Bhoke Munanka, Waziri wa zamani wa Nchi ofisi ya Rais akishughulika Usalama, afariki

Naomba tuweke rekodi sawa kwenye mjadala unaoendelea.

Kuna mjumbe alisema kwamba Mzee Munanka alikuwa importer wa magari ya scania, nadhani hapo ilikuwa kabla wa-Swede hawajajenga ile plant yao pale Kibaha.

Kijiji chetu (zama zile za ujamaa) kilifanikiwa kununua lori la scania mwaka 1978, hiyo ina maanisha kwamba hayo magari yalikuwepo kabla ya kujengwa kwa ile plant pale Kibaha.

Nikitumia maelezo ya Mkuu FMES Marquiz walianza kutumia mtindo wa Chenkeencha, telemuka tangu mwaka 1979 na hapo walikuwa wanatumia hiyo style ya LBT 111.

Labda tuulize sasa, before 1983 nani alikuwa akiingiza hayo magari hapa nchini kwa kuwa tayari yalikuwepo.

Wenye taarifa zaidi endeleeni kutuwekea then tutasoma na kujua kipi ni kipi.
 
kumbe ufisadi ulianza long time!tupeni news ambao hatukuwepo miaka hiyo
 
Madela-wa Madilu,
Facts, ndugu yangu, facts.
Ile meli haikuzama kwa sababu haikuwa lakeworthy. Meli ilizama kwa sababu ilipakia watu kupita kiasi. Kuna rafiki yangu aliikosa meli hiyo anasema ilipokuwa inaondoka Bukoba tayari ilikuwa imeshaanza kuelemea upande mmoja.

Huu ndio ukweli wenyewe jamaa ni jazba tuu
Wala hakuhusika na ununuzi wa ile meli na ndege za ATC bali ni Agustino mwingira menejat TRC enzi hizo ni Juma Lweno na ile meli ilinunuliwa mpya kabisa
Jamaa hana data ila ana Jazba tuu
Utamwitaje fisadi wakati aliamua kuwaachieni serikali yenu mbona huyo Chenge kawaibia na bado anang'ang'ania
Lowasa ameanzisha operesheni ya kujisafisha ili arudi tena
Please use your common sense
 
Sasa kuna kosa gani hapa la Ufisadi kuendelea kuwa na deal na serikali wakati unajua fika hakuna mtu aliyeweza kufanya biashara yoyote bila idhini ya vyombo vyetu. Tanzania hadi leo hiii hata ufanye biashara gani halali bado unatakiwa kupitia vyombo hivi. nachokuomba sema wazi ni kitu gani alikifanya nje ya sheria!.. kufanya deal na serikali hata mimi nimewahi ku supply Maharage Magereza enzi za mwalimu unataka kusema nilikuwa fisadi?

Mkuu kama yako ni the case, basi Rostam na Lowassa wamekosa nini? Hivi kuna kitu hata kimoja cha ufisadi ambacho kimefanywa nje ya sheria?

Ni Hotel gani aliyolala kwa usiku mmoja akalipa dollar 5000.. na hukusema mwaka gani, Hivi leo nikienda lala hotel ya $1500 kwa usiku mmoja Ufisadi wangu ni upi?.. nitazidi kukuuliza mkuu alipokuwa madarakani ni hotel gani ilitoza hizo dollar na hesabu hizi umezipata wapi?..

Nimesema nimechoka na mafisadi kuwaibia wananchi hku wakienda nje na kuala hotel za Dola $ 5000 kwa siku kwa hela zetu walipa kodi, sikusema ni Bhoke ndiye aliyefanya hivyo, nimetoa mifano mingi sana kuhusu wizi wake, sasa nashangaa kuwa bado unataka niseme tu huku huna majibu ya niliyoyasema tayari,

ninarudia tena kuwa hawa mafisadi muwaambie kuwa hatutakuwa na msamaha nao hata wakifa, kwa sababu wanayoyafanya wakiwa wazima pia huuwa wananchi wengine wasiokuwa na nguvu au kujuana na rais aliyeko madarakani, muwaambie waache wizi wa hela za taifa, huyu
Bhoke ndiye chanzo cha kununua ndege mbovu a ATC, Meli mbovu za TR, yaani I can go on and on! he is just a fisadi!
 
Labda tuulize sasa, before 1983 nani alikuwa akiingiza hayo magari hapa nchini kwa kuwa tayari yalikuwepo.

Wenye taarifa zaidi endeleeni kutuwekea then tutasoma na kujua kipi ni kipi
.

Rostam amesema kuwa familia yake imeanza biashara mwaka 1852, kwa hiyo yeye sio fisadi, sasa huyu mzeee kwa sababu alikuwa akileta Scania mwaka 1960 basi na yeye hakuwa fisadi, what a legal defense!

Mkuu mimi sijui aliyekuwa akileta Scania, kabla au huko nyuma, lakini najua one thing kuwa huyu Mzee alikuwa fisadi!
 
Keil, Unajua inashangaza sana kuona watu tunabishana hapa wakati hawa watu wote wako Ulaya na nchi zilizoendelea...Wanayona haya kila siku za maisha yao.
Wanajua wazi nini maana ya Importer na kiwanda cha assembly pia wanafahamu vizuri kwamba Munanka hakuwa mmiliki wa kiwanda hicho..Labda Field Marshall Es anaweza kutueleza vizuri kuhusika kwa Munanka kiasi kwamba iwe ni Ufisadi..
Shukran kwa sababu nilitaka kumkumbusha Field marshall Es kuwa anajua wazi kwamba nilikuwa karibu sana na watu wenye mabus ya transport toka miaka ya 70 kwa hiyo najua ninachokizungumza.

Mkuu FMES, hakuna mtu aliyesema Ufisadi wa Rostam umeanza toka mwaka 1852 kwanza alikuwa hajazaliwa, Babu yake hajazaliwa wala kuolewa.. nani anajua!.. we careless of history ya mababu zake.
Mkuu jaribu kutuelewa tunazungumzia kitu gani.. Ufisadi wa Rostam ni leo hii hayo majigambo yake na familia yake haiwezi kuondoa ukweli kwamba yeye ni Fisadi na pengine baba yake wa karibu na wakati huu alikuwa mtu safi!
 
Wala hakuhusika na ununuzi wa ile meli na ndege za ATC bali ni Agustino mwingira menejat TRC enzi hizo ni Juma Lweno na ile meli ilinunuliwa mpya kabisa
Jamaa hana data ila ana Jazba tuu

1. Nijuavyo ni kwamba meli zilinunuliwa toka EAC, tena baada ya Rwehumbiza kuzikataa kabisa kuwa hazifai, aliznunua huyu mzee akishirikiana na Captain Frouhn, kutoka Norway, aliyekuwa amemuoa mama mmoja wa Singida, aliyekuwa Manager wa Cartering wa Railways, ambaye ndiye hasa aliyekuwa aksihirkiana na huyu mzuingu kutufanyia utapeli, baadaye serikali ilimpa huyu mzugnu masaa 24 kuondoka nchini baada ya ile ajali ya MV. Bukoba.

2. Ndege mbovu ninajua kwua alikwenda kuzinunua na Bakari Mwapachu, kabla ya hapo ATC ilikuwa na ndege za kukodi kutoka Ethiopian Airlines, zile ndege walizozinunua Saudia, zilikuwa bomu hata shirika lilipokufa ilishindikana kuziuza!

Jazba? sijawahi kuwa nayo kwenye mijadala hasira na ufisadi dhidi ya wananchi wanyonge, kweli ninakuwa nazo sana ninapojua kuwa kiongozi anyetajwa ni fisadi, kama huyu mzee marehemu huyu alikuwa fisadi tena wa kutupwa na marafiki zake kina Batengas!
 
kumbe ufisadi ulianza long time!tupeni news ambao hatukuwepo miaka hiyo

you got this right, mkuu ufisadi ulianza long time ago hii ya sasa ni maendelezo tu!

Wanajua wazi nini maana ya Importer na kiwanda cha assembly pia wanafahamu vizuri kwamba Munanka hakuwa mmiliki wa kiwanda hicho..Labda Field Marshall Es anaweza kutueleza vizuri kuhusika kwa Munanka kiasi kwamba iwe ni Ufisadi..

Bob ninasema hivi huyu mzee alikuwa fisadi period, kuwa na assembly ya Scania, haina anything to do na yeye kuwemo kwenye deals nyingi za serikali ambazo wala hazikuwa zinatangazwa kama sheria inavyotaka kutokana na connections zake,

Ninasema this man was a fisadi, kwani mafisadi hawana mashirika legitimate?
 
Field Marshal Es,
Nimeuliza hapa ni meli gani inayozungumziwa?..
Baada ya kuvunjika kwa EAC tanzania tuliambulia hizo meli za lake victoria tena Bukoba haikuwa ktk hesabu ya meli tulizochukua.
Mv Bukoba ni meli iliyopatikana baada ya kuvunjika kwa EAC tena miaka ya 80 ktk jitihada za kuboresha huduma za usafiri ziwa Victoria..
Na ajabu basi hizo unazosema mbovu Mv Victoria na ndogo kama Clarius bado zinafanya kazi hadi leo chini ya tawala nne. yaani ahat bila aibu kweli meli hizo bado mnaziweka majini wakati zimenunuliwa toka mkoloni?.. acheni FMES mbona wazushi nyie!
Hizo deal ziseme basi mbona ulimi mzito au?
 
Rostam amesema kuwa familia yake imeanza biashara mwaka 1852, kwa hiyo yeye sio fisadi, sasa huyu mzeee kwa sababu alikuwa akileta Scania mwaka 1960 basi na yeye hakuwa fisadi, what a legal defense!

Mkuu mimi sijui aliyekuwa akileta Scania, kabla au huko nyuma, lakini najua one thing kuwa huyu Mzee alikuwa fisadi!

Mkuu FMES,

Sikuwa na lengo la kutetea mtu, bali nilikuwa ninajaribu kuweka rekodi sawa. Kuna mtu (Dua) alikuwa hana uhakika kama scania zilikuwepo Tanzania tangu 1970, na kuna mwingine alisema Mzee Munanka ndiye alikuwa anafanya biashara ya ku-import hayo malori ya scania.

Lengo langu ilikuwa ni kuchokonoa zaidi ili nipate more details na ndiyo maana nikaonyesha kwamba malori ya scania yalikuwepo muda mrefu kabla hata TAMCO haijajengwa.

Ilikuwa ni juu ya wachangiaji kuangalia kama ni kweli Mzee Munanka alikuwa ana-import hayo malori. Je, alifuata sheria na taratibu zilizokuwepo wakati huo? Je, alikuwa anaagiza yeye mwenyewe kwa fedha zake ama alikuwa anashirikiana na makampuni ya nje? Kama alitumia fedha zake alizipataje kiasi cha kufanya biashara kubwa kama hiyo?

Nadhani haya ni maswali ambayo yako valid ili kuweza kum-judge mtu kama alitumia vibaya nafasi yake serikalini kwa maslahi yake binafsi ama alikuwa anafanya biashara kama mfanyabiashara wa kawaida.

Ndiyo maana mwishoni nikasema wenye details wazimwage hapa ili tusio na hizo info tuchambue.
 
Kumbukumbu yangu inaniambia kwamba EAC ilipokufa hakukuwa na mgawanyo proper wa mali zilizokuwa zinamilikiwa na mashirika ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Bandari, Posta na Simu, Reli, Usafiri wa Anga na mengineyo).

Je, hiyo meli ambayo ilinunuliwa kutoka EAC iliuzwa na nani wakati EAC ilishasambaratika (yaani ni nani alikuwa msimamizi wa uuzaji wa mali za EAC).

Shirika la Reli Tanzania (TRC), mmiliki wa meli iliyozama, lilianzishwa 1978. Meli inayosemwa imekuja 1980s (kulingana na info zilizopo hapa forum) na wakati huo EAC ilishakufa kitambo, sasa ni EAC gani iliyouza hiyo meli?

Wenye details tunaomba ili kuweka rekodi sawa.
 
Ndiyo maana kuna sehemu nimesema itabidi tu-revisit the meaning of the word fisadi.
Marehemu Munanka alikuwa mfanyibiashara kabla ya kuingia serikalini. Na alipoona inafaa arudie biashara zake, aliacha kazi serikalini akiwa kijana kabisa. Kama alikuwa na contracts za serikali hili halimfanyi fisadi kwa mtazamo wangu. Huwezi kumweka huyu leo kwenye kundi moja na akina Lowassa ambao hata hela yao ya kwanza ya kuagizia daladala waliibia serikali, au akina Chenge ambaye kila mkataba uliopita mezani kwake alikwapua $200k na biashara nyingine za madawa ya kulevya, au akina Rostum ambao wanaunda kampuni bandia na kwenda kuchota benki mamilioni ya pesa za walalahoi. Mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani. Kufanya biashara si kosa na natamani Munanka angekuwa mfano kwa viongozi wa sasa ambao wameng'ang'ania vyeo serikalini na huku wanaendesha biashara zisizo na vichwa au miguu.
 
Yote semeni kuna chumvi na ukweli kuhusu Munanka na mikataba ya serikali. Alikuwa lobyst, na kazi ya lobbyst yeyote ni kuja udhaifu wa upande mwingine na kuutumia kwa faida ya mteja wake. Udhaifu wa wasomi wa Tanzania wakati ule, na nachelea kusema hata sasa, ni kuogopa kusimamia principals na kuchunguza mtu anayemtetemesha kwa kutumia jina la ikulu. Hicho ndicho kilichowapata wasaini mikataba enzi hizo kutoka kwa type ya akina Munanka. Juzi tu waziri Mkuu Pinda kazima mjadala wa Kagoda kwa kusingizia usalama wa Taifa, nani bungeni anathubutu kuuliza uhalali wa kauli hiyo?
 
Msipindishe ukweli. Magari yaliyotumika sana kupeleka mizigo Zambia enzi hizo yalikuwa Ni Fiat 682 /690 etc. Sikuwahi kuona hata scania moja enzi hizo. Ukienda Mbeya kuna sehemu inaitwa Mafiat kuenzi magari yaliyokuwa yakiegesha eneo hilo njiani kuelekea au kutoka Zambia!!
 
Naomba Kujua Mwalim Nyerere alimchagua Mh. Malima kuwa Wazir wa Uchumi na Mipango wa wakati gani?....nahitaji kujua hilo ili niunganishe dots juu ya mjadala unaoendelea!!!

Thanks ES kwa habari uliyotupa kama uongo wa Ukweli tutaujua...Bob Mkandara tunashkuru kutetea kile unachokijua...
 
Sijui kama Malima alikuwa waziri wa Wizara hiyo chini ya Nyerere. I bet a nickel ilikuwa chini ya Mwinyi.
 
MKJJ....Nafikiri ES bado yupo online...atusaidie...au kama unae senior karibu tuwaulize...
 
1. Peter Siyovelwa
2. Edward Sokoine
3. John Malecela
4. Paul Sozigwa
5. Job Lusinde
6. Amir Jamal
7. Mack Bomani
8. Adam Sapi
9. Daudi Mwakawago
10. Mhaville
11. Leader Sterling
12. Dr. Bryson
13. Said Maswanya
14. Erasto Mange'nya
15. Lucy Lameck
16. Bibi Titi Mohamed
17. Nossoro Moyo
18. Elinawinga
19. Simon Chiwanga
20. Aaaron Chiduo
21. Ibrahim Kaduma
22. Abdallah Twalipo
23. Abdallah Natepe
24. Thabit Kombo
25. Idrisa Wakil
26. Aboud Jumbe
27. David Musuguri
28. Nsa Kaisi
29. Dr. Salim Salim
30. Gisley Mapunda

Na wengineo wengi ambao siwezi kuwakumbuka vizuri, lakini hawa niliowataja ninawakumbuka sana kuwa walikuwa ni wasafi kabisa, ingawa baadaye kuna watu kama Sozigwa na Mwakawago, walishia kuchafua records zao lakini bado sio kwa ufisadi wa hali ya juu kama wengine ambao sikuwataja hapa.

Ahsante Mkuu!

Mwingine ni Augustino Lyatonga Mrema:confused:
 
Naomba Kujua Mwalim Nyerere alimchagua Mh. Malima kuwa Wazir wa Uchumi na Mipango wa wakati gani?....nahitaji kujua hilo ili niunganishe dots juu ya mjadala unaoendelea!!!

Thanks ES kwa habari uliyotupa kama uongo wa Ukweli tutaujua...Bob Mkandara tunashkuru kutetea kile unachokijua...

Malima ni waziri aliyekuwa kipenzi cha Mwalimu ni alipigania sana uhuru wa nchi yetu akaenda kusoma Marekani na akapewa kuwa mkuu wa chuo cha Fedha(IFM) wa Kwanza na Mwalimu Nyerere, akaenda tena Marekani na mwalimu akamrudisha nyumbani na ni Malima aliyepinga kununuliwa kwa meli kwa kusema kuwa haikuwa na viwango watu wakaenda Ikulu kwa Mwalimu Nyerere nae akamwambia Professor Malima kubali tu, ndio maana Ripoti ya mauaji ya MV Bukoba yamefanywa siri kubwa hadi leo hii hakuna ripoti ya ajali ile kwani inamgusa Mwalimu moja kwa moja kwa kudanganywa na watu wake na Marehemu Malima alipinga vikali.

Rais Mwinyi amemridhi Malima kutoka kwa Nyerere kama alivyowarithi kina Warioba au John Malecela na mwingine wa karibu sana kwa mwalimu alikuwa Mustafa Nyang'anyi akamfanyia hadi mpango wa kuwa balozi marekani kipindi cha Mkapa.
 
Sijui kama Malima alikuwa waziri wa Wizara hiyo chini ya Nyerere. I bet a nickel ilikuwa chini ya Mwinyi.
Mwanakjj
Hili nalo hulijui? basi hujui historia ya nchi yako.Fuatilia kesi ya uchaguzi kati ya Professor MALIMA na Abbas Mwingamno jimbo la MKuranga wakati wa Mwalimu lilikuwa jimbo la Kisarawe.

Kipindi cha Mwinyi huyu PROFESSOR malima alipewa uwaziri wizara ya elimu,biashara na Fedha, kipindi cha Mwalimu alikuwa na wizara yenye dhamana na ununuzi wa MV bUKOBA.
 
Back
Top Bottom