Betty Machangu Vs Shally Raymond: Wanawake wa CCM wanaotoana macho kisa ubunge

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Nikisema ni mchuano wa kukata na shoka mwaka 2020 sitakosea kwa hawa wanawake wawili wa CCM mkoani Kilimanjaro,Betty machangu na Shally Raymond.

Bahati mbaya sana mchuano wao ni wa kishamba,mchuano wa kuchafuana,kila mmoja akitumia nguvu ya pesa na wapambe wake na kama CCM watakifanya hawaoni basi lolote laweza tokea hapo mwakani.

Itakumbukwa kuwa Betty Machangu mwaka 2010 alikamatwa na Takukuru kwenye moja ya Nyumba za kulala wageni mjini Moshi akiwa na baadhi ya viongozi wa UWT Moshi Vijijini wakiandaa mazingira ya kuwapa rushwa ili wafanikishe ushindi wa machangu.

Ndani ya Nyumba hiyo ya kulala wageni palikutwa bahasha zenye pesa zikiwa tayari zimeandikwa majina ya wajumbe wa UWT wenye maamuzi ya kuchangua pamoja na doti moja ya Kitenge kwa kila mjumbe.

Sasa unaambiwa bosi wa Takukuru badala ya kupongezwa akahamishwa,Betty Machangu hakufunguliwa mashitaka yoyote lakini taarifa zinapasha kuwa kuna ka mchezo kalichezwa na washindani wake ambao ndiyo waliomchoma kwa Takukuru.

Wakati tukiwa na muda mfupi kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani,juzi juzi wabaya wa Shally Raymond nao wakamchoma huko Takukuru,wakadai amemwaga sukari ya kutosha kwa wanawake wa UWT Moshi VIjijini,Takukuru wakatinga ulipo mzigo na wakaukuta kweli kweli na hata wajumbe walikuwepo tayari kupewa sukari yao.

Nani kasema CCM wanaweza kuumizana wenyewe kwa wenyewe?,tuhubutu yako,kibao kikageuzwa unaambiwa,mchezo ukachezwa sukari ile iliyokuwa isambazwe kwa kina mama wa UWT ili muda ukifika wapige kura ya ndiyo kwa Shally Raymond,sasa imepelekwa kwenye ile shule Kongwe ya Ashira ambayo hivi karibuni iliungua moto.

Lakini bado mambo yanaenda ndivyo sivyo kwa Shally Raymond,kwani wasbaya wake bado wamemshikia bango,wanadai sukari ili ilikuwa ni hongo kwa wajumbe wa UWT wilaya ya Moshi Vijijini,nani ataibuka mshindi ni suala la kusubiri na kuona.

Hiyo ndiyo CCM,anayebisha anyooshe mkono,afanye kama anajikuna
 
Just a tip of an iceberg

Namna ulivyosimulia ni kama vile hao Wajumbe wao ni Maroboti, wakiitiwa rushwa na yeyote wao jukumu lao ni kwenda tu kupokea, dili likibumburuka basi wanaondoka kurudi kwenye shuguli zao.

Hivi wao huwa hawawajibiki kwa lolote?
 
Back
Top Bottom