Betterment Fees ya kuendeleza Makongo Juu, kuna ufisadi unataka kutendeka hapa au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Betterment Fees ya kuendeleza Makongo Juu, kuna ufisadi unataka kutendeka hapa au?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kabila, Mar 12, 2012.

 1. K

  Kabila New Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jana nilikuwa kwenye kikao cha wananchi wa Makongo juu kuhusiana na kuendeleza Makongo juu ili liwe eneo la kisasa zaidi, viwanja kupangwa, barabara nzuri na za kisasa, maji na huduma za jamii.

  Cost nzima ya Project ni Tshs 24.7 Billion.

  Hii Project mwanzoni nillisikia kuwa itakuwa funded na World Bank. Sijasikia kama serikali itatoa fungu lolote mpaka sasa hivi. Halmashauri ya Kinondoni watatoa 500M kwaajili ya barabara.


  Sasa Mimi naona kuna ufisadi unataka kufanyika hapa kwasababu pendekezo mojawapo ni kwamba wananchi tulio na maeneo kule tulipie "Betterment Fee" kiasi cha Tsh 5,500 kwa sq metre ambayo roughly kama una eka 1 itakucost atleast Tsh 26M. Hii ni hela nyingi sana kulipia eneo langu katika muda huu ambao hali ya maisha iko juu sana. Plus ninalipa kodi nyingine nyingi tu.

  Kwa harakaharaka wamepiga mahesabu wameona kuwa watu wote tukilipa "Betterment Fee" jumla itakusanywa Tsh 25 Billion.

  Ufisadi ninaouona mimi ni kwamba:

  1. Kama kutakuwa na hela nyingine yeyote kutoka serikalini au WorlBank wajanja watakula.
  2. Kama mwananchi atashindwa kulipia eneo lake serikali italichukua (hapa wajanja watauziana kwa bei ndogo zaidi) ---> Hii ni statement ya Waziri wa Ardhi na Makazi ambaye naye ni Mkazi wa Makongo.
  3. Tumeambiawa kuwa kama eneo likibomolewa kupisha barabara utalipwa Tsh 800 kwa sq metre (ofcourse wananchi wamepinga sana hii, sasa sijui kama itafanyiwa kazi).

  NB:
  Kuna kamati inayowakilisha wananchi wa makongo ambayo imependekeza kuwa hii Betterment Fees isiwepo sasa sijui kama itasikilizwa.

  Sijui mtazamo wenu wana JF katika hii
   
Loading...