Best Quote: "Hata ingekuwa JM ningemtosa"

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,033
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,033 280
Nadhani hii itabakia kuwa ni kauli ya kijasiri zaidi na ambayo imeonesha uzito mkubwa. Hongera mama Malecela kwa kuweka maslahi ya TAifa mbele.

Mama Malecela aliyasema hayo akidai kuwa hakuna mtu aliyeoonewa na hawa wote ni marafiki zake lakini kwenye Taifa hana urafiki.
 
M

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2006
Messages
752
Likes
22
Points
35
M

Mafuchila

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2006
752 22 35
Big up iron lady...
 
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,707
Likes
267
Points
180
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,707 267 180
Pengine naye anaitafuta umaarufu kupitia kwa PM mwathirika, Siasa bwana !!!!!
 
Steve Dii

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2007
Messages
6,419
Likes
81
Points
145
Steve Dii

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2007
6,419 81 145
Pengine naye anaitafuta umaarufu kupitia kwa PM mwathirika, Siasa bwana !!!!!
True true true, You never know katika siasa, si uliona aliyosema Mzindakaya "BoT safi"....., but I hope not for huyu mama, ameonesha msimamo mzuri sana mpaka hivi sasa! She simply rocks!

SteveD.
 
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,232
Likes
91
Points
145
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,232 91 145
Huyu mama kwa kweli nampongeza kwa kauli zake za hivi karibuni

...hongera sana Mama

Hivi Mkuu Kitila Mkumbo yuko wapiii??,........nazi-miss analysis zake za upande wa pili hasa ikifikia kwenye matukio ndani ya siasa
 
K

Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,143
Likes
506
Points
180
K

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,143 506 180
Huyo mama nimemfuatilia kwa muda kidogo na mpaka sasa i can count on her lakini isije ikawa big talk and do nothing,time will tell!
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,033
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,033 280
Jamani angalieni nukuu mbalimbali kufuatana na sakata hili ili tuweze kuziweka hapa kama kumbukumbu.

Leo hii vijana wa chuo kikuu waliandamana kidogo wakifurahia kujiuzulu kwa wakubwa hawa!

Kijana mmoja amenipa msemo ambao sikuwahi kuusikia:

Alisema: "Ncha ya mkuki haipigwi konzi" na akaongeza kusema "Nyuki hakutambatiwi"...

Nilifurahia...
 
Rufiji

Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2006
Messages
1,754
Likes
263
Points
180
Rufiji

Rufiji

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2006
1,754 263 180
Mwanakijiji,

Vipi kuhusu ile line ya Spika kwa Karamagi. Manake Karamagi alisema watakuja hapa kushangilia , spika akamjibu kushangilia Tanzania sio kosa !

Mimi nimemkubali huyu Mama kwani kweli Amemkoma Nyani Giladi , ameweza kusimama na kuzungumza mambo kwa ufasaha mkubwa na zaidi aliweza kujenga hoja zilizoenda shule ! Nilipenda pale aliposema hawa watu sio wa hawajaonewa na huku akionyesha kopi nne za barua toka kwa waziri mkuu kwenda kwa Karamagi kumongoza nini cha kufanya kuhusu hilo deal la Richmond
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,033
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,033 280
Rufiji sikuisikia hiyo.. but that is one of the best line..
 
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2007
Messages
5,194
Likes
17
Points
0
M

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2007
5,194 17 0
Nadhani hii itabakia kuwa ni kauli ya kijasiri zaidi na ambayo imeonesha uzito mkubwa. Hongera mama Malecela kwa kuweka maslahi ya TAifa mbele.

Mama Malecela aliyasema hayo akidai kuwa hakuna mtu aliyeoonewa na hawa wote ni marafiki zake lakini kwenye Taifa hana urafiki.
Hongera mama Malecela!
 
Icadon

Icadon

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2007
Messages
3,589
Likes
29
Points
0
Icadon

Icadon

JF-Expert Member
Joined Mar 21, 2007
3,589 29 0
Jamani angalieni nukuu mbalimbali kufuatana na sakata hili ili tuweze kuziweka hapa kama kumbukumbu.

Leo hii vijana wa chuo kikuu waliandamana kidogo wakifurahia kujiuzulu kwa wakubwa hawa!

Kijana mmoja amenipa msemo ambao sikuwahi kuusikia:

Alisema: "Ncha ya mkuki haipigwi konzi" na akaongeza kusema "Nyuki hakutambatiwi"...

