Bi. Kiroboto; Bunge letu 'NI LA WAPGA MAKOFI'... Kwa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bi. Kiroboto; Bunge letu 'NI LA WAPGA MAKOFI'... Kwa nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pasco_jr_ngumi, Apr 19, 2011.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hoja……
  ………waheshimiwa wabunge
  mnaunga mkono
  hoja?..Ndiyooooooooo!..........
  Hizi ndio kauli kuu mbili kwa wabunge
  wetu ya kwanza ni ya baadhi ya
  wabunge ambao wakisimama hawaachi
  kusema kauli hiyo ya kuunga mkono
  hoja huku ya pili ikitumika mara nyingi
  na spika kwenye kufikia maamuzi
  mbalimbali ambapo wabunge wetu mara
  nyingi ni watu wa ndiyo.
  Inasikitisha sana! Wabunge wetu
  wamekuwa wavivu wa kujenga hoja
  wamepwaya sana kiasi cha kwamba
  wamebaki kuwa watu wa ndiyo tu hata
  kwa mambo ambayo hayana maslahi
  kwa taifa au hao wananchi wa
  majimboni mwao, inasikitisha kuona
  kuwa kila mwaka bajeti ya nchi
  imekuwa ya uchungu kama sio jasho na
  damu kwa mtanzania masikini, bajeti
  hizi zimekuwa zinashindwa kumkomboa
  mtanzania kutoka kwenye lindi la
  umasikini lakini cha ajabu ni kuwa bajeti
  hizi zilipitishwa bungeni na wabunge
  wetu na iwapo wewe msomaji wangu
  unadhani huu ni mzaha au naongopa
  basi subiri hilo bunge la bajeti la mwezi
  juni utaona hali halisi jinsi wabunge
  wetu walivyopwaya kwenye kujenga
  hoja watapitisha bajeti itakayozidi
  kutukamua.
  Huwa nashindwa kuelewa hivi kuna
  wabunge wanaenda bungeni kusema
  ndiyo tena kwa makelele makubwa?
  utadhani hizo kelee zao za ndiyo
  zinaboresha shule za kata majimboni
  kwao? Au zinawasaidia mamia ya
  masikini wa jimboni kwao kuweza
  kujikimu kimaisha? Wabunge hawa
  ndiyo huonekana majimboni kila baada
  ya miaka mitano kisha hawachaguliwi
  bali wanatumia fedha kununua uongozi
  na kwa bahati mbaya ndiyo hivyo
  TAKUKURU haina la kufanya na hata
  ikithubutu mara kibao watuhumiwa
  wanashinda kesi na kuachiwa huru kisa
  TAKUKURU wanakosea kufungua
  mashtaka, ajabu sana!
  Na hata baadhi ya wabunge wa vyama
  Fulani wakijitutumua kusema umezuka
  mchezo wa kitoto wa kuwazomea ,
  inasikitisha kuona kuwa CCM ndiyo
  walikuwa vinara wa kuwazomea
  wabunge wa CHADEMA na hata kuna
  wakati wabunge wa CHADEMA
  wamemlaumu waziwazi spika Anne
  Makinda kuwa anakibeba chama chake
  cha CCM na hata wabunge wa upinzani
  wakijitutumua kupinga maamuzi
  legelege kwa nguvu ya hoja kwa
  bahati mbaya wenzao wa CCM wapo
  wengi hivyo wanatumia hoja ya nguvu
  kuzima hoja za wapinzani.
  Hivi wabunge wetu wanajua kweli kwa
  nini wapo bungeni? Wanafahamu tabu
  tulizonazo? Hivi hawa wabunge
  wanaounga mkono hoja wanafahamu
  kuwa kuna ndugu zetu wako mahabusu
  kwa mwaka wa tatu sasa bila
  kusomewa kesi? Hivi wanafahamu kuwa
  kuna ndugu zetu wanaporwa ardhi
  kwa hoja za uwekezaji? Wanafahamu
  kuwa madini yetu yanazidi kuisha na
  kubakisha mashimo ya kuzalisha mbu
  wa maralia huku wenyewe hatufaidiki
  kitu? Hivi hawa wabunge wanafahamu
  kuwa kuna ndugu wamefeli kwenye
  shule za kata kwa sababu tu serikali
  inafanya mzaha na elimu?
  Hivi hawa watu wanafahamu kuwa ajali
  za bararani zinazidi kutumaliza kwa
  uzembe wa vyombo husika? Hivi hawa
  watu wanafahamu jinsi gani vijana
  wetu walipigwa pale Mlimani na Dodoma
  kwa sababu ya kudai nyongeza ya
  fedha za kujikimu kitu cha haki kabisa?
  Inauma sana waache mzaha kabisa sisi
  masikini wa nchi hii tunateseka tu bila
  sababu za msingi haiwezekani
  tukaendelea kuwa masikini huku
  wanaotusababishia umasikini huo ni
  wao tunawajua , HAKIKA HAWA
  HAWAVUMILIKI MAANDISHI YASHAANDIKWA
  UKUTANI UNABII NI LAZIMA UTIMIE TU.
  Hivi kwani hawa wabunge wasioweza
  hata kuchambua mambo kwa hoja kwa
  nini wasijiuzulu tu? Wanafanya nini
  bungeni? Au kuitikia ndiyo? Wanakera
  sana yaani wanakubali kila kitu kwa
  nini lakini? Mbona wenzetu kule
  Uingereza wanajadili mambo kwa hoja?
  Au hapo Kenya mbona bunge lao si
  mchezo kwa jinsi wanavyojadili mambo
  kwa hoja, sisi tuna nini? tumerogwa ?
  mbona sisi ni watu wa ndiyo huku
  tukiendelea kudidimia kwenye umasikini
  wa kutisha? Naam! Tatizo ni wabunge
  wetu kupenda kupiga makofi hata
  kwenye mambo yasiyotusaidia
  wamekuwa watu wa ndiyo sana wana
  uwezo mdogo sana wa kuje
   
