Beware... It's not me! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beware... It's not me!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Mar 4, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kuna mdau mmoja anajiita zikchvieck motseck na Email yake ni <motseck@gmail.com> akiwa anatuma ujumbe huu:Asanteni sana kwa kuniunga mkono na jamboforums.com

  Na dhamira yake SI NJEMA hata kidogo japo ujumbe ulioambatana na kichwa hicho cha habari ni huu:

  Tafadhali someni maandishi yake na angalieni document ambayo iko attached inasema IMETOKA kwa nani. Ni wazi ni mwanamke na picha aliyoambatanisha SI YANGU.

  Nasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza kwa wote watakaokumbana na barua pepe hiyo ambayo imeanza kusambazwa na mtu huyu tangia tarehe 27 Februari.

  Nasisitiza, si mimi! Ni rahisi kwenu kumjua mhusika wa kitu hiki ambaye naamini anafanya kwa nia ya kumponza mtu ama kunifanya nionekane kama ninayetafuta sifa ama umaarufu kirahisi.

  Pls ignore the message and beware that such Tanzanians exist.

  Ahsanteni

  NOTE:
  Angalia muda nilioandikia ujumbe huu, na ukipata barua pepe yake angalia alichoandika na oanisha na niandikacho. Simlaumu; ni kazi ya 'wale' imeanza rasmi dhidi yangu
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante invisible kwa kuweka hili wazi... naona hawa hawataki kuacha hujuma zao ila MUNGU yupo tu tutawaumbua kila wakati wakijitokeza.
   
 3. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Invi... Mkuu, tupo pamoja!!! Asante kwa kutupa heads up!!!!

  Kaaz kweli kweli na watachonga saaana juu yako na yetu (JamboFurums) lakini wataishia patupuuuuu!!!

  Aluta Continua!!
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hapa kama wanaamini kuwa kuna siku wataweza kupambana na nguvu ya umma wajue tuu kuwa wameliwa vibaya sana .

  Wakumbuke tuu kuwa what goes around comes around.......
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Imenisikitisha lakini natambua kuwa ni mapambano na nguvu za giza. Kuna siku zitashindwa.

  Labda nitoe RAI yangu hapa:

  Hata kama natumia jina la "Invisible" sina ubaya na serikali ya Tanzania. Naipenda nchi yangu, nawapenda watanzania. Nakubaliana na ukweli kuwa tupo ulimwengu wa tatu na tunajitahidi (serikali yetu) kupambana na kila aina ya adui wa maendeleo ya taifa letu. Maradhi, Ujinga na Umasikini vinatakiwa vipigwe vita vikali sana.

  Kinachofanyika JF si kupambana na serikali bali kuipa serikali ushirikiano katika kupambana na maadui hawa. Ndio maana JF ni mjumuisho wa majukwaa mengi (si siasa tu) kwa ajili ya kuleta mijadala endelevu ya namna ya kuinua maisha ya watanzania.

  Suala la UFISADI lisiwe kigezo cha kudai JF imeanzishwa ili kupambana nacho; ni adui mmojawapo ambaye tumekumbana naye safarini na si rahisi kumwacha akiwa hai, anapigwa vita 'vitakatifu' ili kuhakikisha anakufa kabisa.

  Kamwe, jina langu ama la rafiki yangu ama la mzazi wangu ama la mwanachama wangu (wa JF) lisitumike kama kigezo cha kutafuta mchawi. Taifa hili ni letu sote na kwa pamoja tuna wajibu wa kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania na vizazi vijavyo yanawezekana. Unafiki, uzandiki, kebehi na hulka za kuchafuliana majina hazitotupeleka popote. Badala ya kupoteza muda katika kufanya hayo tuangalie namna ya kuinua maisha ya watanzania wenzetu na walimwengu kwa ujumla kwa kutumia akili zetu, uwezo wetu kifedha na mali katika kuliokoa taifa.

  Nilichoweza ni kusaidia kuwepo kwa mijadala endelevu kwa njia ya mtandao na nikasaidia kuwepo kwa fursa hiyo na kuitoa kwa watanzania. Dhamira yaweza kuwa njema na ikaharibiwa na wachache, siwalaumu kwakuwa hatufanani mitizamo.

  Nilishasema na nitaendelea kusema: JF ipo kwa ajili ya watanzania wote ikiendeshwa na watanzania. Kamwe sintothubutu kukubali taifa langu lidhalilishwe kupitia JF. Na endapo wanachama mtaona penye kuwa na mapungufu kiungwana tufahamisheni nasi tutashughulikia.

  Nikiwasiliana na wanachama ama yeyote kwa masuala ya JF LAZIMA nitumie <invisible@jamboforums.com> au <webmaster@jamboforums.com> na si vinginevyo.

  Ahsanteni
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Binafsi sijapata kuiona hiyo mail. Tunashukuru kwa taarifa hiyo, tutachukua tahadhari.
   
 7. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Invisible:
  You said it very well. Serikali ya Tanzania au CCM sio adui wa JF.
  Adui ni viongozi wabovu, wala rushwa, waonevu kwa wananchi, mafisadi n.k.

  Kama watu wenye sifa hizo wamo CCM, serikalini, katika vyama vya upinzani, au katika vyombo vya kuwatumikia wananchi, kama polisi, magereza, mashirika, ni haki yetu kuwashambulia kwa nguvu zote.

  The only sacred cow, ni Tanzania yetu sote.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Huyu ndiye Ndugu Hasara [our hero I may say] ambaye alipewa laptop kama zawadi na mtu ambaye alimwamini na ndiyo anayoitumia kuandika mambo haya. Kwa yeyote ambaye ni mwanachama wa JF ni rahisi kusoma between the lines na kujua kuwa ujumbe huu ni wa nani na dhamira yake ni nini. Nimeonelea ni vema niwajulisheni juu ya ujumbe huu ili mkiupata isijekuwa tabu kunilazimu nitoe statement zaidi ya hii.

  Mwenye kumsaidia hiyo pc amesikitika kujua msaada wake umetumika hivi. Kumradhi kwa wote endapo kutakuwa na usumbufu wa aina yoyote kutokana na barua pepe hiyo.

  Ahsanteni na nawatakia mijadala myema.
   
 9. green29

  green29 JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Inasikitika sana... ni rahisi kusoma the motive behind this dusty brain!
   
 10. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hasira HASARA

  Huu jamaa hajui kuwa anaendelea kuisadia kuitangaza jambo forums kwa ushambenga wake

  Asha
   
 11. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  KAWEKA PICHA AMBAYO IMETENGENEZWA NA PHOTOSHOP

  Kazini Kwangu Ni Hapa kampuni ( KAANDIKA JINA LA KAMPUNI) Muda Wa Kazi 8.00 Am- 3.00pm

  KAANDIKA JINA LA MTU
  KAANDIKA CHEO CHA MTU
  KAANDIKA JINA LA KAMPUNI
  P.O.Box KAANDIKA ANUANI YA MTU,
  Dar es Salaam -Tanzania
  Namba ya simu :- KAANDIKA NAMBA YA MTU


  Mimi Ndiyo Invisible Mwenywe mmiliki wa jamboforums.com

  Ukiwa na mikataba mibovu niletee, kwenye anuani hapo juu habari chafuchafu za watu, viongozi matajiri mimi ndiye mwenyewe wa kuwarekebisha. Jamboforums.com itawakomesha. Serikali imejaribu imeshindwa Tanzania sasa tuna uhuru wa habari.jina langu ni invisible na sinta badilisha. Nitaweka uchunguzi wa BoT soon……

  IP na manjina yenu yapo salama.

  Karibuniu JF.

  Ninapatikana Hapa chuoni Jioni Kuazaia Saa Kumi Jioni ninachukua masoma ya jioni. Au wasiliana na mkuu wangu wa chuo atakupa info. Zangu au emai zangu hapo chini.

  Sambaza ujume huu kila mtu anijuwe nina vyo pigana na mafisadi Tanzania.

  KAWEKA ANUANI YA CHUO FLANI CHA DAR ES SALAAM

  E-mail : KAWEKA BARUA PEPE KADHAA AMBAZO HATA HIVYO ZILIKUWA ZINAJIRUDIARUDIA


  Mheshimiwa Invisible mi ningefarijika sana kama ungeweka hizo details alizotumia yani adresess na jina la kampuni, cheo chake,na namba ya simu na hiko chuo alichodai ndo anapatikana.. Nimesema hivi kwa sababu yawezekana kabisa wengi wetu humu ndani tusikutane na hiyo email.
  Thanx mods for keeping JF Alive.
  I salute u all
   
 12. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waache waandelee kututafuta. Sisi tupo na tutaendeleza mapambano ya kifkra hapa. Twajua mafisadi wanaplay part kubwa sana kwa kufund juhudi za hawa wanaojiita usalama wa taifa hili kutunyamazisha.Sisi tupo na mapambano haya yataendelea kama kawa.
   
 13. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Invisible
  Wazo la Waga ni sahihi kabisa. Kwa upande wangu sijapokea e-mail hiyo na hizi taarifa nimezipata hapa JF.Hebu tupe info kamili na hilo attached files kwanini usiliweke hapa ubaoni tulione. Hakuna haja ya kuficha,liweke hapa tulione na tujue hicho chuo na hiyo kampuni iliyuotajwa. This is serious. Please Invisible,let us know. Yeye kama ni usalama wa taifa,tunataka tumonyeshe hiyo kazi tunaiweza,mie nitamfuata hapo hapo nione atanifanya nini na nitajitambulishe kwa username na jina langu kamili nimuone atafanya nini.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiv huyu dogo ana matatizo gani? (sina haja ya kumtaja jina) mnaweza kumdharau na kumpuuza lakini wajinga kama hawa wanaweza kuleta madhara makubwa mbele huko.

  Sasa sina nia ya kumtisha mtu lakini nakwambia dogo Dar ni sehemu ndogo sana endelea na upuuzi wako halafu uone kitakachokupata and I mean it
   
 15. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,657
  Likes Received: 2,462
  Trophy Points: 280
  Kaka Masatu,

  taratibu kaka,wajita hatuna utamaduni wa kumuonya adui,bali ni swift action tu mtu anashika adabu yake.Well for the first time nimekuona kweli umekasirika for the interest of our beloved nation despite your diehard and conservative ushabiki na uanachama kwa CCM,kudos bro,tell the young man to stop the nonsense.
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Invisible,

  Sioni haja ya kuweka wazi hiyo kampuni na anwani au chuo, maana vinawezekana ni vya mwana JF ambaye yeye anaamini ni Invisible!, hivyo kukaweka identity ya huyo shujaa wazi. JF hatutaki ID za watu.

  Ficha ID zote alizotumia, ila mwambie cha moto kitamfikia sio muda mrefu akumbuke wafanyiziaji wanamjua na nyendo zake zinafahamika!
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Naam, JF si maadui wa SK wala CCM bali ni maadui wa mafisadi waliojiingiza kwa wingi ndani ya CCM na SK na kujivisha ngozi ya uongozi ili wakidhi nia yao ya kufanya ufisadi dhidi ya walipa kodi na kuzorotesha maendeleo ya Watanzania na wale wote ambao wanaojitahidi kwa njia moja au nyingine kuwalinda mafisadi hao.
   
 18. M

  Masatu JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Yamekuwa haya!
   
 19. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Hata wafanye nini wana wa JF kumkoma nyani ndio jadi yetu....hureeeeeeeeeeeeeeee
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...