Nilifurahia...
"tatizo ni uaziri mkuu.Kwamba ionenekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe."
"ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu." Edward Lowassa

"Naamini mnapata maombi ya mchungaji Rwakatare, unaongea kama una nguvu za Mungu" Samwel Sitta
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
92
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 92 0
"ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu." Edward Lowassa
Just Go in peace brother, next time ukitaka haki fikiria utaratibu wa kuwaibia wananchi na kuwanyima umeme wakaishia kulala giza, huku ukisingizia uchumi unapaa na kuwapa wanyonge masikio ya kasungura na wakati nyama yote umeshika wewe na kina Karamagi na the likes, malipo ni hapa hapa, maana sasa utakuwa na hela ambazo haziiingiii, ila zinatoka tu maana zilikuwa zinaingia kutokana na power, huna tena!

Ila please usisahau kuwa God is still alive, sijui kama ulikuwa unalijua hilo

Jut go!
 
E

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2007
Messages
461
Likes
3
Points
0
E

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2007
461 3 0
.........hebu tuleteeni TAPE RECORDING YA EL alivyokuwa akijitetea pale DODOMA.
 
W

watu wewe

Member
Joined
May 20, 2006
Messages
39
Likes
0
Points
0
W

watu wewe

Member
Joined May 20, 2006
39 0 0
Mh. Spika nimetafakari kwa kina sana jambo hili, nikajiuliza kulikoni mpaka watu wazima wakakaa na kuamua kufanya haya…nimetafakari sana na kugundua haya yote ni Uwaziri Mkuu…it is their wish which am going to grant…Mh. Spika nimetafakari sana jana usiku juu ya jambo hili, nimeamua kumuandikia Mh. Rais barua ya kujiuzulu….!” Mh. Edward Lowassa

“Yesu hakutenda dhambi lakini alihukumiwa..” Karamagi

“Siogopi kuwajibika kwa maana hiyo…lakini mkimsingi mimi ni mtu ninayeheshimu uwajibikaji…namuomba Rais kujiuzulu…” Dk. Msabaha

“Karamagi ni rafiki yangu, Msabaha ni rafiki yangu, lakini katika hili sina urafiki na mtu, hata angekua Malecela (mumewe)……”, Mh. Mama Anna Kilango (CCM).

“Richmond ni wahuni tu, ina kiofisi cha Internet tu pale karibu na hoteli yangu ya Keys Hoteli, siju Serikali iliwaokota wapi wahuni hawa…,katika nchi kama China, watu hawa sio tu wanajiuzulu, wananyongwa hadharani…” Mh. Ndesamburo (CHADEMA).
 
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Messages
249
Likes
4
Points
0
F

FDR Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2007
249 4 0
Big up iron lady...
Thubutu yako ,Iron Lady ? huyo wa kwako wewe lakini kwetu sisi haingii ktk reokdi za kujifagilia kijingajinga tu bungeni.

A serious person hawezi kunyamaza kimya kwa kutishiwa eti asijihusishe na Richmonduli. Jana anasema eti aliitwa na kutishwa!!!!!

Shame.

Hafai kuwa hata mkuu wa wil;aya
 
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,232
Likes
91
Points
145
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,232 91 145
``Tusiwaachie akina Kabwe tu kuwakosoa viongozi wabovu serikalini, bali tuungane bila kujali vyama na kulifanya bunge kuwa mtetezi mkubwa wa wananchi,``

..........hayo maneno mazito na ya kutia moyo sana toka kwa huyu Mama.......hongera mama keep it up!!
 
U

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2007
Messages
317
Likes
53
Points
35
U

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2007
317 53 35
Hii hapa chini nadhani ni kiboko. Je kweli alisema JK haya? maana imeingia ktk PM yangu leo.

Hotuba ya Rais Kikwete

Leo asubuhi nimepokea barua ya Waziri Mkuu ya kujiuzulu kwa masikitiko makubwa kwani tumefanya naye kazi muda mrefu na nilitegemea atumie vipaji vyake vingi kuongoza serikali yangu kwa muda mrefu. Wengi mtakumbuka enzi za Boyz2Men. Nasikitika sana kwa hatua taifa letu lilipofikia.

Aidha, nimepokea na kusoma ripoti ya Dr Mwakyembe kwa masikitiko maradufu ya yale yaliyonipata kwa barua ya ndugu Lowassa. Sina mengi ya kusema, ila jioni hii naomba wananchi mnipe ridhaa yenu kuanza mchakato wa kina wa kuondoa taifa hili kwenye dimbwi la ufisadi, ubadhirifu, wizi, utawala wa ki-imla, na kutojali matakwa na malalamiko ya wananchi.

Awali ya yote nikiri kwamba kwa miaka yote niliyokuwa kwenye shughuli na uongozi wa uma, lazma kuna nyakati chache ambazo nami niliwahi kuterereka kimaadili. Pale matendo yangu hayakukidhi mategemeo ya wananchi naomba msamaha wao. Hata hivyo inafika wakati nchi kusafishwa kwa manufaa ya umma. Bila hivyo nchi yetu itasambaratika kama majirani zetu na nchi nyingine kama USSR, Yugoslavia nk. Nimenuia kuiokoa nchi yetu toka kwenye hatma hii, na kwa hili nitaomba na kuhitaji msaada wenu. Hatua za awali.

Kwanza, nakataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kama hakuandamani na kujiuzulu kwa baraza lote la Mawaziri ili nianze upya kuomba kibali cha kuwaongoza wananchi bila fununu za ufisadi na bila dharau kwa serikali yao.

Pili, natangaza kugandisha (to freeze) akaunti zote za mali za wale waliohusika na shutuma za Richmond, na BoT, pamoja na kushika rehani mali zao zote zisizohamishika kwa nia ya kurudishia serikali mali yoote ambayo inaweza kuwa iliibiwa na washutumiwa. Ili wasife njaa serikali itaendelea kuwalipa nusu mshahara hadi uchunguzi au mashtaka kumalizika.

Tatu, nawahimiza viongozi wote waliojihusisha na ufisadi wowote wa kimsingi kama kwenye mikataba ya madini, Netgroup Solutions, Uuzaji wa Mashirika na Raslimali za Umma, Ununuzi wa rada na ndege ya Rais, Ununuzi wa vifaa vya Jeshi, Mikataba na TANESCO kama IPTL, Kiwira, nk, wakiri kwangu kimaandishi kushiriki kwao na kuorodhesha mali walizopata kutokana na matendo hayo. Wakifanya hivyo sitawachukulia hatua za kisheria ila nitawasimamisha kazi ya umma na kurudisha mali ya wananchi panapohusika.

Wasiojitokeza kwa hiari naagiza vyombo vyote vya uchunguzi vya dola kufuatilia kwa undani na waletwe mbele ya sheria mara moja.

Ndugu wananchi, hii vita dhidi ya wabadhirifu itahitaji ushirikiano wenu na naomba mniunge mkono kwa kila namna.
Nimeagiza vyombo husika kuhakikisha watuhumiwa hawawezi kutoroka au kutorosha mali hadi uchunguzi umalizike. Aidha nimeagiza vyombo vya dola viwe macho kudhibiti wakorofi wachache watakojaribu kuleta ghasia.

Mungu ibariki Tanzania.

Asanteni.

(Anavua miwani, anafuatwa kwenye jukwaa na Makamu wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Chadema, CUF, UDP na kuzingirwa na Chief Justice, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Polisi na Mkuu wa Magereza. Wanatoka nje ya Bunge kwa hatua kakamavu za kijeshi. Wabunge wanasimama na kumshangilia kwa nderemo na vifujo)!!!!!!

Hii kazi kweli kweli. Watu ni lazima wajisalimishe.
 
T

TechMaro

Senior Member
Joined
Feb 8, 2008
Messages
102
Likes
0
Points
33
T

TechMaro

Senior Member
Joined Feb 8, 2008
102 0 33
Duh hiyo hotuba umeitoa wapi???

Kuhusu Mama Malecela, so far she is brave and bold, big up sana.
Tanzania inawahitaji watu kama hao, na najua ataendelea kuwa hivyo.
Kwa wanaosema ni usanii, shauri yao, by the way, amesaidia kuwaamsha wabunge wa sisiem waliokuwa wanakubali kufanywa mandondocha, that's a great service to the nation.
Naamini ataendelea na ujasiri huo....
Nilichojifunza kutokana na ujasiri wake ni kwamba, Tanzania ya sasa haitasimama kwa kumtegemea mtu mmoja. Ona Boyz2Men walivyotuangusha, hata baada ya kuwaamini sana awali. Yeye ametoka kama mkombozi wa wanyonge na akasimama kidete. Siku akibadilika na kuanza kukumbatia maslahi binafsi(ni mfano tu mama, sio kukubeza), nina uhakika watakuja wengine ambao watamkomboa mtanzania.
Naomba kuwakilisha.
 
