Bi Harusi Matatani Kwa Kumng'ata Bwana Harusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bi Harusi Matatani Kwa Kumng'ata Bwana Harusi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 24, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bi Harusi mmoja nchini Marekani amejikuta akiingia matatani na kupigwa marufuku kumsogelea mumewe baada ya kumng'ata mumewe huyo usiku wa sherehe ya harusi yaoBi Harusi, Bernadette Besario Catan-Keeler mwenye umri wa miaka 30, amejikuta akiingia matatani baada ya kuyashindilia meno yake kwenye mabega na mikono ya mumewe wakati wa sherehe ya harusi yao.

  Tukio hilo lilitokea Florida nchini Marekani baada ya bwana harusi aliyetajwa kwa jina la Mike Catan-Keeler, kuchukizwa na kitendo cha bi harusi kuanza kucheza dansi na mwanaume mwingine na hivyo kuamua kuondoka toka kwenye ukumbi ambamo sherehe ya harusi yao ilikuwa ikifanyika.

  Bernadette alimfuata Mike nje ambapo mzozo ulizuka na bila kuvuta subira alimsukuma na kisha kumng'ata kwenye bega lake la kushoto.

  Mzozo huo uliendelea kwenye nyumba ya wanandoa hao ambapo, Bernadette alimchania shati Mike na alimng'ata tena mkononi.

  Bernadette alifikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya shambulio la kudhuru mwili.

  "Kwa wanandoa wapya, huu si mwanzo mzuri wa maisha ya ndoa", alisema John Hurley, jaji wa kesi hiyo katika mahakama ya Broward.

  "Naamini hii itaakuwa ni kama kujikwaa kwenye kisiki, naamini mtazimaliza tofauti zenu na kuanza maisha marefu ya pamoja", alisema jaji Hurley.

  Mike alimuomba jaji amuonee huruma mkewe akisema kuwa wakati Bernadette anafanya matendo hayo alikuwa amelewa.

  Akimuachia huru kwa dhamana , jaji Hurley aliamuru Bernadette aache kunywa pombe na akae mbali na mumewe..
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duu!! Hii hatari
   
Loading...