Bi. Fatma Jumanne, msaidizi wa nyumbani wa Bi. Joyce Mukya, anashikiliwa na Polisi akihojiwa kusuhu Mbowe Kuvunjika Mguu

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Inasemekana hali imezidi kuwa tata na haijulikani alipo! Ndugu yangu aliyepo Dodoma jirani yao kanitonya!

=====

1592485165641.png

Tumefuatilia kwa karibu taarifa za Polisi Tanzania kumshikilia Bi. Fatma Jumanne, msaidizi wa nyumbani wa Bi. Joyce Mukya, kinyume cha sheria tangu jana. Amekuwa akihojiwa kama shahidi wa jeshi hilo kuhusu tukio la kuvamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa Mkiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe.

Jana jioni jeshi hilo likabadili na kuanza kumhoji kama mtuhumiwa, kuwa ametoa taarifa za uongo kuhusu tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Mhe. Freeman Mbowe Bi. Fatma amenyimwa dhamana huku zikiwepo taarifa za kupigwa na kuteswa. Tutatoa taarifa kamilo juu ya suala hili.

Kwa mujibu wa mawakili wanaofuatilia suala hilo, katika mahojiano aliyofanyiwa, Bi. Fatma amelalamika kuwa amekuwa akilazimishwa aseme mambo ambayo hayajui, wanayotaka polisi, kuhusu tukio la kuvamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe.Freeman Mbowe.

Kutokana na mazingira yanayozunguka suala la kuendelea kushikiliwa, kutofikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana kwa Bi. Fatma kinyume cha taratibu za kisheria, tayari wanasheria wameanza utaratibu wa kuwasilisha Mahakama Kuu ombi maalum la kulitaka Jeshi la Polisi limwachie.

Chanzo: CHADEMA
 
Inasemekana hali imezidi kuwa tata na haijulikani alipo! Ndugu yangu aliyepo Dodoma jirani yao kanitonya!

Weka maelezo ya kutosha, sijui unakimbizwa au kunashida gani. Kama huna taarifa za kujitosheleza kuhusu jambo fulani, ni bora ukusanye habari ili uwape walaji kitu kilicho jitosheleza.
 
Ukizaliwa na nyoka huwezi badirika kuwa kenge, hata sefulia utataka kuligonga Kwa sababu tu jinsi ulivyolelewa na kukarilishwa
 
Kwani huyo Fatma ndiye alikuwa na mbowe au alikuwepo mbowe alioumia? Haya mambo mengine yanatia kichefuchefu. Kwa nini wasimkamate huyo boss wakwe pamoja na watu wengine ambao walikuwa na mbowe siku hiyo?

Aliitwa kama shahidi ili atoe maelezo, sasa hawa polisi wamekosa namna wakaona wamgeuzie kibano.
 
Mambo yanazidi kuwa moto , ni vizuri Bi. Fatma Jumanne amepata ufatilizi wa ndugu, jamaa, CHADEMA na jeshi la Polisi. Maana mambo haya hayatakiwi kwenda kimya kimya .
 
Mbowe ajitafakari
Asimuingize beki tatu kwenye siasa chafu

Mbowe ukikunywa pombe kwa starehe ako basi usimsumbue dada wa kazi
Muachieni huyo mtoto wa watu nyie wajinga, mmemkamata mnamlazimisha aseme Mbowe alikuwa amelewa, mtoto wa watu anakataa kusema uongo wenu ndio mnamshikilia siku zote hizi bila kumpeleka mahakamani mnaogopa aibu.
 
Chadema baba wa uongo, msije mkamdhuru tu binti wa watu kutafuta political mileage
 
Bi. Fatma amelalamika kuwa amekuwa akilazimishwa aseme mambo ambayo hayajui
Sasa kilichokuwa kinawawasha ni kitu gani hadi wakimbilie kutoa statement ya kijinga vile kuwa wameshamaliza kazi. Sasa huyunae Housegirl anajua nini? Kwanini Polisi wetu wanakua hivi? Unamuumiza mtoto wa mtu kisa tu unataka kuufurahisha umma? Mbona Mbowe kakaa kimya? au mnaogopa kitu gani?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom