusubiri maoni. Kusoma pia ni uwekezaji. Mshika mbili moja humponyoka.
Mkuu nataka nifanye hivi kutokana na hali yangu ya maisha pindi niwapo chuoni na pia sisomo science...
 
km unaweza fanya saloon ya kiume m mwenyewe nipo chuo UDSM-duce nilifungua saloon then nikafungua mgahawa so saiv shida nimetupa kuleeeeee saloon napata 60 kw wik na mgahawa sikosi kuanzia 30 to 50 per day .km upo dsm njoo inbobo

Sent from my T800 using JamiiForums mobile app
mkuu niambie ulifanyaje Tafadhali maana nina mpango wa kuanzisha salon lakn capital sio enough sasa sijui nitapataje ya kuongezea

Sent from my HUAWEI Y360-U82 using JamiiForums mobile app
 
Habari wakuu...

Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili kutokana na sababu mbalimbali imenibidi kufikilia kufanya biashara ila hadi sasa nimefikiria kufanya biashara nyingi sana ila lengo la biashara nayo niliyopanga kufanya ni ile ambayo haitaingiliana sana na masomo yangu pindi niwapo chuoni...

Kwa nini nimekuja hapa katika jukwaa hili?
-jambo la kwanza naomba mnoshauri biaahara ipi ninaweza fanya na mbinu ya ufanisi katika kufanikisha biashara hiyo?

Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu coz sisi tumepia vyuoni kama wewe,unaweza ukadharau hii biashara but amini nakuambia unaweza ukawa kila siku unatoka na 20,000/

Tafuta Kibegi cha mgongoni nenda kwenye maduka ya jumla nunua pipi zile za kisista duu yani pipi kijiti au hata ivory,gum like Batook,n.k,vocha za kukwangua na kurusha,biskuti,karanga,tambi na hata ubuyu.then uwe unazunguka campus amini utauza sana coz maeneo mengi ya chuo biashara hizi hazipo(hawaruhusu machinga kuingia chuoni).sasa kwa vile watu ni wavivu kuvuka barabara au kutembea kufata pipi au biskuti au vocha madukani we utatumia advantage hiyo kupiga salio.

Biashara za kipuuzi ndo zinalipa sana bora tu usiwe na aibu,uzuri wa biashara hii ni kwamba haiitaji usimamizi ofisi ni mgongoni mwako,haili muda wako wa masomo,unaweza kuifanya hata darasani wakati lecture inaendelea,haina usumbufu wa TRA,easy to carry,watu wakishakuzoea ndo nafasi yako nzuri ya kupiga hatua 1000 ahead!

kila la heri!!
 
Hapo chuoni kuna watu wana vibanda vya aina zote za biashara na ndiyo shughuli yao. Utashindana nao vipi?
Kama unasoma Sayansi sahau biashara. Kama umechaguliwa kozi zingine lainilaini endelea kusubiri maoni. Kusoma pia ni uwekezaji. Mshika mbili moja humponyoka.
Huna Facts.
1.Kuna watu wamesoma course ngumu chuoni na bado wamefungua kampuni bado wakiwa chuoni.
2.Biashara si za vibanda vinavyozunguka eneo uliopo tu..biashara popote.


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nikushauri kitu mdogo wangu coz sisi tumepia vyuoni kama wewe,unaweza ukadharau hii biashara but amini nakuambia unaweza ukawa kila siku unatoka na 20,000/

Tafuta Kibegi cha mgongoni nenda kwenye maduka ya jumla nunua pipi zile za kisista duu yani pipi kijiti au hata ivory,gum like Batook,n.k,vocha za kukwangua na kurusha,biskuti,karanga,tambi na hata ubuyu.then uwe unazunguka campus amini utauza sana coz maeneo mengi ya chuo biashara hizi hazipo ndani ya maeneo ya chuo(hawaruhusu machinga kuingia chuoni).sasa kwa vile watu ni wavivu kuvuka kutembea kufata pipi au biskuti au vocha we utatumia advantage hiyo kupiga salio.

Biashara za kipuuzi ndo zinalipa sana bora tu usiwe na aibu,uzuri wa biashara hii ni kwamba haiitaji usimamizi ofisi ni mgongoni mwako,haili muda wako wa masomo,unaweza kuifanya hata darasani wakati lecture inaendelea,haina usumbufu wa TRA,easy to carry,watu wakishakuzoea ndo nafasi yako nzuri ya kupiga hatua 1000 ahead!

kila la heri!!
Hii ni kweli kabisa nakuunga mkono 100%

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Huna Facts.
1.Kuna watu wamesoma course ngumu chuoni na bado wamefungua kampuni bado wakiwa chuoni.
2.Biashara si za vibanda vinavyozunguka eneo uliopo tu..biashara popote.


