Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Watanzania mkae macho na mkae chonjo. Nafunga bao la Ushindi dakika ya 89 kwenye Uchaguzi huu 2020

Hii hotuba aliyoitoa Membe nahisi itakuwa katumwa na wazee wa kazi kuiunganisha CCM ili ngosha aonekane hakukosea alipomkata chamani.

Habari yenyewe hii hapa

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe, amesema kuwa kabla hajafukuzwa na chama chake cha awali cha CCM, alikuwa anao mpango wa kukipindua chama hicho kiuongozi kwa kushirikiana na watu wengine sita na alikuwa na jumla ya wabunge 78.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba, 19, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo pia ameeleza mustakabali wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 28 ,mwaka huu, kwa kuuaminisha umma wa Watanzania kuwa yeye ndiye mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo.

"Mimi nilikuwa CCM nikatataka kukabiliana na rais aliyepo madarakani peke yangu kumuondoa, lakini washukuru walinifukuza, tulijianda na wana CCM wenzangu, achilia mbali tulikuwa watu 6 tuliokuwa tayari kuiondoa Serikali madarakani, mimi nilikuwa na wabunge 78, kwa bahati mbaya 46 wamefyekwa lakini wako CCM, 32 wamebaki hata mkininyonga siwezi kuwataja kwa sababu watatumbuliwa tu", amesimulia Membe.

Aidha Membe ameongeza kuwa, "Kuungana kwa vyama vya upinzani ni lazima chama tawala kipasuke ili kundi la pili lije upande wa pili ili kusaidia chama tawala kuangushwa CCM mwisho wake umefika na tunawaondoa madarakani Oktoba 28".
 
ZITTO ni sumu Kali, tumuogope zaidi ya Corona.

ZITTO alipanga na maccm kumleta Membe ACT Sharif Hamadi aliahamsitukia kitambo.
 
..mbona magufuli amekuwa akifanya kampeni makanisani na misikitini tangu aingie madarakani?

..mbona ccm imekuwa ikipigiwa kampeni na viongozi wa dini na ktk kampeni hizi?

..kamati ya amani ya viongozi wa dini iko kwa ajili ya ccm, au kwa ajili ya nchi, na vyama vyote vya siasa?

..Watanzania tuache UNAFIKI. kuliko kuendelea kuwafanya viongozi wa dini kuwa miliki ya ccm, ni bora tukawapa uhuru kukampeni waziwazi kwa yeyote wanayemuunga mkono.
Membe kwa background yake anajua anazungumza nini , nimemuelewa ndio maana nikastress hiyo point,

Ni hatari sana kutumia hiyo kete, tunachezea moto karibu na tank ya mafuta.

Hili jambo liachwe mara moja.
 
Membe haieleweki kwakweli yani anapepesuka pepesuka na hivyo kasikia kuwa zitto anaunga mkoo juhudi za lissu ndo anazidi kupagawa ..
 
Membe kwa background yake anajua anazungumza nini , nimemuelewa ndio maana nikastress hiyo point,

Ni hatari sana kutumia hiyo kete, tunachezea moto karibu na tank ya mafuta.

Hili jambo liachwe mara moja.
Moto uwake tu hatuna cha kupoteza sisi..ccm ishatupa mateso hadi yamekuwa sehemu ya maisha yetu.

Wanaoogopa ni wenyenacho wanaojisifu wanatembelea v8. Sisi wanyonge hatuna cha kupoteza zaidi ya unyonge wetu.
 
Kama una akili timamu na umemsikiliza Mheshimiwa Membe ,inataka juha aliebobea ndio atapata ugumu kwa alivyoianika CCM ,ameivua nguo hazarani.

Amezungumza ukweli mtupu,jamaa ni kiboko ukimuona unaona yupo poa kabisa,lakini uamuzi wa kuichambua serikali kiaina ,imezidi kuhamisha kura za CCM na kuzielekeza kwa kupelekwa.

Hongera membe ,CCM wamekimbiwa na wasanii wamekusanya viongozi wa dini nao wapo njiani kuwatoroka.

Sasa ni kweli CCM inazama katika bahari kuu.
 
Nimesikia kauli ya bw. Membe kwa jinsi alivyo na msimamo thabiti usiyoyumba...biashara ya kuyumbishwa yumbishwa Kama aliyofanyiwa Dr Slaa kipindi kile hataka kuisikia..kwa sababu kipindi kile walikuwa wameshajipanga ukawa, mara akaletwa mzee wa safari ya matumaini ghafla..wakavurugana wenyewe kwa wenyewe.

Sasa same case aliyokuja nayo Lissu..mzee Membe hataki hiyo biashara na nimempenda amekiri kwamba vyama hivi vya upinzani Bado vichanga..kete ya Urais kiukweli Bado Sana, ila wanaweza kujitahidi wakapata wabunge wabunge kadhaa..kwa sababu ndio mwanzo....big up kwa msimamo wako huo. Ningeshangaa Membe na diplomasia na ukongwe wote alionao eti am support Lissu..mtoto wa juzi. Ni ajabu na kweli.
 
Walisema watu binafsi Zitto na Maalim Seif, hakikusema chama! Ndivyo alivyosema Membe. Inamaanisha kuwa hakuna siku yoyote ambayo chama kilikaa na kukubaliana kumuunga mkono Lissu
Kwaiyo Membe hamuheshimu Zitto na Maalim seif anataka kuleta mpasuko kwa kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Zitto na Mwenyekiti wa Chama chake Maalim Seif
 
Membe hana issue anataka kupunguza kura za rais Tundu Lissu ccm iendelee kupeta, tayari kashakula mlungula
 
Labda naye hawaheshimu kwa kumpigia kampeni wa chama kingine. Jambo ambalo ni nadra sana kwa viongozi wa juu kushabikia mgombea wa chama kingine.

Mrema alianza mwaka 2015 kumpigia debe wa chama kingine na kubezwa sana, kumbe wapo wengi. Yetu macho na masikio
Kwaiyo Membe hamuheshimu Zitto na Maalim seif anataka kuleta mpasuko kwa kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Zitto na Mwenyekiti wa Chama chake Maalim Seif
 
Maalim Seif nimemwelewa sana leo,huyu jamaa kavuruga hesabu zote; Inawezekana mzee wetu kachero goli lake la dakika 89 lilikuwa ni kuvuruga upinzanii kwa kumuunga mkono kiongozi wa chama kijani
 
Maalim Seif nimemwelewa sana leo,huyu jamaa kavuruga hesabu zote; Inawezekana mzee wetu kachero goli lake la dakika 89 lilikuwa ni kuvuruga upinzanii kwa kumuunga mkono kiongozi wa chama kijani
Tena pengine angetangaza kumuunga mgombea wa kijani kwenye jukwaa moja na lissu akiwemo-na angekuwa ameharibu kampeni ya mwisho ya hapa Dar kutokana na taharuki.
 
Back
Top Bottom