W

watu wewe

Member
Joined
May 20, 2006
Messages
39
Likes
0
Points
0
W

watu wewe

Member
Joined May 20, 2006
39 0 0
Hii hapa chini nadhani ni kiboko. Je kweli alisema JK haya? maana imeingia ktk PM yangu leo.

Hotuba ya Rais Kikwete

Leo asubuhi nimepokea barua ya Waziri Mkuu ya kujiuzulu kwa masikitiko makubwa kwani tumefanya naye kazi muda mrefu na nilitegemea atumie vipaji vyake vingi kuongoza serikali yangu kwa muda mrefu. Wengi mtakumbuka enzi za Boyz2Men. Nasikitika sana kwa hatua taifa letu lilipofikia.

Aidha, nimepokea na kusoma ripoti ya Dr Mwakyembe kwa masikitiko maradufu ya yale yaliyonipata kwa barua ya ndugu Lowassa. Sina mengi ya kusema, ila jioni hii naomba wananchi mnipe ridhaa yenu kuanza mchakato wa kina wa kuondoa taifa hili kwenye dimbwi la ufisadi, ubadhirifu, wizi, utawala wa ki-imla, na kutojali matakwa na malalamiko ya wananchi.

Awali ya yote nikiri kwamba kwa miaka yote niliyokuwa kwenye shughuli na uongozi wa uma, lazma kuna nyakati chache ambazo nami niliwahi kuterereka kimaadili. Pale matendo yangu hayakukidhi mategemeo ya wananchi naomba msamaha wao. Hata hivyo inafika wakati nchi kusafishwa kwa manufaa ya umma. Bila hivyo nchi yetu itasambaratika kama majirani zetu na nchi nyingine kama USSR, Yugoslavia nk. Nimenuia kuiokoa nchi yetu toka kwenye hatma hii, na kwa hili nitaomba na kuhitaji msaada wenu. Hatua za awali.

Kwanza, nakataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kama hakuandamani na kujiuzulu kwa baraza lote la Mawaziri ili nianze upya kuomba kibali cha kuwaongoza wananchi bila fununu za ufisadi na bila dharau kwa serikali yao.

Pili, natangaza kugandisha (to freeze) akaunti zote za mali za wale waliohusika na shutuma za Richmond, na BoT, pamoja na kushika rehani mali zao zote zisizohamishika kwa nia ya kurudishia serikali mali yoote ambayo inaweza kuwa iliibiwa na washutumiwa. Ili wasife njaa serikali itaendelea kuwalipa nusu mshahara hadi uchunguzi au mashtaka kumalizika.

Tatu, nawahimiza viongozi wote waliojihusisha na ufisadi wowote wa kimsingi kama kwenye mikataba ya madini, Netgroup Solutions, Uuzaji wa Mashirika na Raslimali za Umma, Ununuzi wa rada na ndege ya Rais, Ununuzi wa vifaa vya Jeshi, Mikataba na TANESCO kama IPTL, Kiwira, nk, wakiri kwangu kimaandishi kushiriki kwao na kuorodhesha mali walizopata kutokana na matendo hayo. Wakifanya hivyo sitawachukulia hatua za kisheria ila nitawasimamisha kazi ya umma na kurudisha mali ya wananchi panapohusika.

Wasiojitokeza kwa hiari naagiza vyombo vyote vya uchunguzi vya dola kufuatilia kwa undani na waletwe mbele ya sheria mara moja.

Ndugu wananchi, hii vita dhidi ya wabadhirifu itahitaji ushirikiano wenu na naomba mniunge mkono kwa kila namna.
Nimeagiza vyombo husika kuhakikisha watuhumiwa hawawezi kutoroka au kutorosha mali hadi uchunguzi umalizike. Aidha nimeagiza vyombo vya dola viwe macho kudhibiti wakorofi wachache watakojaribu kuleta ghasia.

Mungu ibariki Tanzania.

Asanteni.

(Anavua miwani, anafuatwa kwenye jukwaa na Makamu wa Rais, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu wa CCM, Chadema, CUF, UDP na kuzingirwa na Chief Justice, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa Polisi na Mkuu wa Magereza. Wanatoka nje ya Bunge kwa hatua kakamavu za kijeshi. Wabunge wanasimama na kumshangilia kwa nderemo na vifujo)!!!!!!

Hii kazi kweli kweli. Watu ni lazima wajisalimishe.
Hiyo imetoka Tanzanet ... hayo ni wishful thinking ya jamaa mmoja; siyo JK
 
Forum statistics

Threads 1,237,962
Members 475,776
Posts 29,308,029