Bi Hellen, tunataka taarifa iliyokwenda The Hague si maneno matupu

Tutatulia wenyewe kwani haya mambo ya jeshi la polisi fufanya mauaji raia yameanza leo. ngoja tuzike alafu tusubiri tume ya uchunguzi milele kwa majibu. wanamuaibisha rais wa nchi hii bana wanamgusa hadi chini ya makalio wala hatikisiki.
 
Pamoja na ukweli kuwa Mahakama zetu sasa hivi zimekuwa kichaka cha kusitiri maovu ya Serikalii, bado naamini wanasheria wana mchango mkubwa katika kupinga kitaalamu uonevu na unyama huu wanaofanyiwa wenye nchi.

Tunaona maeneo mengine, wanasheria binafsi na hata kupitia Taasisi zao za kitaaluma, wanaikaba koo Serikali na kuiburuza mahakamani! Hapa kwetu hili haliwezekani?

Ni hivi majuzi tu, nikitoa mifano michache, mwanasheria mmoja kamburuza mahakamani AG wa kenya, akimtaka umma ufahamishwe alichoteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi moja yenye nguvu duniani. Hata tume ya Prof. Saitoti, wanasheria wa familia wamejumuishwa.

Wanasheria wetu, na chama chenu, kunani? Tunajua pengine mikataba ya ovyo Nchi inayoingia ni kutokana na mashinikizo mbalimbali mnayopata, japo Nchi inavuja damu kwa kukosa uzalendo.Hatuwezi kumuachia Mchungaji peke yake!

Ikibidi uanzishwe mfuko na kusaidia wanaoendesha kesi za kupinga maovu.

Huyu mama na wengine, waungwe mkono
 
Huo ni msimamo niliokuwa nasisitiza kwa Vituo vya Sheria nchini. Nina amini kuwa uamuzi huu utasaidia hata kupunguza safari za JK kwenda nchi za nje pale The Hauge itakapotoa Hati ya Kukamatwa kwa Rais JK, Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Vuai Nahodha (wakati huo) na Nchimbi kwa sasa. Ni uamzi sahihi. Na sisi wananchi tuaandae maandamano yasiyo na kikomo KATIKA VIWANJA VYA UHURU NCHI NZIMA

Kama namuona wakati hati ya kukamatwa itakapotolewa na asivyopenda kukaa kwake sijui itakuwaje!
 
kile kkituo wanajua tu kupiga kelele ila kuongea point za kisheria wako nyuma sana. walitakiwa waliongee hili kipindi kile cha mauaji ya arusha, yale kidogo ndo yalikuwa yanaelekea kwenye crimes against humanity, lakini hili la kumuua mtu mmoja mmoja hili ni murder ya kawaida na icc hawawezi kumpokea.

Sina utaalam wa sheria, lakini nami nilifikiria kuwa issue ya mmoja mmoja ni ngumu kupelekwa kwa dada wa Ocampo. Issue kama hizi tungehangaika nazo wenyewe, wanahabari wangeanza na kugomea kuandika habari zote za serikali. Hata sie raia wa kawaida nina imani tuna nafasi kubwa tu, hofu yangu tunatawaliwa na uoga sijui?!
 
huyu anakurupuka tu, hana lolote.
Kuna mengi anaweza kuyafanya kabla ya kufika huko na yamemshinda tayari.
 
kile kkituo wanajua tu kupiga kelele ila kuongea point za kisheria wako nyuma sana. walitakiwa waliongee hili kipindi kile cha mauaji ya arusha, yale kidogo ndo yalikuwa yanaelekea kwenye crimes against humanity, lakini hili la kumuua mtu mmoja mmoja hili ni murder ya kawaida na icc hawawezi kumpokea.

Enyi wanasheria ukichanganya je na ile brutality walifanyiwa wananchi wale? yaani mbali na aliyekufa lakini kuna watu walifanyiwa vitendo vibaya na polisi hili je?
Bahati mbaya ndio ninapanga kuanza LLB OUT kwa hiyo kwa sheria nyingi niko mtupu! Nilishazoea kujichukulia sheria zangu mkononi!
 
Siasa tupu...Dr Slaa ndio afikishwe the hague kwa kukaidi amri halali na kusababisha vifo!
Wewe mtupu kweli kichwani kama mapolisi. Sio kila amri ni halali... Kamuulize Kikwete kwa nini anang'ang'ania kujenga barabara ya lami ngorongoro kinyume na amri halali aliyopewa na bwana wakubwa?
Kua angalau inchi tatu zaidi ili ujue sio kila amri ni halali! Ziko zingine ni batili ati! hata hiyo amri wanayopewa askari piga ua ni batili!
 
