Bi kizee asafari kilometa 50 kumpinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bi kizee asafari kilometa 50 kumpinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, May 5, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  WAZEE zaidi ya 1,000 waliokuwa wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete juzi kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee walikuwa wakimshangilia mara kwa mara, lakini si Bi Asha Omary, 70, aliyekuwa kijijini kwake wilayani Kisarawe.
  Kikongwe huyo alisikiliza hotuba hiyo, iliyobatilisha mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, kwenye redio akiwa Kijiji cha Bwana, Kata ya Kibuta na hasira alizopata kutokana na kauli za rais, zilimfanya aamue kusafiri takriban kilomita 35 kuanzia saa 1:00 asubuhi kuja jijini Dar es salaam kueleza jinsi alivyokerwa.“Kama kiongozi wa taifa, rais angetumia maneno ya busara na hekima yasiyo na ukali ndani yake katika kutatua tatizo kwa sababu wafanyakazi wanadai haki yao na wanayo haki ya kufanya hivyo,” alisema Asha alipofika ofisi za gazeti la Mwananchi majira ya saa 4:30 jana.
  “Rais amejisahau na anatumia vibaya mamlaka aliyopewa na Watanzania kuwakandamiza wafanyakazi, amesahau kuwa nafasi hiyo imetokana na wananchi wote wakiwapo hao wafanyakazi.”
  Bi Asha alikuwa akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete kuhusu mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kuanza leo, hotuba ambayo iliwashambulia viongozi wa Tucta kuwa ni "waongo, wanafiki, wazandiki na wafitini" kwa madai kuwa wamekuwa hawawaelezi wanachama wao kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya pande hizo.

  Katika hotuba hiyo ya dakika 95, ambayo pia ilirushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), TBC Taifa na redio Uhuru, Rais Kikwete, ambaye alikuwa akishangiliwa mara kwa mara na wazee hao ambao wengi walivalia mavazi ya rangi za njano na kijani, alitangaza mgomo huo kuwa ni batili kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
  Bi Asha, ambaye ni mkulima wa jembe la mkono, alisema rais hakutumia hekima na busara katika kutatua kero za wafanyakazi bali alitumia cheo chake kuwatisha wafanyakazi katika kutetea haki zao.
  Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi kwa kuwa ndio wanaotoa huduma zote muhimu kwa wananchi wote hasa masikini ambao ni wakulima.
  Alisema rais na familia yake wanatibiwa nje ya nchi ndiyo mana haoni umuhimu wa kutatua kero za wafanyakazi badala yake anatoa majibu ya dharau kuwa kama hawataki kufanya kazi waache.
  “Au kwa kuwa rais na viongozi wenzake wanatibiwa Ulaya na Marekani ndio maana anatoa vitisho au anataka uwe kama mgomo wa mwaka juzi kwenye Hospitali (ya Taifa) ya Muhimbili ambako watu walipoteza maisha,” alihoji Asha.
  “Kama wafanyakazi nao wakisema liwalo na liwe wakachukua hasira kama alizochukuwa rais, itakuwaje; madaktari, manesi na watumishi wengine wakigoma, je haitasababisha maafa kwa Watanzania?”
  Asha ambaye alitumia muda wa dakika 70 kueleza masikitiko yake, alisema wakati rais anawatisha wafanyakazi ili wasigome, anapaswa kufunga safari kwenda maeneo ya vjijini kujionea hiyo misaada ya matrekta na ‘Power Tiller’ kama imewafikia wananchi au inatumiwa na viongozi wa vijiji kwa maslahi yao.
  Rais katika hotuba yake alisema serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh315,000 kwa watumishi wa umma kwa sababu wananchi wengine watakosa huduma za afya, pembejeo za kilimo na hata vifaa vya elimu na walimu.
  “Sisi wakulima hatuwezi kugoma lakini kwa muda mrefu hata hizo pembejeo na matrekta anayoyazungumzia hatuyaoni, mbona hachukui hatua na kutoa hotuba kali kwa maafisa wake ili na sisi tupate hizo pembejeo,” alihoji Asha ambaye ni mtoto pekee katika familia yao.
  “Sisi vijijini hatuna huduma bora za afya, maji, barabara, shule na rais anasikia kila siku Watanzania wakilalamikia hali hiyo. Je kwa nini rais asitumie cheo chake kuchukua hatua kutatua matatizo ya wananchi kama alivyoamua kwa wafanyakazi,” alisema Asha kwa hasira.
  Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Asha alisema enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, bei za vyakula zilikuwa zinafanana katika maduka yote, lakini sasa kila mfanyabiashara ana bei zake.
  “Je serikali inashindwa kusimamia tatizo la kupanda kwa gharama za maisha au rais anawaogopa wafanyabiashara... na kama anawaogopa itakuwaje kwa Watanzania,” alihoji Asha.“Namuomba rais siku moja angalau afanye ziara ya kupita katika maduka na kuhoji au kuangalia bei za vyakula halafu alinganishe na vipato vyetu sisi Watanzania kama tunamudu.”
  Katika harakati za kutatua tatizo la ugumu wa maisha yake, bibi huyo alisema alishaenda ikulu mara mbili na kugonga hodi ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), inayoongozwa na mke wa rais, Mama Salma Kikwete ili kuomba mkopo kwa ajili ya kufanya biashara.Asha alisimulia kuwa alifanikiwa kuonana na mmoja wa watendaji wa Wama na kumuelea shida yake, lakini alijibiwa kwamba fedha za Wama zina mlolongo mrefu na kwamba yeye hawezi kuzipata.
  “Nilipohoji ni mlolongo gani, hakunifafanulia ila aliishia kuniambia tu kwamba ni mkubwa na huwezi kupata fedha hizi... rudi nyumbani. Nikamuuliza je hizo fedha mnazotangaza kwamba mnawakopesha wanawake ni wanawake wote au mna wanawake maalum ambao wanastahiki, sikupata jibu,” alisema Asha huku akionekana kuwa na hasira.
  Baada ya hapo nilijua kuwa fedha za Wama ni za watu maalum na sio kila mwanamke.
  Hata hivyo, Asha alimuomba Mwenyezi Mungu ampe amuweke katika afya njema Rais Kikwete ili aweze kutumia hekima na busara katika uongozi wake; amuepushe na kutumia ubabe na cheo chake katika kuwaongoza Watanzania.
  “Uongozi ni dhamana aliyopewa na Mwenyezi Mungu na Mwenyezi: Mungu pia ndiye anayeweza kumnyang’anya dhamana hiyo wala si Watanzania kama anavyodhani, hivyo ajitahidi kuwa mwadilifu, mwenye hekima, busara na imani katika uongozi wake,” alisema Asha.Pia aliwaombea wafanyakazi ambao wanataka kuingia katika mgomo kutofanya hivyo kwa kuwa wakifanya hivyo watadhulumu haki za Watanzania.
  “Nawaombea kwa Mungu viongozi wa Tucta wawashawishi wafanyakazi wasigome ili wasibebe dhima ya kudhulumu haki za Watanzania watakaokosa huduma mbalimbali kwa muda wote watakaogoma, Aaaammmiiin,” alisema Asha ambaye ni mkulima wa kilimo cha jembe la mkono.