Post sent using JamiiForums mobile app
basi mpe mbinu kama alivyoomba itakuwa poa
 
VIGEZO (1) MTAJI (2) MUDA (3) CASHFLOW (4) FAIDA (5) GROWTH


1. MLM:

Hi ndio biashara moja ambayo wanafunzi wengi Ulaya wanapiga pesa sana sasa hivi imefika Tanzania na Kenya: Nchini Nigeria mamilionea wengi vijana wametokea katika mtandao huu. Kenya pia na SA vijana wengi wamejikita katika biashara hii. MLM ni Mult Level Marketing.
NAMNA YA KUANZA:
Kwa kifupi biashara hii unahitajika kuwa mwanachama wa kampuni inayo sambaza bidhaa kwa mtindo wa MLM au mtandao, ndipo ununue bidhaa katika bei ya chini uzitumie au uuze kwa rejareja. Na kisha ualike watu wengine wengi nao wawe wanachama wa kampuni hiyo ya MLM, kila mwanachama unaye mwalika utalipwa kiasi flani cha pesa yake ya manunuzi ya bidhaa. Mtaji wa kuanzia katika kampuni hizi ni SIFURI had Million 10. KAMATA FURSA
KWA NINI WANAFUNZI/WANACHUO? Haihitaji mtaji mkubwa incase huna, haihitaji muda mwingi, hauhitajiki leseni wala huhitaji mwuza duka. Kuna uwezekano mkubwa wa wewe kufanya biashara na dunia nzima katika sekunde moja kama utafuata mbinu utakazofundishwa. Makapuni yanayojihusisha na biashara hizi yamejikita katika bidhaa za afya, urembo, kilimo na airtime.
UWEZEKANO WA KIPATO: SIFURI hadi BILLIONEA ndani ya siku 30 hadi miaka mitano. Utaweza kuona kama mwanafunzi ukiingia katika biashara ya MLM mwaka wa kwanza na ukatumia boom lako vizuri utakapokuwa unamaliza chuo utakuwa unatengeza pesa sawa na mtu aliyeaajiriwa au umemzidi kabisa. Sasa ajira hapo utaitafuta kwa maringo bila presha.
SECRET BEHIND SUCCESSFUL PEOPLE: Kuzungusha mtaji mara nyingi, kualika watu wengi kwa kadri inavyowezekana. Mtaji wako ni wanafunzi uliosoma nao na unaosoma nao.




2. MOBILE MONEY:
(M-PESA, EAZY PESA, TIGO PESA NA AIRTEL MONEY)
Hii inajulikana sana but ili upige pesa vizuri inabidi uwe na float nzuri hapo chuoni kwako kuanzia 1,000,000 hadi 10,000,000 kwa siku. Au laki3 kama upo karibu na benki au super dealer itakuwa safi. Faida ni kubwa mfano mtaji wa 300,000 sehemu ya mtaani tu inakupa 45,000 hadi 120,000 kwa mwezi. Mungu akupe nini? Gunia la chawa? Biashara hii ni rahisi sana kwa mwanfunzi maana unatembea na duka lako, muuzaji wewe wateja unao kila saa darasani, lecture room, discussion, disco na nyumba za ibada. KAMATA FURSA




3. MUDA WA MAONGEZI (AIRTIME): KAMATA FURSA HII, sio ile ya zamani ambayo unauza vocha za kukwangua, hapa unauza muda wa maongezi. Ukisha kuwa na mobile money basi wewe jiunge na RIFARO Africa utapiga pesa. Line za ZANTEL, TIGO na AIRTEL pia wanakuunga. Kifupi ni kwamba hii Rfearo ni mkama MLM lakini wao wapo kwenye airtime. Unahitaji mtaji kidogo kati ya elf77 na 150. Kwa maelezo zaidi google Rifaro Africa au whatsapp or text me +255 752 693 692.



4. UANDISHI WA VITABU au DOCUMENTARY:
Haya vijana wa IT na wale watundu wa simu na computer, wale mnaopenda umbea na udaku sasa umbea na uduku uweke kitabuni kwa staili tofauti. Andika story za maisha, umeshazisikia ama wewe mwenyewe au zile za kufikirika, weka kwenye laptop yako au flash disk uza kwa wachapishaji. Inaweza kuwa short story au series ili mradi iwe ya kuvutia. Jifunze namna rahisi ya kutengeneza documentary za kuvutia kisha rusha facebook na mitandao ya kijamii wafanya biashara watakutafuta kwa ajili ya kutengeneza matangazo yao.


5. UTUNZAJI BUSTANI
wewe kijana wa SUA hii inakuhusu nenda mjini tafuta watu wanohitaji kutunziwa bustani zao za nyumbani hasa UKOKA, unda timu za vijana wasimamie mara kwa mara. Hii biashara inalipa sasa ivi town. Wewe kazi yako ni mipango tuu – aka – Manager. Mbolea za maji safi kabisa ambayo unaweza weka mfukoni sasa hivi zipo Tanzania, lita moja inatosha ekari2 unusu




6. BETTING AMA WANAITA MKEKA: Vijana hapa sina la kuongeza mana wengi mnapiga hela wekeend kama hamna akili nzuri, kuna betting website mbili Tanzania ambazo zipo juu (1) MERIDIAN (2) MBET na moja haiko online (3) PREMIER BETTING. Kama unataka kupunguza risk ya kupoteza cheza online betting ingawa premier betting nayo ni bomba vijana mnaijua. ONYO betting ni addictive na unaweza poteza boom lako usipokuwa makini, be responsible.



7. DALALI: Chagua eno lako moja la udalali hasa hasa unalolijua sana, kama magari, computer, simu, viwanja yaani vile vitu watu wanavitafuta na vina bei kubwa. Tumia blogs, face book, jamii forum na matangazo madogo magazetini kuuza. Hapa unaweza piga pesa ndefu ya kutosha mwaka mwaka 1



8. MC: Nasema kama wewe ni mdakuzi na m-mbeya wacha kuumiza shingo na kichwa kwa umbeya wako, tengeneza hela kuwa MC mtaji kidogo unahitajika kama nguo za kazi, mike ya kisasa na music system. Anza na vipati/vishereha vidogo vidogo kama birthday parties, mikutano midogo, send offs na hatimaye utajikuta upo harusini, mikutano mikubwa ya injili na ya kimataifa.




9. NM – Network marketing,
Hii sawa na udalali ila hapa unauza vitu vyako matandaoni tu, yaani matangazo yako yote yapo mtandaoni, wateja wako wote wako mtandaoni. Wewe unacheza na simu na laptop, au tablate au hizo computer za chuo. Tembea na mooderm muda ukifika wa kuuza unaunga modern unapiga kazi le say 1 hour per day inatosha, wenye shida watakutafuta. Kama huna bidhaa ya kuuza nitafute nikuelezee bidhaa lukuki za kuuza huko mitandanoni.



10. BLOGGER:
Sasa unaweza ku-blog kwa raha zako au kublog kwa kuuza products ikiwa utakuwa umechagua moja kati ya miradi hii hapa 1,4,5,7,8,9,11,14,15 basi ili uuze usiku na mchana huna budi kuwa na blog ya kukutangazia bidhaa zako dunia nzima 24/7. Hapo utakuwa umevuka mbali sana. Wale amabo muko tayari msisite kuwasiliana nami kwa ajili ya hii shuhulu ya blogging


11. PROOF READING (KUHAKIKI MAANDISHI):
Wale wataalamu wa ngwini hata hizi page zangu 2 nilikuwa nahitaji mtu wa kuzikosoa ili zisomeke vizuri halafu nimlipe. Sasa ukitafuta mtandaoni hupati hata mmoja MKO WAPI? Funguka jitangaze buree huko mitandaoni matangazo madogo zoom ni buree. Mtaji hapa ni elfu20 tu ya kununua dictionary ya TUKI na ile ya oxford pocket size.



12. PROJECT WRITE UP, BUSINESS PLANNING AND RESEARCH
Uandishi wa miradi ya kibiashara, ya kijamii (projects) na utengenezaji wa bajeti, ma inginia, wahasibu, sosiolojia na walimu hii inawahusu sana. Anza na miradi idogo midogo kama ya biashara yako mwenyewe angalia mtandaoni wanaandaje miradi na je unaweza kutetea mradi wako ukapewa hela? Tafuta maresearchers mbalimbali jiunge nao hata kwa bure ili upate uzoefu mwisho utazipiga mwenyewe.



13. ELECTRONICS TECHNICIAN: Wanafunzi wa IT narudi tena kwenu, ufundi wa simu, za wanafunzi wenu, TV na music system nani anatengeza? Kwa nini msitengeneze wenyewe?



14. PRODUCT DESIGN – BUNI BIDHAA: Hapa mi ndio napenda mfano buni sabuni ya kuogea inayozuia mbu wasikung’ate, kifaa kinachogundua mwongo mahakamani. Unda bidhaa, iamagine, imagine, ota, ota, ota. Unda bidhaa uza kwa wenye pesa ili wazitengeneze sio lazima wewe utengeneze



15. TUTION
Hapa sina la kuongeza, lakini pia jaribu MOBILE TUTIONING kupitia whatsapp. Malipo yatafanyika kwa Mobile Money. Ambaye hajatuma pesa humtumii masomo.
Nakushukuru sana mpenzi msomaji wa kipande hiki nina uhakika katika haya machache kuna lako moja umelipata, ukiwa hujapata rudia kusoma siku nyingine, rudia tena na tena. Yapo mengine mengi ila kwako mwanafunzi hayo naona yanatosha ukizingatia upatikanaji wa mtaji, muda,faida, cashflow na ukuaji wa mradi.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom