Bernard Morrison aomba radhi Simba kwa utovu wa nidhamu alioufanya

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison ameomba radhi kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na kwa uongozi wa klabu yake kwa utovu wa nidhamu aliouonyesha.

Imeelezwa kuwa Morrison ambaye ni raia wa Ghana ametumia group la mtandao wa WhatsApp kuomba radhi kwa wenzake kisha akaomba wafikishe salamu kwa uongozi, lakini pia aliutuma ujumbe huo pia kwa viongozi.

Mchezaji mmoja wa Simba ameeleza kuwa Morrison ambaye alidaiwa kutoroka kambini wiki iliyopita, kisha kusimamishwa na uongozi wa klabu kutokana na kufanya matukio ya kujirudia, anajutia makosa yake aliyoyafanya lakini uongozi haujatoa jibu lolote kwake hadi sasa, na hata wachezaji wenzake hawajamjibu chochote.

Simba wapo katika mchakato wa kujiandaa na mchezo wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Jumapili Februari 13, 2022.

Source: Mwanaspoti

morrison-pic-data.jpg
 
Ile post yake ya something huge ilikuwa ni mbwembwe kuonesha mchizi ana plan B

Lakini baada ya GSM kujitoa udhamini na mfululizo wa malalamiko kutoka Yanga jamaa amefikia maamuzi mazuri kaweza kuzisoma alama za nyakati

Kagundua wazo la kurudi yanga ni wrong move
 
Huyo ameshasaini mkataba wa awali huko Utopolo asituchanganye aende huko kwa wavuta bangi wenzake
 
"haa bana nugu nugu ni mtu mbaya sana,ananifundisha mimi kiswahili ya matusi bana"
Nikasema"hii maweee"Nungungungu atatuharibia huyu mtu.
 
yaani akiruhusiwa kurudi kambini tuu, atawaraghai wachezaji woote na mwisho wa siku simba itafungwa na kila itakayo kutana nayo...
 
Back
Top Bottom