  Chanzo Mwananchi.
   
 2. K

  Konaball JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Ataambiwa ana agenda ya siri au ametumwa!!!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  WRITTINGS ON THE WALL.
  KIKWETE SIJUI ANAJIFUNZA NINI NA HAYA MAANDISHI UKUTANI YANAYOSEMA
  MENE MENE TEKEL UPHARSIN(PARSIN)

  [​IMG]


  Dan 5:25 And this is the inscription that was written:

  MENE, MENE, TEKEL, UPHARSIN.

  :26 This is the interpretation of each word.
  MENE: God has numbered your kingdom, and finished
  it;
  :27 TEKEL: You have been weighed in the balances, and
  found wanting;
  :28 PERES: Your kingdom has been divided, and given to
  the Medes and Persians.

  .
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huyo ni mzee wa kweli na kweli anaijua hii nchi ilipotoka, ilipo na inapokwenda, hawa wa dar es salaam wengi wao wakiwa ni madalali ni wana CCM na ndio wako kwenye list ya Tshirt, Kofia na Pilau katika kipindi cha uchaguzi
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ni aibu kwa wale wazee wengine!
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo mzee ataambiwa sio mzawa wa Tanzania.
  Naomba nimlipie nauli ya kurudi Kisarawe jamani.
   
 7. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mzalendo wa kweli.

  Rais kuongea uongo ni jambo la kufedhehesha mno. It is beyond any right minded person scope of comprehension. A president LYING infornt of poorest dying oldest people in Dar. Shame .
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hao ndio wale wazee wachache wenye utambuzi..kama angekuwe kwenye ule ukumbi nadhani angenyanyua kidole na kusema...Mheshimiwa ...unacheza faulo..
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hawa ndo wazee wanaotakiwa Tanzania? Ana vision na uelewa mkubwa wa viongozi wa Tanzania. Hii ni aibu kwa wazee vihiyo wa dar es salaam.
   
 10. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tungepata wazee kama hawa watano tu kwenye ule mkutano.......nadhani tungeandika historia nyingine tofauti kabisa na hii tunayoisikia.
   
 11. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyo bi kizee alikuwa anatafuta bwana wa kustarehe naye kwakuwa kule kisarawe wazee makamo yake wameshamchoka kutokana na ukahaba wake.Miaka 70 tayari ameshaolewa na kuachwa mara 9,aibu!
   
 12. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,129
  Likes Received: 1,252
  Trophy Points: 280
  Mara zote mtu hujitambulisha alivyo kwa jinsi anavyoongea, watu wenye akili sasa wamejua tuna rais wa namna gani na waliomchagua pia wajiangalie maana nawakilisha taswira yao. Bibi hajaonyesha tu uzalendo bali ameutimilsha na kuufanya.
   
 13. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,129
  Likes Received: 1,252
  Trophy Points: 280

  mhh kama tukianza ku personalize issues itakuwaje? unataka tukuambie wewe umepitia wapenzi wangapi mpaka hapo ulipo na unafanya jitihada gani kuwatafuta wengine?
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Usipoteze muda wako kujibizana na huyo hujajua ni nani?
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Sometimes tuwe makini jamani - tunajadili nini namna hii? shame.
   
 16. M

  Msindima JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Mmhh mwenzetu umeyajuliya wapi hayo? naona unataka kuvuruga post kwa makusudi.
   
 17. M

  Msindima JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda sana hii.
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Inaelekea na wewe ni mmojawapo wa hao mabwana waliowahi kustarehe na huyu bibi kwa mujibu wa maelekezo yakona ndio maana unatupa habari za kina jinsi hii.Kwa hiyo kama nyie wote ''mlistareheshana'' sioni sababu ya kuiweka hapa.Huyu bibi ni shujaa mara mia ya wewe na usitake kutuchafulia hewa.Mungu akusamehe bure kwa kuwa hujui ulitendalo.Amen.
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kunawatanzania wenye akili mbovu kiasi hiki duuu! haoni hata mwelekeo wa nchi analeta utani wake wakijinga au yeye ndo mwenyetabia hizooooo!!!
  HULEEEEEE BIBI AMSHA VIJANA WALIOLALA!
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  haya yanahusikaje hapa?.....
   
Loading...