Bhoke Munanka, Waziri wa zamani wa Nchi ofisi ya Rais akishughulika Usalama, afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bhoke Munanka, Waziri wa zamani wa Nchi ofisi ya Rais akishughulika Usalama, afariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jul 26, 2008.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mwanasiasa mkongwe Bhoke Munanka (81) Amefariki dunia katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kuanzia juzi.

  Munanka mmoja wa wanasiasa wa walioshiriki kupigania uhuru wa Tanganyika.

  Alikuwa miongoni mwa mawaziri katika baraza la mawaziri la kwanza la mawaziri wa Tanganyika huru, akiwa waziri wa Nchi Ofisi ysa Rais akishughulikia Usalama wa Taifa.

  Amewahi pia kuwa mbunge wa Tarime na Mhasibu mkuu wa chama cha (TANU) kabla na baada ya uhuru
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  RIP Bhoke Munanka, Mungu amuweke mahali pema, lakini ukweli lazima kusemwa, ninamjua sana huyu mkulu maana aliwahi kuwa jirani mitaa ya Ocean Road na Luthuli.

  Kama ni ufisadi Tanzania, huyu ndiye aliyeuanza wengine wanafuatia tu, kina Rostam na Lowassa ni cha mtoto kwa huyu, unajua at one time huyu mkulu alikuwa na kazi flani ya uthibiti wa mali za serikali under Mwalimu, yaani serikali ikitaka kununua anything big nje, ilikuwa lazima yeye ndiye aende kuhakiki kwanza ndio serikali ikubali kutoa mapesa yetu walipa kodi,

  I mean, talking about ufisadi huyu ndiye hasa aliyeuanzisha, lakini anyways Mungu amuweke mahali pema peponi!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  FMES,
  With all due respect, Mzee Munanka ilibidi aache kazi serikalini alipoanzisha biashara ya kuingiza malori ya SCANIA. For that I will always respect him. Hakuchanganya biashara na siasa. Hata ubunge wa Tarime aliachia ngazi. RIP
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Field Marshall Es,
  Mkuu tafadhali haya matusi tena mkuu..
  Huyu ni mzee wetu na tunamfahamu sana kwamba hakuwa na kitu kiasi cha kumweka ktk kundi la kina Lowassa na Rostam. Bokhe hakuwa na nguvu ya Ufisadi hata kidogo na watoto wake wali struggle kimaisha kama watoto wa watu wengine, na kama walipewa kitu basi hakuna kiongozi ambaye hakufanya hivyo kulingana na sheria.
  Kweli alikuwa na mapunghufu yake ya kibinadamu, hakuna jhaja ya kuorodhesha hasa baada ya kufa na pengine huko kwao amebeba lawama nyingi zaidi kwa sababu alihama kabisa na kutafuta makazi mapya!...jambo ambalo sii hatramu hata kidogo ndio matunda ya UHURU.
  Mungu amweke mahala pema peponi, tupo pamoja na familia yake ktk maombolezi!
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Jul 26, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280


  Mkuu,

  Hapo ndiko kumkoma nyani maanake huwa sometimes nachoshwa na watu wanaosifia marehemu hata kama alifanya mabaya.Ndiyo unafiki unaowafanya watenda maovu waendeleze uovu kwani wamajua wakifa wataitwa wasafi.

  Safi sana mkuu.

  Btw. Apumzike kwa amani
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ben,
  Samahani sana UNAFIKI ni kumsema mtu kisha kufa, alipokuwa hai mlikuwa wapi?
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Ni kweli, ila kwa case hii si kwamba FMES amezungumza sasa kwa sababu alishindwa kufanya hivyo kabla kutokana na jamaa kuwa hai.
  .
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Nyie wakuu acheni hizo, unasema hakuwa na kitu na ile compound ambayo ndani ina nyumba zake na za watoto wake alziijengaje, ninarudia tena kuwa huyu marehemu na Mungu amlaze mahali pema sana ndio hasa chanzo cha ufisadi bongo, kama zilimuishia ni sawa lakini alikuwa fisadi huyu tena namba moja!

  And I mean it, na ninamuombea kwa Mungu, lakini huyu ndiye hasa fisadi original! Hawa wote kina Rostam cha mtoto kwa huyu!
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Alianzishaje hiyo biashara tena enzi zile? Huyu na Mzee Tabu Mangara walikuwa kundi moja na Chief Fundikira (RIP) wote mafisadi wasiokuwa na uwezo mkubwa wa kuona mbali ndio maana waka-invest vibaya zikawaishia kabla hawajafa, lakini ni mafisadi anyways na Mungu awaweke mahali pema peponi na tuko na familia zao pia wakati huu mgumu wa maombolezo!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Nimemtaja huyu fisadi kwenye kila topic ya Mwalimu na his chosen's, huyu ndiye aliyekuwa mtoto hasa wa Mwalimu, na ni mmoja kati ya viongozi wachahce under Mwalimu walioruhusiwa kufanya anything, ukienda kwenye topic zote za Mwalimu, kuanzia BCS, nimemtaja sana huyu marehemu, kuwa ni fisadi namba moja na I stand behind my words kuwa ndio tunaomboleza lakini the man was fisadi period!
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Jul 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,767
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Jasusi,FMES,Mkandara,

  ..hivi huyu Mzee fedha na mali zote zile alikuwa anatoa wapi?

  ..wananchi tulikuwa na hali mbaya sana kimaisha lakini Munanka alionekana kutajirika bila ya kuwa na biashara zake hazieleweki.

  ..hoja kwamba watoto wake walikuwa wakisota haina msingi. some families are just like that.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Field Marshall Es,
  Wakati wa Nyerere haikukatazwa kuingia magari makubwa nchini.. mfumo wa siasa yetu uliweka vipaumbele hasa ktk magari makubwa ya mizito, usafiri na Matrekta lakini ni Watanzania wachache sana waliokuwa na access ktk mawasiliano na mashirika ya Nje. Wengine walishindwa kabisa kufikiria inawezekana Elimu ya biashara pia ilikuwa ndogo kutokana na kuelewa vibaya siasa ya Ujamaa.
  Huyu mzee alikuwa na uwezo huo pia aliweza ku excute.. Wengi kati yetu tunapanga kila siku kufanya biashara hii ama ile lakini tunashindwa kufuatilia, ni wale tu ambao wanawezxa kuchukua risk ktk vitu walivyovifanyia Physical study ndio hufanikiwa..
  Wapo watu wengi sana waliofanikiwa wakati wa Ujamaa (Nyerere) kwa kuchukua risk ambazo kwanza walitazama soko kisha sheria zilizokuwepo.. Nyie Mabaharia na ujanja wenu wote mlikuwa kituletea Daladala, nguo, raba na santuri za kina Michael Jackosn badala ya kufikiria biashara zenye manufaa chini ya mfumo wa kijamaa..
  Taratibu za biashara kidunia bado kabisa hazijabadilika ila mifumo ndiyo imekuwa wazi zaidi..hata wewe leo hii unaweza kuingiza kampuni kubwa nchini kusambaza Matrekta na huna uwezo mkubwa isipokuwa uwezo wa kuongea (communicate) ktk lugha ya biashara..Kina Bakhresa walitumia nafasi hizo kujinyanyua toka ushona viatu hadi kuwa wajasiriamali wenye uwezo mkubwa..
  Sasa unapojaribu kufikiria ile faida aloipata kutokana na biashara ya kuingiza ma Scania nchini na kuijengea hoja wakati yeye hakuwa tena kiongozi serikalini ukaja mlinganisha na kina Lowassa na Rostam ni matusi mkuu..Wee nambie ni sheria gani alovunja ktk shughuli zake kama tunavyowazungumzia kina Lowassa na Rostma.
  Nitarudia kusema unazungumza vitu kutokana na matokeo ya kazi ngumu aliyoifanya mzee huyu...
  Just imagine Tanzania ya Nyerere bila maroli ya Scania nchini...tungeendelea kuwa na malori na Reyland au Coma ambayo leo hii sijui kama yapo duniani na vipuri vyake ktk soko la magari makubwa.. Tanzania ingekuwa sawa na Cuba!
   
 13. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Amen
  Poleni sana wafiwa, Mungu awape faraja wakati huu wa Majonzi.

  Ninaomba mwenye picha yake atuwekee maana nilikuwa simfahamu.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hujaeleza alifanya vipi ufisadi katika kazi yake ya kudhibiti kazi za Serikali.

  Anyway, ninaloweza kusema ni kwamba Munanka na kina Rupia (Senior) ni baadhi ya matajiri wazalendo waliokuwa wamemzunguka Nyerere enzi zile. Wakati wa taifisha taifisha, ambapo kuna wengi walinyang'anywa mali zao, hawa watu nasikia walipeteshwa, ikiwa ni pamoja na majumba ya Rupia Kariakoo.

  Kama ni kweli -na mazingira yanaonyesha ni kweli -basi that's another blemish on the storied record of the "principled" Great Leader.
   
 15. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  munanka,alikuwa secretary,katika serikali ya mkoloni,hence alimwibia siri nyingi nyerere,hence nyerere aliweza always kuwa one step ahead of the colonial authorities.risks involved ilikuwa kubwa sana,as a result after independence huyu mtu was rewarded well,na katika process akawa untouchable
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jul 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,767
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  FMES,Mkandara,Jasusi,..

  ..huo utaratibu wa kuagiza mascania ulitokea wapi?

  ..ninavyoelewa wakati ule serikali ilikuwa haitumii middlemen ktk zabuni na manunuzi.

  ..pia makampuni ya usafirishaji[kamata,kauru,kaudo,...] yalikuwa ni mali ya serikali.

  ..hayo mascania aliyokuwa akiagiza wateja wake walikuwa ni kina nani?

  ..pi tulianzisha kiwanda chetu cha ku-assemble mascania pale kibaha kwa msaada wa Sweden. hivi mlitegemea ktk mazingira yale turuhusu wachuuzi binafsi wa scania.

  ..halafu huo mtaji wa biashara kubwa namna hiyo aliutoa wapi na yeye alikuwa mwanasiasa?
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe unadhani tumesahau kuhusu ile meli ilozama Ziwa Victoria kwa sababu ilikuwa ni meli maalumu kwaajiri ya mito lakini yeye Bhoke alikula fweza na kuruhusu inunuliwe na kutumika Ziwani??????

  Watu kibao walikufa na yeye Bhoke hata hakuguswa, walioguswa ni wale walio ikagua meli mwaka mmoja nyuma na kuipa kibali cha kuendelea kufanya kazi.

  Kama watoto wake wame na wana struggle kama watu wengine hiyo haiwezi kumzuia yeye kuwa Mtangulizi wa Mafisadi, ila inawaonyesha wazi mafisadi wa leo kwamba wanawachimbia mashimo ya Volkeno watoto wao. Fedha walizo iba zitakwisha wakiwa bado hai. Mungu awazishie maisha Mafisadi wote ili wapate kuuona uovu wao ukiwasambaratisha wao na vilembwe wao.

  Kuupuuza ushauri wa kitaalamu kwa makusudi ili kujaza mifuko yao mapesa ni Mapungufu ya kibinadamu??

  Give me a break!!
   
 18. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  correct me if i am wrong,me i thought ile meli ililetwa enzi ya mkoloni.sadly though i lost an uncle whose body was never found
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Jul 26, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,767
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  son of alaska,

  ..kwanza pole sana kwa kupoteza ndugu yako ktk ajali ya ziwa Victoria.

  ..umeshaelezwa hapo kwamba meli ile ililetwa baada ya uhuru na wahusika wanajulikana.

  ..tena kuna tetesi kwamba usafirishaji wake toka Dar kwenda Mwanza uliharibu barabara ya kwenda Mwanza.
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Unajua wakuu ni vyema mkarudi nyuma kujifunza historia ya siasa ya taifa letu, kwa sababu unajuaje tunakokwenda kama hujui tulikotoka? No wonder hapa JF kuna watu hamuishi ubishi bila hoja za msingi, I mean hebu niambie kati ya ndege zote za serikali na ATC under utawala wa Mwalimu, tulizonunua iliwahi kuwa nzima au mpya? Hebu niambie ni meli ipi kati ya zote tulizonunua under Mwalimu ilikuwa nzima au mpya?

  Hivi wewe kweli ulikuwa hata unajua kuwa kuna mtu kwenye serikali ya Mwalimu, alikuwa na cheo cha huyu marehemu? Eti mthibiti wa mali za serikali, kazi gani hiyo? Kwa ni hakukuwa na General Auditor Mzee Aboud? Filimbi nyingi hata historia ya taifa lako mwenyewe huijui? Wewe unamjua Bhoke Munankha au unamsikia? Kuna fisadi wa kumzidi huyu?

  Kwa kweli wakuu I am not so sorry on this, hawa viongozi wetu ni uamuzi wao kuchagua avenue watakazozipita sasa hivi wakiwa hai, ndani ya uongozi wa taifa letu, sasa wakichagua njia za ufisadi shauri yao sisi hautabadili historia ya siasa yetu eti kwa sababu sasa umekufa, no way fisadi ni fisadi, tutasema tena kwa nuguvu sana ili mafisadi waliobaki wajue wazi kuwa hakuna kuziba wala kukufichia uozo wako hapa, I am a Christian na ninaiminia sana Biblia kuwa kila neno ndani yake ni la Mungu, sasa kama Mungu kule ametupa mifano ya watu wake waliokuwa wazuri na waovu, unataka mimi leo nifanye nini? Nimsifie fisadi eti kwa sababu ya msiba?

  Huyu marehemu Munankha ndiye hasa chanzo cha ufisadi bongo!
   
Loading...