Dk Helen Kijo Bisimba kama mtaface financial constrain ili kufungua na kuendesha kesi hii nawashauri mmseme tuwachangie kama tunavyoichangia CDM.
 
mAMA TUPO NYUMA YAKO,WAMEZOEA SANA HAWA. USIMSAHAU NA MWEMA NA KUNDI LAKI. PIA MWEMA ABADILI JINA AITWE SAID MBAYA
 
hizi ni hasira zitakazofanikiwa, au ni hasiza za watu wasiojua nini maana ya icc na kesi za aina gani zinatakiwa kwenda pale? hivi ukiwa na hasira ndio uchukua njia isiyo sahihi ambayo hautafanikiwa, utachekwa tu na kuonekana hauna akili?
 
Kufika The hague directly unaweza usifunguliwe mlango.Ila ukianza lobby na regional offices, other international human rights watch dogs,kuna uwezekano ukafika The Hague na hot news.

Uswiss kuna office NGOs nyingi sana za human rights,suala la kwenda uholanzi ni suala la campaign zaidi kabala ya kujiweka mahali pa kisheria.What if patahitajika mahakama maalumu?Zitapatikana wapi hela?Mbona watu wengi sana huwa mashitaka yao wanasema wanashitaki mahakamani , ila kiukweli wengi hupitia polisi kwanza.

Njia yoyote atakayopitia mama kidjo ni njema bora afike pale panapostahili.
 
The Hague iko uswiss...hahaha,jamani we nawe ni mwandishi wa habari au?....The Hague iko uhalanzi bro, the Netherlands...halafu kwa kifupi, pale LHRC ni wabovu sana wa sheria, na hawana wanasheria waliobobea kwenye masuala ya sheria za kimataifa, hakuna hata mmoja, kama yupo mtaje pale...wote hawajui zaidi ya kupiga tu kele....

Nashauri watafute ushauri labda kwa wanasheria walioko pale ICTR arusha, ila pale, kuanzia kijo wote hawajui sheria inayohusu hayo..ndio maana hadi leo hii wanaamini kwa matendo yaliyofanywa tu na polisi yanafikia kiwango cha kushitakiwa the hague, pale wamejaa vilaza watupu.

Hiyo nchi kwenye red iko bara gani? Unakosoa kumbe na wewe kiazi!
 
The Hague iko uswiss...hahaha,jamani we nawe ni mwandishi wa habari au?....The Hague iko uhalanzi bro, the Netherlands...halafu kwa kifupi, pale LHRC ni wabovu sana wa sheria, na hawana wanasheria waliobobea kwenye masuala ya sheria za kimataifa, hakuna hata mmoja, kama yupo mtaje pale...wote hawajui zaidi ya kupiga tu kele....

Nashauri watafute ushauri labda kwa wanasheria walioko pale ICTR arusha, ila pale, kuanzia kijo wote hawajui sheria inayohusu hayo..ndio maana hadi leo hii wanaamini kwa matendo yaliyofanywa tu na polisi yanafikia kiwango cha kushitakiwa the hague, pale wamejaa vilaza watupu.

Kwa bahati mbaya sana umeongea bila kuwa na evidence ya ni wapi na wapi wanasheria wa LHRC walipowahi kusimamia kesi wakashindwa ama kwa uzembe ama kwa 'kutokujua kitu'. Pia huwajui wanasheria Kama Madame.Lulu Urio,Harold Sungusia.. Hujui kama ni mwaka jana tu Madame.Hellen Kidjo Bisimba amerudi toka masomoni na hujui alikuwa akisomea nini.. Huwa napenda kusoma comment za watu hasa zenye ushahidi.. Hii ya kwako si tu kwamba imekosa ushahidi bali imepoteza credibillity ya kuitwa comment.

Thanks
 
Kufika The hague directly unaweza usifunguliwe mlango.Ila ukianza lobby na regional offices, other international human rights watch dogs,kuna uwezekano ukafika The Hague na hot news.

Uswiss kuna office NGOs nyingi sana za human rights,suala la kwenda uholanzi ni suala la campaign zaidi kabala ya kujiweka mahali pa kisheria.What if patahitajika mahakama maalumu?Zitapatikana wapi hela?Mbona watu wengi sana huwa mashitaka yao wanasema wanashitaki mahakamani , ila kiukweli wengi hupitia polisi kwanza.

Njia yoyote atakayopitia mama kidjo ni njema bora afike pale panapostahili.

Very good analysis.. Kuna wanaodhani kuwa kwenda The Hague ni kama unakwenda kituo cha polisi au serikali za mitaa. Kuna taratibu na lobbying za hali ya juu!. Ni lazima kuhakikisha kuwa unayo support ya kutosha ya mashirika wenzako waone kweli uliyo nayo ni issue ndipo uisogelee The Hague.
 
Back
Top Bottom