Bi. Anna, avunjwa mkono na askari polisi Manyoni

sizy

Member
Jun 14, 2010
29
4
Askari polisi anayejulikana kwa jina la Ester ambaye anafanya kazi katika ofisi ya polisi Manyoni amempiga na kumvuja mkono bi Anna anayeishi katika mtaa Kaloleni.

Taarifa za awali zina sema kwamba Polisi huyo alifika nyumbani kwa bi Anna kwa ajili ya kumkamata kwa sababu ya kutuhumiwa na majirani kwamba anawatesa watoto wake.

Polisi huyo badala ya kumchukua Bi Anna na kumpeleka kituoni, alianza kumpiga na baadaye kwa kumvunja mkono kwa kutumia mpini wa jembe la mkono.

Taarifa hizi zilimfikia OCD wa wilaya ya Manyoni naye kuamru apewe PF3 na apelekwe hospital ili kuthibitisha kama mkono huo umevunjika

Dakitari wa Hospital ya wilaya ya Manyoni Dr. Mollel alithibitisha Mkono wa Bi Anna Kuvunjika ila haukusababishwa na Kipigo cha Askari bali ulivunjika wenyewe na siyo siku ya kipigo.

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni.

Watu wanajiuliza iweje mtu avunjike mkono halafu aendelee kukaa nyumbani pasi na Matibabu!? Je Dr alikuwa katika hali gani kiyajua haya! Afande Ester aliwezaje kumpa kipondo mtu ambaye ni tayari mgonjwa aliyevunjika mkono!?

Wito wetu ni kuviomba vyombo vyenye mamlaka kulifanyia uchunguzi hili, haki itendeke!

[HASHTAG]#VoiceForVoiceless[/HASHTAG]
[HASHTAG]#WeNeedJustice[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Fight4Manyoni[/HASHTAG]
 
acha avunjwe anastahili maana anatesa watoto wasio na hatia
 
Mtaacha ishu ya msingi ya kuteswa watoto mtahamia kwenye kuvunjwa mkono, mkono unatibika ndani ya wiki sita na watoto je
 
Tuhuma za Anna zitathibitishwa na mahakama tu kwa mjibu wa sheria. Isitoshe mleta mada kasema Anna anatuhumiwa kunyanyasa watoto, hoja hapa amewanyanyasaje mpk aadhibiwe on spot?. Napinga udhalilishaji watoto lkn napinga zaidi polisi kupiga mtuhumiwa.
Afande Ester umeshindwa kazi unasitahili kutumbuliwa na kushitakiwa kwa shambulio maramoja.
 
hili ni jambo la kawaida, Polisi wapo juu ya sharia.
 
Hawez kuwatesa watoto wake, huyo bibie anawarudi watoto wake, msilichukulie suala hili kisiasa
 
Hii Tabia ya Polisi kushambulia washtakiwa inaota mizizi sana siku hizi, wao wanajiona ndio wao kwa kila kitu Esther ashitakiwe na Anna ashitakiwe pia wote kwa mujibu wa sheria , sio mmoja aachwe kwa sababu kuna watu wanamlinda hapana haitokubalika
 
kama alikuwa anatesa watoto angemvunja kiuno kabisa
Bado imebaki kuwa imagination na ndio maana hata wewe umeanza na kama....!! Hata hivyo hakuna sheria inayotaka polisi amuhukumu mtuhumiwa kwa kosa alilofanya judgment zote hufanyika mahakamani tena si kwa maamuzi au utashi binafsi wa Hakimu Bali ni kwa vifungu vya sheria
 
sawa mkuu .. nimeanza na kama sababu sina uhakika
 
Back
Top Bottom