Bia bei juu

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Katika hali isiyo ya kawaida makampuni ya bia nchini yamejipandishia bei za bia kienyeji bila kuwataarifu wateja wao.Hali hii imetokea kuanzia jumapili tr 08 feb 2009.
Tumezoea kunywa kwa mfano Kilimanjaro na Safari kwa sh.1200/= zimepanda mpaka 1300 na 1400 huku Castle na Serengeti tulikuwa tunakunywa kwa sh.1300/= kwa sasa imepanda mpaka 1400 na 1500.
Napenda kulalamika kwa makampuni husika kwa kupandisha bei gafla bila kuwataarifu wateja wao husika na hii imeleta kero sana kwa sisi wanywaji mpaka tukajua tunaibiwa.
Kama inawezekana tunaomba serikali iunde chombo cha kusimamia bei za bidhaa kama ilivyo kwa nyanja zingine kama kwenye mafuta na usafiri kuna EWURA.

Ukiangalia kwa undani zaidi makampuni ya pombe ndo walipaji wazuri wa kodi nchini ukilinganisha na nyanja zingine kama madini,kilimo n.k
 
Last edited:
Katika hali isiyo ya kawaida makampuni ya bia nchini yamejipandishia bei za bia kienyeji bila kuwataarifu wateja wao.Hali hii imetokea kuanzia jumapili tr 08 feb 2008.

Ni typo error au you mean it?
 
nchi haina mwenyewe kila mtu anaserikali yake, wa mafuta wakiamua poa wa bia poa, wa daladala poa ilimradi ni fujo tu
 
Mtu akiona bia ghali...si afadhali unywe tu hata soda?

Soda ni 350-400 tu!

Wacha wapandishe tu, sisi tutahamia huku.......

131425.jpg
 
katika hali isiyo ya kawaida makampuni ya bia nchini yamejipandishia bei za bia kienyeji bila kuwataarifu wateja wao.hali hii imetokea kuanzia jumapili tr 08 feb 2008.
Tumezoea kunywa kwa mfano kilimanjaro na safari kwa sh.1200/= zimepanda mpaka 1300 na 1400 huku castle na serengeti tulikuwa tunakunywa kwa sh.1300/= kwa sasa imepanda mpaka 1400 na 1500.
Napenda kulalamika kwa makampuni husika kwa kupandisha bei gafla bila kuwataarifu wateja wao husika na hii imeleta kero sana kwa sisi wanywaji mpaka tukajua tunaibiwa.
Kama inawezekana tunaomba serikali iunde chombo cha kusimamia bei za bidhaa kama ilivyo kwa nyanja zingine kama kwenye mafuta na usafiri kuna ewura.

Ukiangalia kwa undani zaidi makampuni ya pombe ndo walipaji wazuri wa kodi nchini ukilinganisha na nyanja zingine kama madini,kilimo n.k

ni sawa kabisa.
 
Katika hali isiyo ya kawaida makampuni ya bia nchini yamejipandishia bei za bia kienyeji bila kuwataarifu wateja wao.Hali hii imetokea kuanzia jumapili tr 08 feb 2008.
Tumezoea kunywa kwa mfano Kilimanjaro na Safari kwa sh.1200/= zimepanda mpaka 1300 na 1400 huku Castle na Serengeti tulikuwa tunakunywa kwa sh.1300/= kwa sasa imepanda mpaka 1400 na 1500.
Napenda kulalamika kwa makampuni husika kwa kupandisha bei gafla bila kuwataarifu wateja wao husika na hii imeleta kero sana kwa sisi wanywaji mpaka tukajua tunaibiwa.
Kama inawezekana tunaomba serikali iunde chombo cha kusimamia bei za bidhaa kama ilivyo kwa nyanja zingine kama kwenye mafuta na usafiri kuna EWURA.
Ukiangalia kwa undani zaidi makampuni ya pombe ndo walipaji wazuri wa kodi nchini ukilinganisha na nyanja zingine kama madini,kilimo n.k

Wacha wapandishe tulipe kodi zaidi, yaani mnataka EWURA iwatetee mpaka kwenye ULEVI? is it a necessity commodity? inawagusa wananchi wengi na wa kawaida? kazi kweli kweli, hata sigara zikiongezwa bei wengine mtaandamana

Mtu akiona bia ghali...si afadhali unywe tu hata soda?

Soda ni 350-400 tu!

Soda mmhhhh KISUKARI JE????
 
Mkuu wewe unalalamika ,uku kwetu naona....imekuwa kama kawaida...naona sasa 1300 tusker,Castle 1500/= watauza..2000 zote.....
 
Mkuu wewe unalalamika ,uku kwetu naona....imekuwa kama kawaida...naona sasa 1300 tusker,Castle 1500/= watauza..2000 zote.....
Hii mitaa yangu Bia imepanda kwa muda wa mwezi sasa, kwa ongezeko la kati senti 10 hadi senti 30..Happy hour bado zinasaidia
 
Happy hour bado zinasaidia
umenikumbusha mbaaaali saaana......tehe tehe kuna sehemu nilienda basi happy hour unajitwalia kama beer 20 hivi unaziweka mezani pembeni na toto la kihabeshi likipitisha mikono uwanda wa lake victoria akitafuta sangara bila kusahau cigar kuubwa.....si unajua happy hour ilikuwa inaanza saa 9 jioni basi mie saa 8 nipo pale......saa 2 hivi usiku mie mfalme ni kuzibua vizibo.....
 
