Bia aziona mbaya baada ya kubwagiwa mtoto bar na mzazi mwenzie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bia aziona mbaya baada ya kubwagiwa mtoto bar na mzazi mwenzie

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 26, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,483
  Likes Received: 5,718
  Trophy Points: 280
  MWANAUME mmoja mkazi wa Manzese, jijini Dar es Salaam alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya mzazi mwenzie kumsusia mtoto wakati akiwa katika sehemu za starehe akijivinjari.
  Mwanaume huyo juzi, majira ya saa 2:47 akiwa katika baa iliyotambulika kwa jina la Moshi Bar iliyopo maeneo ya Manzese Tiptop alikutwa na dhahama hiyo bila kutarajia.


  Wakati akiendelea kunywa kinywaji chake aina ya Kilimanjaro, ghafla alitokea dada mmoja jina halikuweza kupatikana akiwa na mtoto anayekadiriwa kuwa ni wa mwaka mmoja na zaidi alimbwagia mwanaume mtoto huyo huku akitoa maneno kumtupia mwanaume huyo.


  Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi mahali hapo, mwanamke huyo alimuacha hapo mtoto huyo na yeye aliondoka na kumtupia maneno baba huyo ya kashfa hali iliyofannya nifahamishe ibaini kuwa mwanamke huyo alitelekezwa na mwanaume huyo.

  MWanaume huyo alikuwa katika wakati mgumu mahali hapo hali iliyofanya aone aibu na motto huyo huyo aliyekuwa wa kume kuanza kulia na kusababisha bia azione za uchungu baada ya motto huyo kuanza kulia.

  MWanaume huyo alijaribu kumchukulia chakula aina ya chips mtoto huyo kwa kudhani labda angeweza kunyamaza lakini utulivu wa mtoto huyo haukupatikana na kuendelea kulia mahali hapo.

  NIFAHAMISHE ilishuhudia baba huyo akimbeba mtoto huyo na kuondoka nae mahali hapo na haikujulikana mara moja alikuwa akielea wapi kwa wakati huo.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,839
  Trophy Points: 280
  good! kwa nn hatuwathamini wake zetu?
   
Loading...