Bi. Fatima Matola: Mama mpigania uhuru wa Tanganyika asiyefahamika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
Hapo chini ni nyumba ya Bi. Fatima Matola mwanachama wa TANU mazalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika.

Baba wa Taifa alikuwa akifikia nyumba hii wakati wa kupigania uhuru.
Nani keshapata kusikia jina hili la Bi. Fatima Matola?

Kuna hotuba ya Baba wa Taifa anasema kuwa safari yake ya kwanza baada ya kuundwa TANU mwaka wa 1954 alikwenda Mbeya.

Lakini Nyaraka za Sykes zinaonyesha kuwa safari ya kwanza ya Baba wa Taifa ilikuwa Mororgoro akifuatana na Zuberi Mtemvu.

Kuna barua ya tarehe 15 Agosti, 1954 mwezi mmoja tu baada ya kuundwa TANU kutoka kwa Mtemvu akimwandikia Ally Sykes, Mtemvu akieleza matatizo waliyoyapata yeye na Nyerere Morogoro katika kuitangaza TANU.

Hii ndiyo safari ya kwanza ya Baba wa Taifa katika kuitangaza TANU na safari ya pili ilikuwa Lindi.

Ikiwa safari hii ya Mbeya kwa namna yoyote ilikuwa ndiyo ya kwanza basi Baba wa Taifa alifikia nyumbani kwa Bi. Fatima Matola ambae nyumba yake ndiyo hiyo hapo chini kwenye picha.

Kuna mtu yeyote anaemfahamu shujaa huyu atupe historia yake?

Picha kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima Jumamosi Oktoba 14, 2017
 
Bila shaka hapa ni Soko Matola.
upload_2017-10-14_21-26-33.jpeg
 
Mimi napenda sana history ziwe wazi kwa mana tusipende uongo hadi kwa watu ambao wametangulia mbele za haki, mtu akifa story au uhalisia wa maisha yake hayawezi kuleta tatizo lolote kwa sisi ambao tupo hai,,
Kwa mfano kama wagombania uhuru walikuwa wengi ila kama aliteuliwa mtuwambae wanadhani atafaa kusimamia hilo basi asipewe kipaumbele sana kwamba ni wewe aliganikisha jambo hilo la uhuru je leo tujiulize kila kukicha panapatikana muasisi mwingine wa kushiriki, au kushauri, au mwasisi flani', History haipo wazi nchini kwetu wekeni history ili nchini kujibebe kiutalii jamani, kuna sisi watu tunapenda ukweli wazee
 
Mzee saidi unajua mengi sana, Nilikuwa najiuliza neno soko matola mbeya limetoka wapi?
 
Kwa hiyo baba wa taifa kufikia nyumbani kwa huyo mama ndo kunamfanya huyo mama awe mpigania uhuru wa Tanganyika au kuna mengine zaidi aliyoyafanya?
Nyani Ngabu,
Katika miaka ya 1950 wakati TANU inapambana na Waingereza kudai uhuru
Nyerere akiwa kiongozi ulikuwa huwezi kumkaribia kirahisi.

TANU ilikuwa na kikosi chake maalum Bantu Group ambacho kazi yake kuu
ilikuwa ulinzi na uhamasishaji.

DomeS9UO-eEp4pl70R0AFEWD_y2XK8fBDKPXO1E-9f2M0Gwp_jsQ2pbC3Yc2YegivcibpioQMxm8aJua7Brctg_1p19UkzRh0BtmyEAqcBKzBa7lPriofow2fXMR7x-A0tKKlly5lEc7gq4Ow9imrxk83OX76fIo6p50Nu3t1vayjrOq-nLrfxw8V4hrrmrTvPHXjI8oaNFRMxaxgBd5VqU0eMGhEPzZpl0jGfCSBOxvF-GR84GudwpBgTBYbpPHQt7z28aJmwD6foj9T_5kvq2HCkaoeRFterv6ZfJ8uk2jyvFLJR5qpnYN3pHMe-dqtNiGHTmHxn_0C_epAH3jYnizTcKOg7gaXbmcHO0VLxv1YkC57B8ZK6mvU2TF-kEuOiZ5uLPyv4kZr9AqDhWSAFGBcQPKWyRHfDTQAJwA6Gx3fK7BhOEN1idxkoCC9oFMOxO9fTzUkaeWeZofmM4w5W7hSIqXICTQxxB2sqjXBbOkMdY4asKPtptgAQfap2vzDDom9la0oyTy6B85aJYMm1CjPTU0o5ZKFT_6KgTsa9xRkTctyQXg2D050ol6ql0ldYEk0tTU2LH-WE04pZwxH1Z41BKVACEZae_shLLJ=w822-h629-no

Mbele kulia ni Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia na nyuma yao ni Bantu Group angalia silaha za jadi
walizobeba.

Nyerere alikuwa akila na kulala akiwa safarini kwa watu walioaminika.

Nyerere alipoacha kazi alihamia Dar es Salaam na alikaa nyumbani kwa Abdul
Sykes,
Mtaa wa Stanley na Sikukuu.

TANU haikuamini Nyerere akae na mtu yoyote yule isipokuwa akakae kwa Abdul.
Sasa ukitaka kujua kwa nini iliamuliwa hivyo mjue Abdul alikuwa nani katika TANU.

Halikadhalika jiulize ilikuwaje Nyerere alipokwenda Lindi mwaka wa 1955 kwa nini
alifikia nyumbani kwa Suleiman Masudi Mnonji Mtaa wa Makonde.