Mzee uko zinakuwa kama za promosheni...unanunua za kutosha kabasa kumaliza siku????....mambo ya lake victoria basi mnaweza kesha....
 
Mzee uko zinakuwa kama za promosheni...unanunua za kutosha kabasa kumaliza siku????....mambo ya lake victoria basi mnaweza kesha....
enzi hizo ilikuwa kama beer ni shin 100 basi happy hour nakuwa 40......ia muda wakew kuanzia saa 8 mpaka saa 2 usiku...kuanzia hapo bei inakuwa ya kawaida......si unanua mabitozi kama NN happy hour hawaji humo ndani mnakuwa woote wa mikoroshino lkn ikifika saa 2 night unakuwa mfalme....maana una jeuri ya kutuliza toto lolote......happy hour does bwana.....
 
Mkuu ni type error kama ulivyo kosea na wewe hapo juu.

Mwenzangu ulizidisha --- 2008 vs 2009?

Anyway tuache hili.....!

Unajua makampuni ya bia na sigara they know well in advance kwamba kunako July serikali itawapandishia kodi tu! So what they normally do, huwaandaa wateja wao well in advance waizoee bei mpya...kama utakuwa umefuatilia budget za miaka kama kumi iliyopita hakuna mwaka uliopita bila ya kuongeza kodi kwenye vilevi...na utaona w.e.f 1 July, ambapo viwango vipya vya kodi huanza kutumika, bei za vilevi huwa hazibadiliki....wanakuwa wamesha adjust miezi mitatu au nne iliyopita! So tegemea kabisa kodi kuongezeka kny vilevi ifikapo July 09 but makampuni husika hayataongeza bei ya vilevi hivyo!

Ok sina ugomvi sana serikali kutoza kodi kubwa kwenye vilevi, ugomvi wangu na serikali ni upofu wa kuexplore new tax venues......wao wamekalili tu, wakitaka kuongeza mapato....wanaangalia tu vinywaji, sigara, PAYE (waajiriwa), VAT, Import duty, excise duty basi! Hawafikiri kuongeza wigo wa kodi (tax base) maeneo mengine yasiyo rasmi kama kwenye real estates, biashara ndogo ndogo (small & SMEs) like wale wafanyabiashara wa k/koo, watu wenye mabaa like yale ya Sinza etc....hawawafanya biashara hukadiriwa kodi ndogo kweli mpaka unashangaa!

Kwa mfano mfanyabiashara wa nguo kariakoo say mtaa wa Kongo....pango la frem ya duka analipa kati ya Tshs 200,000 hadi Tshs 1,000,000 kwa mwezi. ok tuchukulie analipa Tshs 500,000*12=6,000,000...alitakiwa awasilishe Tra Tshs 600,000 kama kodi ya zuio,lakini wapi hii kodi hakuna anaye lipa pale k/koo, hili la kwanza.

Pili, chukulia huyu mfanyabiashara ana mtaji wa say Tshs 100mil.....pale k/koo kuizungusha hii hela baada ya mwaka mmoja lazima utakuwa na zaidi ya Tshs 200,000,000 (I know some guys who have managed to do this).....sasa hawa TRA wao mtu akisha jisajiri, they just do a ''remote assessment'' ya tax watamwambia we mbwana mwaka huu utalipa Tshs 500,000, kama kodi ya biashara yake! Sasa imagine, huyu mtu ametengeneza faida ya zaidi ya Tshs 50mil analipa Tshs 500,000 tu kwa mwaka, badala ya Tshs 50,000,000*30%=15,000,000! wakati, muajiriwa na kama mshahara kake say ka gross ya Tshs 1,000,000, analipa Ths 174,000 kila mwezi, so kwa mwaka analipa Tsh 2,088,000! This is not fair at all.

So haya matatizo yote ya kupanda kwa bei za bia etc husababishwa na kodi, na kodi hupanda kila mwaka kwenye vilevi b'se serikali lacks creativity ya kuongeza wigo wa kodi, so ends upa kuwaumiza watu wachache!

So wakuu, suala la kuongezeka bei za kilaji is inevitable kama serikali itaendelea kuwa pofu wa kutoona maeneo mengine ya kutoza kodi!
 
Kwani ni lazima na muhimu sana kunywa bia?

Ndio maana nashangaa duniani kote, vitu muhimu vinapewa umuhimu kidogo!! Lita moja ya maji inauzwa karibia 1000 wakati ya maziwa inauzwa 500-800!! Unga wa sembe umepanda kutoka shs 300 mwaka 2005 had 1000 mwaka 2009 hatupigi kelele. Bia imepanda kwa shs 100 tunataka kutoana roho!!! Kwa mwendo huo, itabidi tuwe an EWURA ya kushughulikia hata safari na matanuzi ya wakulu!
 
Lita moja ya maji inauzwa karibia 1000 wakati ya maziwa inauzwa 500-800!!

Mkuu sijakupata kwenye bei ya maji.Ulitaka kusema bei ya bia au bei ya maji?
 
Mkuu sijakupata kwenye bei ya maji.Ulitaka kusema bei ya bia au bei ya maji?

Mkuu ni maji ya kunywa ya chupa! Najaribu kulinganisha bei ya maji na maziwa! Kipi kilitakiwa kuwa na bei kubwa?? Au kwa sababu maji yanatoka kiwandani?:confused:
 
Back
Top Bottom