Biashara 5 bora za mtaji mdogo za kufanya ata ukiwa nyumbani

Aug 24, 2021
27
16
Kuanza biashara kunahitaji maandalizi. Nikimaanisha unahitaji kuwa na maarifa flani tofauti kulinganisha na wale uliowakuta ili ata nao pia wajifunze kutoka kwako. Ikiwezekana na wewe uendelee kujifunza kutoka kwao. Kwenye kipengele hiki tutaenda kuangalia namna ya kufungua biashara ukiwa nyumbani.

Na jinsi ya kutumia kipato kidogo unachokipata.Ili kufungua biashara nyingine ndogo ndogo ambazo zitaendelea kukuongezea kipato.

Tukianza na maarifa ya kufungua biashara ukiwa nyumbani. Ni vema ukatambua kuwa na vitendea kazi vichache ili uweze kufungua biashara ukiwa nyumbani. Vitendea kazi hivyo ni kama jiko la kupikia. likiwa la kuni sawa au la mkaa. Pia yawezekana ukahitaji mafuta ya kupikia na mihogo au viazi. Maana biashara nnayo taka kuiongelea ya kwanza hapa ni biashara tunayoona kila siku tukipita njiani ambayo ni biashara ya kukaanga mihogo.

Biashara hii ya kukaanga mihogo unaweza ukafanya ukiwa mahali popote iwe ni nyumbani kwako au mahali pengine ambapo unataka. Na maamuzi ya kuchagua eneo yanatokana na wingi wa watu waliopo karibu na wewe.

Ukijaribu kuangalia biashara hii kwa ufupi.Utajikuta unaweza ukaifanya ukiwa nyumbani na pia ni biashara ya mtaji mdogo.
"Jua biashara nyingine nyingi zaidi hapa"

Biashara nyingine ambayo unaweza ukaifanya ukiwa nyumbani ni biashara ya ususi. Kusuka ni biashara mojawapo inayoongeza kipato kwa wanawake wengi. Na ntahakikisha kwenye vipengele vijavyo nita orodhesha biashara za kufanya ukiwa nyumbani kwa wanawake na wanaume. Ili kila mtu awe na uelewa sahihi wa biashara inayomfaa.

Kwanza tukianza kuelezea kwa ufupi kuhusu biashara mbali mbali za kufanya. Ni muhimu tukaelewa kuwa biashara hizi zinaendana na ujuzi.

Ujuzi ndio swala la kwanza kabisa litakalo kupa uhuru Zaidi wa kufanya biashara yeyote. Na biashara ambayo utaifanya haita itaji uwe na kipato kikubwa. Wala eneo maalumu la kuifanyia.

Kwa wale wanaofahamu vijana ambao wanatengeneza baiskeli au pikipiki. Wale mtaji wao huwa mdogo sana kwa kuanzia. Na kazi zao huwa wanaweza wakazifanya mahali popote. Hii yote ni kutokana na ujuzi walionao.

Ndio maana narudi tena kwenye msimamo wa watu kuongeza kwanza ujuzi kabla ya kuanza kutafuta biashara rahisi Zaidi ya kufanya.

Lakini swali ni kwamba ujuzi huu utaupata wapi?. Na ni watu gani huwa wanatoa mafunzo ya ujasiriamali? Na mafunzo hayo huwa ni bure au unalipia?

Kikubwa cha kutambua hapa ni kama unatoa mafunzo ya ujasiriamali na ungependa kuwapa watanzania wenzetu ujuzi. Acha namba zako hapo chini ili watu wakutafute.

Kumbuka AA Tanch Trading Company tupo Arusha makao mapya. Na tunatoa ushauri wa kibiashara. Huduma zingine unaweza ukaagiza bidhaa kutoka china. Kupitia kampuni yetu. Mapema na kwa haraka. Kwa bei ya viwandani. Na ukapata faida Zaidi ya vile ulivokuwa unategemea.

Agiza kutoka china na AA Tanch Trading Company Iliopo Arusha Makao Mapya . Tupigie simu au tutembelee kwa kupitia tovuti aatanchtrading com.

Pia kama wewe ni mfanya biashara na unataka kuweka picha ya bidhaa zako mtandaoni.Kupitia mtandao wetu wa sokokuuonline co tz.

Ni vizuri ukawasiliana nasi kwa namba izo izo ntakazoweka hapa.

255 756 591 943/ 0655 591 943
Jiunge group letu la telegram kufaham zaidi kuhusu kampuni yetu(Telegram Group)
 
Back
Top Bottom