Besigye aweka rekodi ya kuwa mtu aliyewahi kukamatwa na Polisi mara nyingi zaidi duniani

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
229
582
Kitabu cha Guiness cha Rekodi za Dunia ambacho huchapishwa kila mwaka kikibeba rekodi za mafanikio ya juu kabisa ya binadamu katika nyanja mbalimbali na maajabu ya asili(Guinness World Book of Records) kimemtangaza Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye kuwa ndie mtu aliyeweka rekodi Duniani ya kukamatwa mara nyingi zaidi na Polisi.

Jumatatu tarehe 20 Januari 2020 alifikisha jumla ya kukamatwa mara 50 ambapo alishikiliwa katika kituo cha Polisi Nalufenya kabla ya kuhutubia wakereketwa wa chama chake katika uwanja wa Bugembe.

Wakati wakijiandaa ghafla vitu havikwenda kama ilivyotegemewa na kujikuta yeye na timu yake wakiingia katika tafrani na Polisi wa vituo vya Jinja, Bugembe na Kakira. Mambo yalizidi kuwa si mambo baada ya Wanajeshi kutoka Barracks za Gadaffi walipofika eneo hilo hadi mabomu ya machozi kutumika.

Kwa mwaka 2016 pekee alikamatwa mara 15 kipindi cha uchaguzi.

Cha kushangaza, Rais huyo mstaafu wa chama cha Forum Democratic Change hajawahi kupewa hukumu hata mara moja ya makosa anayotuhumiwa na kukamatwa nayo.

AE4E45C4-27EE-4143-BA6F-98BED3F27B1D.jpeg
4F5AC084-5451-4E80-B373-3EBCFCDF82AA.jpeg
9EE55274-ED81-4AFE-9919-5207DE464765.jpeg
8D26795C-0651-404D-83D0-FBF614CFA9D5.jpeg
 
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ametajwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama kiongozi aliyekamatwa na polisi mara nyingi zaidi Duniani

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ametajwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama kiongozi aliyekamatwa na polisi mara nyingi zaidi duniani.

Katika taarifa ya kitabu hicho iliyotoka Januari 20, 2020 imeeleza kuwa Besigye amekamatwa mara 50 nchini Uganda, juzi Jumatatu ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa kiongozi huyo kukamatwa na polisi.

Rais huyo mstaafu wa chama cha Forum Democratic Change katika mara 50 alizokamatwa, asilimia 30 ilikuwa mwaka 2016 ambako alikamatwa mara 15.

20200122_180020.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂 waganda watamkumbuka huyu binadamu na kusherehekea maisha yake kuliko M7
 
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ametajwa katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kama kiongozi aliyekamatwa na polisi mara nyingi zaidi duniani

Katika taarifa ya kitabu hicho iliyotoka jana Jumanne Januari 20, 2020 imeeleza kuwa Besigye amekamatwa mara 50 nchini Uganda, juzi Jumatatu ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa kiongozi huyo kukamatwa na polisi

Rais huyo mstaafu wa chama cha Forum Democratic Change katika mara 50 alizokamatwa, asilimia 30 ilikuwa mwaka 2016 ambako alikamatwa mara 15


Chanzo: Mwananchi
 
Kumpiga chura teke ni kumwongezea hatua.. Jamaa kaingia kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia kimaskhara kabisa.. Kukamatwa kumempaisha

Jr
 
Kuna uwezekano Bobby Wine akaivunja record ya Dr Besidye!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom