Bia za Ofa nakunywa tangu jana.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bia za Ofa nakunywa tangu jana..

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by BonBerry112, Oct 22, 2012.

 1. BonBerry112

  BonBerry112 Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simu inaita saa mbili asubuhi
  mwanawani, jamaa hajarudi home
  toka jana, waifu on ze line.
  Ringitoni, sumu ya teja ukonga keko
  segerea, ah sumu ya teja sumu ya
  teja. Jamaa anaamua kupokea.
  Wife: Uko wapi we mwanaume,
  muhuni mkubwa usiku mzima
  humkumbuki mkeo kazi kuzurura,
  mi nimechoka mpuuzi wewe na
  unipe talaka yangu! Tena leo.
  Jamaa: Unakumbuka lile duka ya
  yule sonara? Pale ulipoona ule
  mkufu wa dhahabu ukaupenda sana?
  Wife akaanza kuwa pole: Ndiyo
  mume wangu mpenzi,
  napakumbuka. Maneno siku hizi
  nayo yananitoka, kumbe darling uko
  nje unatafuta maisha ili mkeo
  nipendeze. Nisamehe bure kwa hayo
  maneno. Kwa hiyo, ndo uko hapo, si
  umechoka mpenzi, vipi umeamua
  kuununua kabisa? Wewe nawe
  unanipenda kweli. Asante mume
  wangu. Wahi unywe chai kabla
  hujaenda ofisini basi. Mwaaaaaaah!
  Jamaa: Hapana, sio hivyo, nilitaka
  nikwambie niko kwenye ile bar
  karibu na hili duka, kuna bia za ofa
  nakunywa toka jana!!
   
 2. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Huyu chapombe ni noma, sipati picha mke atamjibu nini
   
 3. RAIS WA WALALAHOI

  RAIS WA WALALAHOI Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ina maana wanawake wanadanganywa na dhahabu ya mwadui?
   
Loading...