Jiulize pia kwa nini Nyerere alipokwenda Moshi alifikia nyumbani kwa Mama Halima
Selengia.

Jiulize tena kwa nini Nyerere alipokwenda Tabora mwaka wa 1958 kweny mkutano
wa Kura Tatu alifikia nyumbani kwa Issa Kibira.

Jiulize mwenyewe hawa ni nani?

Basi unaposikia kuwa Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika alifikia nyumba
ya Mama Fatma Bint Matola elewa kuwa huyo alikuwa mpigania uhuru na katika viongozi wa
juu kabisa katika TANU.
 
Na kwa msingi huo ndipo tunaposema ni vigumu kutenganisha ukombozi wa Tanganyika na waislamu. Huitaji jicho la3 kubaini hilo.
 
Hapo chini ni nyumba ya Bi. Fatima Matola mwanachama wa TANU mazalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika.

Baba wa Taifa alikuwa akifikia nyumba hii wakati wa kupigania uhuru.
Nani keshapata kusikia jina hili la Bi. Fatima Matola?

Kuna hotuba ya Baba wa Taifa anasema kuwa safari yake ya kwanza baada ya kuundwa TANU mwaka wa 1954 alikwenda Mbeya.

Lakini Nyaraka za Sykes zinaonyesha kuwa safari ya kwanza ya Baba wa Taifa ilikuwa Mororgoro akifuatana na Zuberi Mtemvu.

Kuna barua ya tarehe 15 Agosti, 1954 mwezi mmoja tu baada ya kuundwa TANU kutoka kwa Mtemvu akimwandikia Ally Sykes, Mtemvu akieleza matatizo waliyoyapata yeye na Nyerere Morogoro katika kuitangaza TANU.

Hii ndiyo safari ya kwanza ya Baba wa Taifa katika kuitangaza TANU na safari ya pili ilikuwa Lindi.

Ikiwa safari hii ya Mbeya kwa namna yoyote ilikuwa ndiyo ya kwanza basi Baba wa Taifa alifikia nyumbani kwa Bi. Fatima Matola ambae nyumba yake ndiyo hiyo hapo chini kwenye picha.

Kuna mtu yeyote anaemfahamu shujaa huyu atupe historia yake?

Picha kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima Jumamosi Oktoba 14, 2017
Bado ipo hii nyumba? Ienziwe, iwekwe kuwa moja ya kumbukumbu za historia za taifa. Nadhani "soko matola" ni njia pia ya kumuenzi huyo bibi.
 
Na kwa msingi huo ndipo tunaposema ni vigumu kutenganisha ukombozi wa Tanganyika na waislamu. Huitaji jicho la3 kubaini hilo.
Wewe ulitaka utenganishweje labda? Taifa lilikuwa na waumini wa dini nyingi, ukiwepo na uislam, jadi, Ukristu nknk Ulitaka iweje labda? Waislam wasingeshirikishwa ama? Akina Rupia, Chief Kunambi na wengineo nao si walishiriki au?
 
Mkuu hoja yangu hapo ni kuwa waislamu wana mchango wa kipekee ktk ukombozi na uhuru wa Tanganyika, so tuanzie hapo kama unabisha au vip!?
Then ntakupa hoja, mifano, dalili na sababu!
Twende kazi
 
Sawa, natuanzie hapohapo Mkuu! Tuyajibu kwanza maswali haya tu machache. 1.upi ulianza nchini, uislamu au ukristu? 2. Nani alihisi kudhulumiwa na utawala wa kikoloni wa kizungu? 3. Mapigano ya ukoloni yalianza mwaka gani na je aliyeanzisha ni nani? Tukiyajibu haya maswali, tutajua ni nani na madhumuni gani alipigania uhuru wa taifa hili. Je ni muislamu au mwafrika mweusi aliyedhirumiwa vya kutosha na ukoloni wa race zingine? Uje na ufike hadi mapinduzi ya Zanzibar.
 
1.historia inatwambia uislamu ndyo dini ya kwanza kuingia ktk uga wa A.mashariki. rejea " The Early contacts btn Africa and Asian countries" lkn pia historia hyohyo inajibu swali la ukongwe wa dini ya kiislamu na hyo inayodaiwa kuitwa dini ya ukristo, uislamu ulianza tangu karne ya 4th, ikumbukwe uislamu ulikuwepo hata kabla ya kuja mtume wa
mwisho Muhammad, uislamu ulikuwepo tangu enzi za musa(moses), daudi(zaburi) na Adam. Karne ya 7th and ilianza kusambaa.rejea kitabu cha Islamic civilization, cha Abilal Almahdood. Encyclopedia Africanica n.k.
2. Waafrika walihisi kudhurumiwa na ukoloni mkongwe, lkn hapohapo na waislamu kwa nafasi ya upekee walikuwa wakihisi kuonewa na kudhurumiwa huo ukoloni hapa tunarejea vita vya maji maji ikumbukwe hii kwa waislamu ni Jihhad lkn kwa kuwa historia imefichwa wengi mnajua ilikuwa ni vita ya ukoloni mkongwe, kwa ujumla hili ni darasa lengine kwako cyo Leo, lkn itoshe kufahamu hata ktk kipindi hiko madai ya waislamu yalikuwepo. Vile vile kufutwa kwa baraza la waislamu lililokuwepo wakt wa ukoloni kabla hili la bakwata.
3. Mapigano ya kikoloni yalianza tangu karne ya 14th(during primitive mercantilism in Europe) the so called, period of plundering and looting of precious goods, raw materials in Africa.

Back
Top Bottom