best man!!!

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,653
13,474
wakuu wasalaam!
wakuu ninahitaji tution ya chap chap!
rafiki yangu kanipa heshima ya kuwa best man wake siku ya harusi inayotarajiwa kufanyika siku ya jumapili!
kwa vile issue hii ni muhimu nisingependa nimuangushe rafiki yangu!that is why nikaja kwa wataalamu hapa
mnipatie a,b, cs ya nini majukumu yangu kuanzia kanisani hadi kwenye sherehe itakayofanyika baadaye!!
mi najua kumpepea pepea jasho tu,je yako mengine!!please help!
 
kumchombeza kwa vimaneno vya hapa na pale, pia kumtoa hofu, maana ma bwana harusi wengine ni waoga sana
safi buji nadhani hiyo nitaitumia kwani hata mm itakuwa inaniondoa soo kiaina !!
 
Best man maana yake, mbali na kusimamia suala hilo siku ya tukio, anakuwa ndiye mlezi wa familia hiyo mpya, kwa maana ya kutoa miongozo wakati atakapohitajika, na kuhakikisha kuwa wanandoa hao wanakiishi kiapo chao kama walivyokubaliana kanisani!
 
Kumsaidia asiwe na muhemuko mbele za watu, kama alivyosema Buji, pamoja na kuhakikisha anakula siku hiyo kabla ya kwenda kanisani, na anafanya usafi wa kuridhisha kama kunyoa nk, pia kumkumbusha vitu muhimu vitakavyohitajika siku hiyo kama pete
 
Yaani wewe unakua kama Baunsa wake,
Pia akitoka jasho kidogo unamfuta pamoja na kumuweka koti la suti sawa kama limekaa upande
 
Kwanza kabla ya kusema sijui kumfuta jasho na kumpa company asiwe na woga mbele za watu. Je unaelewa jukumu lako kama best man wa hiyo harusi.
Je unaelewa dhana nzima ya kuwa best man au unafikiri issue inaishia kanisani tuu pale
Ni zaidi ya hilo na ni zaidi ya kuwa mpambe
Ni jukumu kubwa kuwa mshauri wa wanandoa wapya
Kuhakikisha inapotokea migogoro unakuwa wa kwanza kujulishwa na kusuluhisha
Mshauri wa wahusika katika masuala ya familia
 
Back
Top Bottom