Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 27,102
- 39,279
Hello members,
Ni kipindi sijakutana nanyi tena ndugu zangu wa MMU natumai mu wazima.
Leo nimekuja na kisa nilichoshuhudia kilichonifanya niandike uzi Huu Siku ya Leo tukielekea valentine day.
Kichwa cha uzi kinasema kwa kimombo “better to return home from a failed marriage than coming back home in a coffin”
Kwa tafsiri sisisi tunaweza kusema “Ni bora zaidi kurudi nyumbani kutoka Ktk ndoa iliyokushinda kuliko kurudi nyumbani ndani ya jeneza”
Huu ni msemo maarufu wa mwanafalsafa fulani wa kizungu.
Kisa kilichopelekea kuandika haya ni tukio la kweli la hivi karibuni la msichana mrembo kuuwawa na mumewe na wazazi kupelekewa mwili wa mtoto wao kwenye jeneza.
Baada ya kufwatilia kisa na mikasa ya ndoa Yao tulibaini msichana alivumilia ukatili usiomithilika toka kwa mwenziwe uliopolekea mauti yake.
Kwanini kuvumilia yote hayo? Kwanini kuficha yote hayo?
Kisa cha msichana huyu kinaakisi maisha yetu wengi tunayopitia humu ndani. Kisa hiki kinawakilisha mlolongo wa madhila yanayotupata wengi ktk mahusiano na tunaamua kuyafumbia macho.
Hebu tutafakari ni uchungu na hasara ya namna gani tunaachia wazazi na jamaa zetu.
Sio aibu kurudi nyumbani kuanza upya ukiwa na tumaini jipya kuliko kurudi ndani ya jeneza.
Nawatakia heri ya siku ya wapendanao.