Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973

Membe anahoji:

"Je Tupo tayari kwenda kwenye Uchaguzi bila kuwa na tume huru?

Tume huru ya Uchaguzi ndugu zangu, maana yake ni kwamba uwe na Tume katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ambayo ina watu wa aina zote. Wa dini zote, vyama vyote, aina zote za Elimu, Wanasiasa Maarufu bila kujali chama Tawala, Wanakuwa kwenye hilo kundi.

Ili wanapo amua kuhusu Mwanachama anayeomba Udiwani au Ubunge, apitishwe bila Upendeleo.

Sasa mtu mmoja akaniuliza, "Kwani huko nyuma Mheshimiwa mlipitishwaje?". Nikasema tulipitishwa kwa utaratibu huo huo lakini katika mazingira ya sasa hivi, ambayo Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa au Mkurugenzi, anajisikia hofu kwamba akipita Mtu wa Chama kingine Cheo chake kinaweza kuondoka, anaweza akafanya vitendo vya Upendeleo kulinda Masrahiya cheo chake.

Kwahiyo katika Mazingira ya sasa lazima tuwe na Tume Huru.

Nikawa najiuliza, hili swala la Tume huru tunafanyaje? Twende nalo hivyo hivyo au tuwe na Tume huru? Jibu likawantiwe na tume huru.

Nikawa pia najiuliza kwamba safsri hii tumeambiwa Waangalizi wa Uchaguzi wa dunia( International observers) hawatakuwepo kwa sababu UNDP hajatoa fedha za Uchaguzi, hawatakuwepo sababu wengi wanahofia Corona.

Je, tupo tayari kwenda kwenye Uchaguzi katika mazingira ya kutokuwa na Waangalizi wa Uchaguzi kutoka kote Duniani watakao Sema Uchaguzi huu ulikuwa wa haki, ulikuwa huru na unao heshimika, tupo tayari kufanya hivyo bila kuwa na Waangalizi wale?

Nikawa najiuliza haya Maswali. Wakati fulani nikasema, inawezekana Uchaguzi huu hautafanyika karibuni utafanyika baadae.

Lakini Wanasiasa wengine wakasema hapana, tukazanie moja tu la kuwa na Tume Huru na kuwa na Waangalizi wa Uchaguzi. Mambo Mawili lakini tuendelee kuwa na Uchaguzi.

Sasa ndo maana tukachukua wiki nzima toka wiki iliyopita, kuongea na Wanasiasa ndani ya Chama na nje ya chama watupe Mwanga wa nini kifanyike".

Pia soma:

Elections 2020 - Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama
 
2434257_987098.jpg

Uongozi wa vyombo vya dola?!!
 
Jecha alifuta, matokeo na Maalim alisusia uchaguzi na hakuna lililobadilika.. Shein amepiga miaka yake mitano saafi kabisa.. Ukisusa wenzio wala na hakitafanyika kitu.
 
Na ufe tu, upinzani gani wa kudai tume huru ukikaribia uchaguzi, kwa nini hawakudai tangu mwanzo? wameshaona mambo yanaenda kombo wanatafuta njia ya kutokushiriki uchanguzi.
Nina mashaka na utimamu wa akili zako.

Wewe na wajinga wenzako mnadhani kazi ya kudai tume huru inatakiwa kufanywa na wapinzani au wanasiasa kumbe hilo ni jukumu la kila mwananchi mwenye mapenzi mema na nchi yake.
 
Kwanza ni aibu kwa wapinzani kushiriki uchaguzi while Hakuna Tume Huru ya uchaguzi kama walivokua wanaidai huko nyuma ....pili inasikitisha sana eti tunataka waangalizi wa kimataifa ...

Mnadhan watawashinda wana Lumumba kwa propaganda!? Shida Tanzania sijaona wapinzani wa kweli wote wapiga dili tu Ccm itatawala miaka 1000.
 
Upinzani kwa sasa unaweza kuyumba sana na ukawa kama umepotea kabisa but unaweza kuja ku gain momentum hata baada ya miaka 10 ijayo na ukaking'oa chama tawala madarakani......
hizi ni hesabu za nyakati.....
wachache sana wanaweza nielewa.....
 
Na ufe tu, upinzani gani wa kudai tume huru ukikaribia uchaguzi, kwa nini hawakudai tangu mwanzo? wameshaona mambo yanaenda kombo wanatafuta njia ya kutokushiriki uchanguzi.
madai ya tume huru yameanza 2020 kakaribia uchaguzi? kama member wa JF anakuwa hivi namna hii,hoko nje kukoje
 
Nina mashaka na utimamu wa akili zako.

Wewe na wajinga wenzako mnadhani kazi ya kudai tume huru inatakiwa kufanywa na wapinzani au wanasiasa kumbe hilo ni jukumu la kila mwananchi mwenye mapenzi mema na nchi yake.
Wewe ndiyo akili yako haina akili, haiwezekani udaganywe na wapinzani kudai tume huru sasa wakati uchaguzi uko karibu. Kwa nini hawakudai tangia mwanzo? Hata huu uchuguzi ukimalizika hawatadai tume huru ila ukikaribia uchaguzi mwingine wataanza makelele ya kudai tume huru.
 
Narudia tena kukwambia
Kazi ya kudai tume huru ya kila mwananchi mwenye akili timamu, wewe endelea kukaa na tumbo lako usubiri wapinzani wadai tume huru kwa niaba yako
 
Naiona roho ya Membe ndani ya Nyalandu kama maandalizi ya asali ya kumpata mgombea sahihi wa kuipeperusha bendera ya CDM.
 
Jecha alifuta, matokeo na Maalim alisusia uchaguzi na hakuna lililobadilika.. Shein amepiga miaka yake mitano saafi kabisa.. Ukisusa wenzio wala na hakitafanyika kitu.
Membe aruhusiwe kijipima na Rais
 
Narudia tena kukwambia
Kazi ya kudai tume huru ya kila mwananchi mwenye akili timamu, wewe endelea kukaa na tumbo lako usubiri wapinzani wadai tume huru kwa niaba yako
Utakuwa na matatizo ya kufikiri, kwa Tanzania watu wengi wanataka tume huru lakini tatizo ni wapinzani wanyewe hawana "support" toka kwa wananchi kwa sababu upinzani wenyewe wako kwa ajili ya matumbo yao(wapiga dili) na hawako kwa ajili ya wananchi ndiyo maana wanaombea mabaya kwa nchi na si maendeleo.
 
Jecha alifuta, matokeo na Maalim alisusia uchaguzi na hakuna lililobadilika.. Shein amepiga miaka yake mitano saafi kabisa.. Ukisusa wenzio wala na hakitafanyika kitu.
je kwa tume ya akina jecha kuna tofauti itakayo patikana kati ya kususa na kushiriki??? tafakari ni heri kususa kulikokusumbua wanakuunga mkono maana mwisho ni hasira kali au we unavyofikira ⚖ ⚖
 
Back
Top Bottom