 2. regam

  regam JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tusilaumu tuu wabunge, kwani wanaingiaje bungeni? Si ni sisi tunaowachagua? Pamoja na kwamba wanaiba kura, kwani wanaokwenda kupiga kura si ni sisi? Sasa tunataka takukuru wafanye nini hapo?
  Jinsi wabunge wanavyobehave bungeni ni kwa sababu ya ujinga wetu. Kuna baadhi ya majimbo yetu wabunge wanaonekana kipindi cha uchaguzi tuu. Wakishachaguliwa hawaonekani kamwe majimboni mwao. Wamejazana dar es salaam. Sasa wakumlaumu ni nani hapo kama sio sisi tunaowachagua? Hata kama wanatununua, takukuru watafanya nini la ajabu? Ujinga ni wetu wajameni. Wataendelea kutotuwakilisha zaidi ya kupiga makofi tuuu na hoja za ndiyo au hapana. Jamani tubadilike!
   
 3. s

  smz JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tuache ushabiki wa kisiasa:

  Nitoe mfano wa Mh. Tundu Lissu: Kiukweli wapiga kura wake walifanya maamuzi sahihi. Hongereni sana wananchi wa Singida jimbo la mh Lissu. Huyu bwana anatumia elimu yake kwa manufaa ya wengi, tofauti na mijitu mingine imo humo kupiga makofi na kuunga mkon hoja asilimia 100.

  Wamo wah wengine wanasubiri saa ya kupiga kura, wakati wa majadiliano hawamo ndani, wako nje wankunywa kahawa na kupiga simu wakidai wanaongea na "wapiga kura wao". Ukifika muda wa kupiga kura kwa lengo la kupitisha musawda fulani, utawona wamejazana ndani.

  Utawasikia "Sisi tuko hapa kuhakikisha muswada unapita" mtu huyo huyo hata hakuchangia mstari mmoja kwenye hoja yenyewe. Anasubiri spika aulize: Wanaokubali waseme ndiyo, utayasikia kwa chorus yakisema NDIYOOOOO ikifuatiwa na makofi yale ya kinafiki.

  Lakini dawa yao ipo na wanajua kuwa 2015 inakuja. Hakianani hamrudi tena mjengoni, mnafikiri hatufuatilii uwakilishi wenu. Hatukuwatuma kwenda kusema NDIYO na kulala bungeni, tumewatuma kuhoji na kutoa michango endelevu. Mnaona miaka 5 ni mingi sana!!?? SUBIRINI.
   
Loading...